Serikali "yasalimu amri" kwa Nimrod Mkono, TRA yafungua minyororo yake siku ya Sikukuu


barafu

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Messages
6,282
Likes
25,803
Points
280
barafu

barafu

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2013
6,282 25,803 280
image-jpeg.364110
image-jpeg.364108Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana imezifungua ofisi za Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, ikiwa ni siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.

TRA waliwasili katika jengo la ofisi hizo zilizoko katika jengo la Bank ya Exim iliyoko jijini Dar es Salaam (ingawa ilikuwa sikukuu), pamoja na Kampuni ya udalali ya Yono na kuzifungua ofisi hizo mbele ya Nimrod Mkono na binti yake.

Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amekiri kufunguliwa kwa ofisi hizo. Kayombo amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya pande mbili na ahadi ya kufanya malipo iliyowekwa na mkono.

“Ni kweli muda upo tuliokubaliana lakini hatutaki uwe katika vyombo vya habari, kutokana na nia ya dhati aliyoonesha Mkono ndio maana tumekubaliana nae,” Kayombo anakaririwa.

Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa ingawa Mkono amefungiwa ofisi zake akidaiwa kodi ya shilingi bilioni 1, yeye anaidai Serikali takribani shilingi bilioni 9 kwa kazi alizofanya ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Chanzo: Mpekuzi
 
talentizo

talentizo

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Messages
462
Likes
107
Points
60
Age
33
talentizo

talentizo

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2014
462 107 60
Maana yake anamalimbikizo ya miaka mingi
 
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2016
Messages
1,469
Likes
1,809
Points
280
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2016
1,469 1,809 280
Hapana mkuu. Hii inaitwa "Mbuzi wa Bwana Heri kala mahindi ya Bwana heri". TRA wanamdai Nimrod mkono 1b, na yeye anaidai serikali 9b.
N a ndiyo maana wamecompromise, Tanzania buana!!
 
T

TKNL

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Messages
624
Likes
486
Points
80
T

TKNL

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2012
624 486 80
Serikali inatu-let down walipa kodi wadogo. Hii ni kuset bad example kwamba ukiwa na pesa unaweza kukwepa kodi na usifanywe kitu. Walitakiwa wakomae huyo jamaa alipe kodi yetu, pesa si anayo?

Hiyo ya kuidai serikali ni issue nyingine ambayo na yeye alitakiwa akomae serikali imlipe, asitumie deni kukwepa kodi.
 
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2016
Messages
1,469
Likes
1,809
Points
280
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2016
1,469 1,809 280
Umeona eeh? Hii nchi ngumu. Sheria ziko kwa ajili ya baadhi ya watu, si kila mtu
Tycoon 'wanaombwa' na kubembelezwa walipe kodi, walala hoi wanakamuliwa hadi utumbo
 
sirluta

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Messages
6,127
Likes
1,471
Points
280
sirluta

sirluta

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2012
6,127 1,471 280
Huyu mzee si ndo tumesikia kwenye historia kuwa alikwapua mabilion BOT halafu akahama nchi hadi Nyerere alipokufa?? Kama anaidai serikali alipataje hizo tender akiwa kiongozi?
 
Obuma

Obuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Messages
2,724
Likes
5,051
Points
280
Obuma

Obuma

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2015
2,724 5,051 280
Uzi wa Nimrodi ulipokuja hapa kuhusu kudaiwa watu walitokwa povu, tulieleza wazi serekali hii isiyokuwa na umakini hadi kwenye teuzi za balozi wa nyumba kumi inaenda kucheza na mwanasheria wa kiwango cha Nimrodi?

Wenye akili tukaliweka wazi kina lizaboni na wale nyumbu wa kijani wakaja na kushangilia serekali inashika hadi mapapa.

Kwa mtu ambaye ameshaijui hii serekali anaelewa,yaani hujijui hata unachofanya unaenda kumparamia gwiji wa sheria?

Balozi kuteua tu shida, mkanganyiko kibao leo unaenda kuhangaika na gwiji wa sheria?

Naona kuwadhalilisha zaidi kawaambia nataka muifungue siku ya sikukuu. Yaani nimrodi ni noma tena na akaenda na mtoto kumuonyesha mwanae unatakiwa uwe jasiri namna hii.

Siku ya sikukuu wafanya kazi wa TRA wanaenda kazini kufungua ofisi ya mtu binafsi?Kwani Nimrodi alikuwa anaulazima gani wa kuingia ofisini siku ya sikukuu?

Ukiangalia vizuri utagundua aliwalazimisha kwa vifungu na ili kuwaonyesha yeye ni nani.Naona mambo yanaiva.
 
kilambalambila

kilambalambila

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Messages
7,957
Likes
4,193
Points
280
kilambalambila

kilambalambila

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2013
7,957 4,193 280
Sasa serikali esalimuje amri hapo? Ushabiki mwingine bwana
 

Forum statistics

Threads 1,238,383
Members 475,954
Posts 29,318,894