Serikali "yasalimu amri" kwa Nimrod Mkono, TRA yafungua minyororo yake siku ya Sikukuu

Hapana mkuu. Hii inaitwa "Mbuzi wa Bwana Heri kala mahindi ya Bwana heri". TRA wanamdai Nimrod mkono 1b, na yeye anaidai serikali 9b.

Hapo kujifanya mjuaji kwa anayekudai mbele za watu lakini baadae unamfata umempigia magoti.
 
Hapo kujifanya mjuaji kwa anayekudai mbele za watu lakini baadae unamfata umempigia magoti.
Sure. Nadhani tuna shida ya kimfumo. Huenda Mkono aliwaambia TRA kwamba hajalipwa pesa zake na Govt, ailipwa atawalipa. Hapo lazima TRA wakae, kwa sababu client ambaye ni Govt anadai 1.1 billion kwa Mkono advocates ilhali, mdaiwa Mkono anaidai govt 9 billion. Hii nchi ngumu sana. Ukituatilia masuala haya unaweza kufa kwa presha
 
Hahaha, asee Ccm wamegonga mwamba kwa Mkono, siku nyingine muache kukurupuka maana mnatia aibu sasa
 
Sure. Nadhani tuna shida ya kimfumo. Huenda Mkono aliwaambia TRA kwamba hajalipwa pesa zake na Govt, ailipwa atawalipa. Hapo lazima TRA wakae, kwa sababu client ambaye ni Govt anadai 1.1 billion kwa Mkono advocates ilhali, mdaiwa Mkono anaidai govt 9 billion. Hii nchi ngumu sana. Ukituatilia masuala haya unaweza kufa kwa presha
Nimekuelewa sana ndugu...
 
Serikali inatu-let down walipa kodi wadogo. Hii ni kuset bad example kwamba ukiwa na pesa unaweza kukwepa kodi na usifanywe kitu. Walitakiwa wakomae huyo jamaa alipe kodi yetu, pesa si anayo?

Hiyo ya kuidai serikali ni issue nyingine ambayo na yeye alitakiwa akomae serikali imlipe, asitumie deni kukwepa kodi.

Sasa kodi inatakiwa kutoka kwenye hizo hela anazoidai serikali...yeye hajalipwa...anatoa wapi hela ya kulipa TRA?
 
Sasa kodi inatakiwa kutoka kwenye hizo hela anazoidai serikali...yeye hajalipwa...anatoa wapi hela ya kulipa TRA?
Kwani wote wanaolipa kodi hawaidai serikali? Muulize Bakhresa, Mengi, Manji na matajiri wengi kama hawatakwambia wana madai serikalini, ina maana na wao wakatae kulipa kodi? Halafu tabia ya kutetea kutolipa kodi mmeitoa wapi? Upinzani wa Tanzania unatia aibu mno!!!
 
Huyu kweli kakarupuka. Nitakuwa nimefanya kosa kumuita jina la wale wa UDOM. Kwa maelezo yako hapo serikali imesalimu amri wapi?
 
Uzi wa Nimrodi ulipokuja hapa kuhusu kudaiwa watu walitokwa povu, tulieleza wazi serekali hii isiyokuwa na umakini hadi kwenye teuzi za balozi wa nyumba kumi inaenda kucheza na mwanasheria wa kiwango cha Nimrodi? Wenye akili tukaliweka wazi kina lizaboni na wale nyumbu wa kijani wakaja na kushangilia serekali inashika hadi mapapa.Kwa mtu ambaye ameshaijui hii serekali anaelewa,yaani hujijui hata unachofanya unaenda kumparamia gwiji wa sheria? Balozi kuteua tu shida, mkanganyiko kibao leo unaenda kuhangaika na gwiji wa sheria? Naona kuwadhalilisha zaidi kawaambia nataka muifungue siku ya sikukuu. Yaani nimrodi ni noma tena na akaenda na mtoto kumuonyesha mwanae unatakiwa uwe jasiri namna hii. Siku ya sikukuu wafanya kazi wa TRA wanaenda kazini kufungua ofisi ya mtu binafsi?Kwani Nimrodi alikuwa anaulazima gani wa kuingia ofisini siku ya sikukuu? Ukiangalia vizuri utagundua aliwalazimisha kwa vifungu na ili kuwaonyesha yeye ni nani.Naona mambo yanaiva.
Ndugu yangu watu wamebebwa na upofu wa mahaba hata kwenye mambo ambayo hata mtoto wa miaka mitatu anaweza kuona ukweli
 
Nimrod Mkono ndio alimuhonga Mbowe milioni 20 asiweke mgombea ubunge Musoma Vijijini... Mbowe anapenda sana pesa bado amelamba kwa lowasa bilioni 10
 
Hhahaaha kwahio Mhujumu uchumi amepewa muda wa kujirekebisha??
 
Kwani wote wanaolipa kodi hawaidai serikali? Muulize Bakhresa, Mengi, Manji na matajiri wengi kama hawatakwambia wana madai serikalini, ina maana na wao wakatae kulipa kodi? Halafu tabia ya kutetea kutolipa kodi mmeitoa wapi? Upinzani wa Tanzania unatia aibu mno!!!

Ile tu kwamba TRA wameharakisha kuifungua hiyo ofisi siku ya sikukuu inaonyesha walishikwa pabaya. Mimi sitetei kutokulipa kodi..na nilivyosikia mara ya kwanza wameifunga ofisi hiyo kwa kutokulipa kodi nikawapongeza TRA...sasa kumbe serikali haijamlipa..ni aibu hii. Sasa labda nikuulize wewe A: hii tabia ya kutetea serilali kutokulipa madeni yake umeitoa wapi? B: hii dhana ya kumuita mtu yeyote ambaye ana mawazo tofauti na wewe mpinzani umeitoa wapi?

Jua kwamba tupo wengine hatufungani na vyama. CCM ikifanya vizuri..tunaipongeza..ikikosea...tunaikosoa. na UKAWA wakifanya vizuri..tunawapongeza...wakikosea..tunawakosoa.
 
Back
Top Bottom