Serikali "yasalimu amri" kwa Nimrod Mkono, TRA yafungua minyororo yake siku ya Sikukuu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg
image.jpeg



Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana imezifungua ofisi za Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, ikiwa ni siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.

TRA waliwasili katika jengo la ofisi hizo zilizoko katika jengo la Bank ya Exim iliyoko jijini Dar es Salaam (ingawa ilikuwa sikukuu), pamoja na Kampuni ya udalali ya Yono na kuzifungua ofisi hizo mbele ya Nimrod Mkono na binti yake.

Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amekiri kufunguliwa kwa ofisi hizo. Kayombo amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya pande mbili na ahadi ya kufanya malipo iliyowekwa na mkono.

“Ni kweli muda upo tuliokubaliana lakini hatutaki uwe katika vyombo vya habari, kutokana na nia ya dhati aliyoonesha Mkono ndio maana tumekubaliana nae,” Kayombo anakaririwa.

Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa ingawa Mkono amefungiwa ofisi zake akidaiwa kodi ya shilingi bilioni 1, yeye anaidai Serikali takribani shilingi bilioni 9 kwa kazi alizofanya ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Chanzo: Mpekuzi
 
Serikali inatu-let down walipa kodi wadogo. Hii ni kuset bad example kwamba ukiwa na pesa unaweza kukwepa kodi na usifanywe kitu. Walitakiwa wakomae huyo jamaa alipe kodi yetu, pesa si anayo?

Hiyo ya kuidai serikali ni issue nyingine ambayo na yeye alitakiwa akomae serikali imlipe, asitumie deni kukwepa kodi.
 
Huyu mzee si ndo tumesikia kwenye historia kuwa alikwapua mabilion BOT halafu akahama nchi hadi Nyerere alipokufa?? Kama anaidai serikali alipataje hizo tender akiwa kiongozi?
 
Uzi wa Nimrodi ulipokuja hapa kuhusu kudaiwa watu walitokwa povu, tulieleza wazi serekali hii isiyokuwa na umakini hadi kwenye teuzi za balozi wa nyumba kumi inaenda kucheza na mwanasheria wa kiwango cha Nimrodi?

Wenye akili tukaliweka wazi kina lizaboni na wale nyumbu wa kijani wakaja na kushangilia serekali inashika hadi mapapa.

Kwa mtu ambaye ameshaijui hii serekali anaelewa,yaani hujijui hata unachofanya unaenda kumparamia gwiji wa sheria?

Balozi kuteua tu shida, mkanganyiko kibao leo unaenda kuhangaika na gwiji wa sheria?

Naona kuwadhalilisha zaidi kawaambia nataka muifungue siku ya sikukuu. Yaani nimrodi ni noma tena na akaenda na mtoto kumuonyesha mwanae unatakiwa uwe jasiri namna hii.

Siku ya sikukuu wafanya kazi wa TRA wanaenda kazini kufungua ofisi ya mtu binafsi?Kwani Nimrodi alikuwa anaulazima gani wa kuingia ofisini siku ya sikukuu?

Ukiangalia vizuri utagundua aliwalazimisha kwa vifungu na ili kuwaonyesha yeye ni nani.Naona mambo yanaiva.
 
Back
Top Bottom