Serikali "yasalimu amri" kwa Nimrod Mkono, TRA yafungua minyororo yake siku ya Sikukuu

Kosa vyote ila sio akili. Safari ya kufikia Tanzania ya viwanda kwa akili hizo ni mpaka Yesu Kristo atakaporudi

Ndio tutafika kwa kufunga biashara ? Viwanda sio nyimbo na maneno...ni sera madhubuti iliyo buniwa na wataalam baada ya kungalia mazingira tuliuo nayo.
Ni sera ambayo inaangalia jee ni viwanda gani tunahitaji na vitakua na kufanikiwa kutoa ajira na kusaidia kununua bidhaa zetu zilizopo hapa Tanzania.
Viwanda ni pamoja na kuwa na sera madhubuti ya kupunguza gharama za uzalishaji ikiwa,o umeme wa bei ya chini hasa tunapo kuwa na desi yetu wenyewe ...

Kama wewe uneona hio sera ya viwanda tutai ekeleza vipi ...tunaomba utuwekee hapa jamvini yuichambue....
 
Hao freemason waliingiaje kwenye huu uzi? Maana thinking yako katika hili imenifanya nione kuwa viongozi wetu wana kazi nzito
 
Mkono ni kati ya watu walioingizia inshi hii hasara kubwa,kesi zote anazoitetea serikali lazima ashindwe huku akiwachaji rate za doller lukuki tena kwa lisaa! Madai anoyoidai serikali yafanyiwe Auditing utakuta apo anadai interest kwa kutolipwa kwa wakati etc.
 
Mkuu kwenye hii kesi inaonyesha wazi kabisa kwamba mkono hajakwepa. Hapa inaonyesha kwamba kodi anayodaiwa inatokana na kazi ambayo ameifanyia serikali..na serikali haijamlipa. Yani wewe jiulize...tangia lini TRA waharakishe kumfungulia mtu ofiso yake siku ambayo siyo ya kazi kiserikali? Hapa ni wazi kabisa walishtukia kwamba wao ndio wamebugi wakaharakisha kuifungua hiyo ofisi kabla hawajashtakiwa mahakamani. Kwahiyo mimi sisemi mkono akwepe kodi..ila serikali imlipe kwanza halafu ndio imbane. Au bora zaidi wakate hiyo kodi yao wampe albaki.

Tangia lini kodi ikaahirishwa kulipwa eti kisa unaidai serikali?? Hii ni kwa Tanzania tu. Km anachelewesha kulipa kodi,wamchaji interest na yeye km mkataba wake unasema serikali ikichelewa awachaji interest then iwe hivyo.
 
Makubaliano gani ambayo mhalifu anafanya na TRA na yakakubalika mpaka wafungue ofisi mbele yake tena siku ya sikukuu.?
 
Kodi inatakiwa ulipwe ndani ya mda stahiki inakuaje wamuache eti kisa anaidai serikali?? Hii ni hapa bongo tu! Kodi ni statutory and no negotiable debts.
Sasa mkuu kodi si unalipa baada ya kupata kipato kama ni mfanyabishara? Sasa wakili mkono kafanya biashara na serikali na haijamlipa je hiyo pesa ya kulipa kodi ataitoa wapi?
 
MAKUBALIANO YAKUFUNGA MNAYAFANYA KWENYE VUOMBABYAJABARI KUUFUNGULIWA MNAYAFANYA Sri
 
Sasa mkuu kodi si unalipa baada ya kupata kipato kama ni mfanyabishara? Sasa wakili mkono kafanya biashara na serikali na haijamlipa je hiyo pesa ya kulipa kodi ataitoa wapi?

Ndio maana ofisi ilifungwa,na huo ndio utaratibu!!serikali km haijamlipa sio Tatizo la TRA,yeye akadai huko serikalini. Ndio maana kuchanganya siasa na kazi mambo hayaendi,ona ss siasa imetumika jamaa wamefungua ofisi mchana kweupe.
 
TRA siku hizi ni Private entity? Ccm kwa Vi.la.za hamjambo! Wewe ni ki.la.za grade one,mwendikasi!
 
Mbuzi wa mwenye shamba kala shamba la mwenye mbuzi.
 
Hao freemason waliingiaje kwenye huu uzi? Maana thinking yako katika hili imenifanya nione kuwa viongozi wetu wana kazi nzito

Wamefikaje ? Basi thinking yako ina walakini.....ukisema usichezee freemason, maana ake bila shaka mtuhumiwa ni memba mzuri wa kuaminika wa fm....
Jaribu ku think kabla ya kuandika
 
TRA siku hizi ni Private entity? Ccm kwa Vi.la.za hamjambo! Wewe ni ki.la.za grade one,mwendikasi!
Hahaha daah udom kumbe Mpo umu JF! Unadhani kwa kua TRA ni ya serikali na serikali inadaiwa ndio wanetoff deni au mkono asilipe kodi kisa anaidai serikali? Wewe sheria za kodi huzijui,na ITA huijui,na napoteza mda kujipu mpuuzi wa div five km wewe.
 
View attachment 364110 View attachment 364108

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana imezifungua ofisi za Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, ikiwa ni siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.

TRA waliwasili katika jengo la ofisi hizo zilizoko katika jengo la Bank ya Exim iliyoko jijini Dar es Salaam (ingawa ilikuwa sikukuu), pamoja na Kampuni ya udalali ya Yono na kuzifungua ofisi hizo mbele ya Nimrod Mkono na binti yake.

Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amekiri kufunguliwa kwa ofisi hizo. Kayombo amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya pande mbili na ahadi ya kufanya malipo iliyowekwa na mkono.

“Ni kweli muda upo tuliokubaliana lakini hatutaki uwe katika vyombo vya habari, kutokana na nia ya dhati aliyoonesha Mkono ndio maana tumekubaliana nae,” Kayombo anakaririwa.

Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa ingawa Mkono amefungiwa ofisi zake akidaiwa kodi ya shilingi bilioni 1, yeye anaidai Serikali takribani shilingi bilioni 9 kwa kazi alizofanya ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Chanzo: Mpekuzi
Walifunga mchana wakafungua usiku wa manane!
 
Back
Top Bottom