Serikali yapiga Marufuku Uhamisho wa Watumishi

Serikali yapiga Marufuku Uhamisho wa Watumishi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Waziri wa Nchi, OR Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema, "Kumekuwa na maombi mengi sana ya baadhi yetu kuomba kubadilisha vituo vya kazi. Nitoe rai, hatutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa sasa. Nafasi zote zimetolewa kulingana na uhitaji wa kila halmashauri au mwajiri husika."

Amesma hayo leo Januari 30, 2026 wakati akizungumza na Wanahabari Jijini Kwenye Ofisi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Pia Soma: KERO - Kuna kero kubwa ya Mkwamo wa vibali vya uhamisho (Utumishi HQ) kwa Watumishi walioomba kuhamia vituo

 
Kwa nini watu wanalazimishwa kufanya kazi maeneo wasiyoyataka??
 
My Take
Kumekuwa na tabia ya watumishi waliopangiwa kazi mfano Nkasi au Malinyi au Kyerwa huko Kuhama Kwa visingizio mbalimbali.

Ambae hataki kazi aache arudi kwao Dar
Screenshot_20260131-071722.jpg
 
Mda mwingine sio fair. Mtu anaomba kazi anaandika anapenda kupangwa Dodoma, halafu wewd unaamua kumpanga Handeni. Wakati huo huo kuna mtu ametoka Handeni au Tanga, unamrusha Dodoma.

Sasa huo si uonevu?
Wewe uchague mahala pa kufanyia kazi kama nani? Kazi unapelekwa popote hutaki acha kusaini mkataba na kiapo
 
Back
Top Bottom