Serikali yaongeza kodi kwenye Betting

Serikali yaongeza kodi kwenye Betting

View attachment 3366167
Serikali imeongeza kiwango cha kodi kwa washindi wa michezo ya kubashiri (Betting) ambapo Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema Ongezeko la kiwango hiko cha fedha kitakachopatikana, asilimia 70 itaenda katika mfuko wa serikali kupambana na Ukimwi na asilimia 30 kuchangia mfuko wa bima ya afya.

“Kufanya marekebisho kwenye sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41. Kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15,” amesema Waziri Mwigulu Nchemba bungeni Dodoma leo wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026. ✍️
Hapo kwenye Ukimwi na Bima ya Afya weka wizi, starehe na matumbo!
 
Kumbe vitu haramu vinawaingizia sana Kodi 🤣🤣
 
yaani mwigulu bana hii wizara haimfai kwasababu ana conflict of interest..imagine yeye kwasababu ana kampuni ya betting kaondoa kodi ili apate zaidi halafu kwa washindi wa betting kawabana kodi
 
yaani mwigulu bana hii wizara haimfai kwasababu ana conflict of interest..imagine yeye kwasababu ana kampuni ya betting kaondoa kodi ili apate zaidi halafu kwa washindi wa betting kawabana kodi
Aibu kubwa ila Mungu wetu yupo kazini
 
Back
Top Bottom