WanaJF,
Serikali kupitia wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imemzawadia Mbwama Samatta kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 1200 (Lowa Density) chenye thamani ya pesa za kitanzania milioni 20 maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Zawadi hiyo imefuatia heshima kubwa ambayo kijana Mbwana Samatta ameipatia taifa kwa kushinda tuzo la mwana soka bora wa mwaka kwa wachezaji wa ndani ya Afrika.
Akizungumza na chanzo chetu cha habari waziri mwenye dhamana ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ameeleza kuwa, kijana Samatta hakika anastaili kupata zawadi hiyo kutoka kwa serikali kwa heshima kubwa ambayo ameipatia Tanzania hususani kwenye soka la kimataifa.
Aidha, wadau mbalimbali wa soka wametoa hisia zao juu ya zawadi hiyo iliyotolewa na serikali kwa kijana Samatta kwa kusema kuwa, zawadi hiyo ya kiwanja inakuwa kama chachu kwa vijana wengine wa Kitanzania kujibidiisha zaidi katika sanaa na michezo kwa kuamini kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini kazi zao.

Last edited: