Serikali yamtaka Luhaga Mpina Kuomba na kupata Ufafanuzi kwa Serikali kabla ya kuzungumza mambo yasiyo na ukweli hadharani

Kwa hiyo huo mbango ndio ushahidi ? Ndio ushahidi unaoweza kumtia mtu hatiani mahakamani?
Nani mlishampeleka mahakamani kwa wizi?

Yani wezi wapeleke mahakamani wezi?

Hii ni ripoti ya CAG aliyopokea Samia hizo pesa zilizopotea nani alifikishwa mahakamani?.

Yani watu wanakuja na matokeo ya tafiti unaita bango?
 
Mkuu utetezi wa mollel ni dhaifu sana angekaa kimya kuficha aibu!
 
Mkuu utetezi wa mollel ni dhaifu sana angekaa kimya kuficha aibu!
Kivipi ni dhaifu na ni dhaifu katika hoja zipi. Vifaa vya plastic surgery vilivyokuwa vinatumika awali ndio hivyo hivyo vinatumika katika au kwa watu wanaohitaji kurekebisha makalio yao iwe ni kwa kuyaongeza au vyovyote vile watakavyo.
 
Kwa hiyo makalio kwanza mengine baadae? Wazazi wetu wanajifungulia sakafuni ila serikali ikaona kuliko kununua vitanda ni heri kuwekeza kwenye matako?
 
Kivipi ni dhaifu na ni dhaifu katika hoja zipi. Vifaa vya plastic surgery vilivyokuwa vinatumika awali ndio hivyo hivyo vinatumika katika au kwa watu wanaohitaji kurekebisha makalio yao iwe ni kwa kuyaongeza au vyovyote vile watakavyo.
Tumeona wengi walifanyiwa hizo surgery huku mtaani maarufu walikuwa wanasema kawekea nyama ya tako walifanyiwa hapa hapa nchini ila mollel kusema watu walikuwa wanakwenda india au uturuki si kweli labda wenye pesa,
Na wenyewe serikali ndio walioanza promo wenye kutaka kurekebishwa shepu sasa huduma ipo hapa hapa nchini mbona hatujuyasikia hayo kabla wawe wakweli baada ya kusikia watu wanalipa pesa ndefu kuweka makalio serikali kupitia wizara ya afya wakaona watumie fursa kwa kununua vifaa wafanye biashara nashangaa Mollel anatoa maelezo meeeengi!
 
Huyu tumesha malizana nae Kisesa ,anajua ubunge mwisho 2025 ,hivyo basi mfa maji kutapatapa lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…