Serikali yakiri kudaiwa Shilingi Bilioni 105 na wakulima wakubwa wa Korosho

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,239
Serikali imekiri kuwa bado inadaiwa bilioni105! Hakika ni maumivu makubwa mnapata. Poleni sana, hii ni zaidi ya uzalendo unaohubiriwa na serikali hii!

Hivi mtalipwa kiasi gani kufidia hasara mliyopata! Hivi serikali inafahamu jinsi watoto wenu walivyoathirika kwa kukosa ada!

Serikali iache kukurupuka katika maamuzi yake!

---------
August 29, 2019

Serikali imekiri kudaiwa shilingi bilioni 105 na wakulima wakubwa wa korosho nchini Tanzania, tofauti na matarajio yake ya kulipa korosho zote ambazo zilikuwa zinagharimu shilingi Bilioni 723 kiwango ambacho amedai ni kikubwa kwa nchi.

Wakulima wakulima wa Korosho kwa mujibu wa Waziri ni wale wenye uzalishaji wa kuanzia kilo 1,500 (tani moja na nusu) na zaidi.

Wakati msimu mpya wa korosho ukiwadia, wakulima hao wakubwa wa korosho wakiwa bado hawajalipwa, Serikali ina mpango wa kuwakopesha wakulima hao pembejeo ili waweze kuzalisha korosho msimu mpya ujao.

Wakati huo huo zaidi ya tani 200,000 za korosho bado zipo ghalani zikisubiri mnunuzi mpya aliyepatikana hivi karibuni toka Vietnam, amebainisha Mh. Waziri ktk mazungumzo hayo exclusive na kituo cha televisheni cha Azam TV cha jijini Dar-es-Salaam, Tanzania.

Chanzo: Azam TV
 
Aisee!Mungu tusunuru.Mwenye haki akitawala nchi huwa na aman.kwa namna hii ndio maana tunakuwa "nchi isiyo na amani".mwisho wa siku hata sudan kusini itakuwa nafuu.
 
August 29, 2019

Serikali imekiri kudaiwa shilingi bilioni 105 na wakulima wakubwa wa korosho nchini Tanzania, tofauti na matarajio yake ya kulipa korosho zote ambazo zilikuwa zinagharimu shilingi Bilioni 723 kiwango ambacho amedai ni kikubwa kwa nchi.

Wakulima wakubwa wa Korosho kwa mujibu wa Waziri ni wale wenye uzalishaji wa kuanzia kilo 1,500 (tani moja na nusu) na zaidi.

Wakati msimu mpya wa korosho ukiwadia, wakulima hao wakubwa wa korosho wakiwa bado hawajalipwa, Serikali ina mpango wa kuwakopesha wakulima hao pembejeo ili waweze kuzalisha korosho msimu mpya ujao.

Wakati huo huo zaidi ya tani 200,000 za korosho bado zipo ghalani zikisubiri mnunuzi mpya aliyepatikana hivi karibuni toka Vietnam, amebainisha Mh. Waziri ktk mazungumzo hayo exclusive na kituo cha televisheni cha Azam TV cha jijini Dar-es-Salaam, Tanzania.

Source: Azam TV
 
Jamani. Walijisifia wana hela za kununua Korosho zote. Sasa kiko wapi? JPM nakumbuka alivyomuaibisha Majaliwa. Baada ya Majaliwa kusema kapata makampuni ya kununua Korosho.
Ila nadhani Magufuli anapaswa kupimwa akili.
Inasikitisha mpaka sasa hivi wakulima hawajalipwa ilhali Serekale ilisema ina mahela.
 
Back
Top Bottom