Baba Mkubwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 827
- 136
Na Reuben Kagaruki, Jijini
WAKATI walimu wanatarajia kuanza mgomo wao nchi nzima Jumatatu kushinikiza kulipwa fedha za malimbikizo yao, Serikali imetoa tamko zito ikisema mgomo huo ni batili huku ikikimbilia Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kuomba iuzuie.
Hatua hiyo ya serikali imetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, alipozungumza na waandishi wa habari leo asubuhi na kutoa msimamo wa Serikali kuhusiana na mgomo uliotangazwa na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT).
Akiwa ameongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Edna Mangesho na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Hamis Dihenga, Luhanjo amesema mgomo huo ni batili kwa sababu baadhi ya vipengele havikutekelezwa.
"Katika kusudio la mgomo wa walimu baadhi ya masharti hayakutimizwa ndio maana Serikali inapinga mgomo batili usio na kikomo,"amesisitiza Luhanjo.
Ameongeza kuwa tayari Serikali imekwishawasilisha Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi maombi ya Anuai Na:21 ya mwaka 2008 kuiomba izuie mgomo usio na kikomo unaokusudiwa kuanza Jumatatu.
"CWT imepelekewa samansi ya kuitwa mahakamani kwa ajili ya shauri hilo la maombi ya Anuai ambalo limepangwa kusikilizwa Jumatatu," amesisitiza Luhanjo.
Amesema kutokana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa, Serikali imekitaka chama cha walimu kusitisha mgomo usio na kikomo. Luhanjo amesema mwalimu atakayeshiriki mgomo huo hatalipwa mshahara na serikali kwa sababu ya kushiriki mgomo batili.
Ametishia kuwa walimu watakaogoma, watalipwa mishahara yao na aliyeitisha mgomo huo. Amesema watakaogoma watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za kazi.
"Mgomo huo hauna maslahi kwa umma na hata kwa walimu wenyewe kwa sababu unakusudiwa kufanyika katika kipindi ambacho wanafunzi wanapaswa kufanya mitihani yao ya kuvuka madarasa na vidato,"amesema.
Ameikumbusha CWT kutambua kuwa suala hilo tayari lipo mahakamani hivyo kitendo cha walimu kugoma kitakuwa sawa na kuishinikiza mahakama kwenye kesi iliyofunguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alitangaza kuwa mgomo huo usiokuwa na kikomo utaanza rasmi Jumatatu ambapo utahusisha walimu wa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na vile vya maendeleo ya jamii ambao ndio wanachama wa CWT.
Mukoba amewataka walimu wasiogope vitisho vya Serikali kwa sababu mgomo huo ni halali. Baraza la Taifa la CWT linatarajia kukutana Januari mwakani ili kupitia utekelezaji wa madai yao.
Source: Dar leo
Hii ndio kawaida ya serikali yetu,badala ya kutatua matatizo inaongeza matatizo. ' WIZI MTUPU'
Jamani mnaofahamu sheria tusaidiane, iliyotengua Hukumu ya Serikali Kuzuia Walimu Kugoma ni Mahakama ya Rufaa (niko tayari kusahihishwa kama nimekosea), sasa inawezekana kuna Mahakama inayoweza kutengua Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa? Au ni Ubabe wa Serikali aka WIZI MTUPU
Ndege
Nikirudi kwa walimu, wao wana haki ya kugoma kwa mujibu wa sheria. Serikali pia ina haki ya kuzuia mgomo ambao ni batili.
Naungana na walimu kuwa madai yao ni ya msingi na wana haki ya kugoma. Siungi mkono mgomo kwenye kipindi hiki cha kusahihisha mitihani ya taifa.
Naiunga mkono serikali kuuzuia mgomo huu wa walimu kwa sababu kwa mujibu wa sheria, hakuna mgomo usiokuwa na ukomo.
Mwisho ombi kwa Mkoba na walimu, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi Wa Umma, Mhe. Hawa
Ghasia yuko hapa New Dheli India kwa ziara muhimu kitaifa. Tafadhalini sana msije mkamtibulia ziara yake akalazimika kuikatisha wakati sie wengine tulioko huku ndio tunategemea kupata mwanya wa kumuona na kumpiga maswali yetu likiwemo hilo la kilio chenu.
Ushauri wangu ni kwenu walimu msigome. Hamuwezi kushindana na serikali. Mkoba atawaponza ila kumbukeni anayewalipa mishahara ni serikali na hata huyo Mkoba anategemea makato toka mshahara huo huo. Gomeni lakini cha moto mtakipata!.
Pasco,
Umejichanganya unaunga mkono serikali,na unaunga mkono waalimu!!! Confused!! Naona umeamua kuwa msemaji wa serikali, 'sie wengine tulioko huku ndio tunategemea kupata mwanya wa kumuona na kumpiga maswali yetu likiwemo hilo la kilio chenu. Unashauri waalimu waweke silaha chini ilinyie mlio Delhi mumuulize Mh Hawa Ghasia, Pasco wa JF naulizia masuala ya waalimu? This is very low....
Wacha waalimu wagome, serikali imeshindwa walipa...wacha wagome kipindi hiki muhimu kwao, haiwezi wafukuza ni kuwatishia nyau tu.
Ushi[/QUOTE
Nimesema naunga mkono madai ya walimu ni genuine na nawaunga mkono waalimu kuitumia haki yao ya kugoma kwa kutumia mgomo halali.
Nikasema siungi mkono waalimu kugoma kipindi hiki cha
Mitihani ya taifa. Na nikasema naunga mkono serikali kuupinga mgonmo ambao hauna ukomo.
Kisheria kila mgomo lazima uwe na ukomo. Mgomo usio na ukomo, sio halali kisheria
Walimu, walimu, walimu msidanganyike mkagoma mgomo wenu sio wa halali na ile hukumu iliyouzuia bado inasimama
Japo sababu za Mahakama kuu kufikia uaamuzi wa kuuzuia ndizo zilizoelezwa kuwa na kasoro, sio hukumu!
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tannzania, Mahakamani ndipo mahali pekee pa kupatia haki. Na Mahakama ya Rufaaa ndio chombo cha Juu kabisa katika utoaji wa haki.
Ila kama bado unahisi uamuzi wa Mahakama ya Rufaa
Haujakutendea haki, unajenga hoja tena lazima iwe na nguvu kisheria kuiomba Mahakama hiyo kupitia tena maamuzi yake. Inaitwa Court Review. Mahakama ikijiridhisha una hoja ya msingi, wanaamua kuitisha Court Review. Kama hukumu ilitolewa na Jaji mmoja, Court Review wanakaa Majaji 3. Wakiamua kama hujaridhika unajenga hoja wanakaa Majaji 5. Kama bado hujaridhika unajenga hoja wanakaa Majaji 7 wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania. Hii inaitwa Full Bench. Uamuzi wake ni Wa Mwisho yaani Final. Hapo ndiyo mwisho wa haki kwa Tanzania.
Zaidi ya hapo hakuna hata Rais hawezi kusaidia. Mwisho wa uwezo wa rais ni kuamua kusaini hati ya kutekelezwa kwa adhabu ya kifo au kutoisaini. Na kutoa misamaha kwa wafungwa.
Nikirudi kwa walimu, wao wana haki ya kugoma kwa mujibu wa sheria. Serikali pia ina haki ya kuzuia mgomo ambao ni batili.
Naungana na walimu kuwa madai yao ni ya msingi na wana haki ya kugoma. Siungi mkono mgomo kwenye kipindi hiki cha kusahihisha mitihani ya taifa.
Naiunga mkono serikali kuuzuia mgomo huu wa walimu kwa sababu kwa mujibu wa sheria, hakuna mgomo usiokuwa na ukomo.
Mwisho ombi kwa Mkoba na walimu, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi Wa Umma, Mhe. Hawa
Ghasia yuko hapa New Dheli India kwa ziara muhimu kitaifa. Tafadhalini sana msije mkamtibulia ziara yake akalazimika kuikatisha wakati sie wengine tulioko huku ndio tunategemea kupata mwanya wa kumuona na kumpiga maswali yetu likiwemo hilo la kilio chenu.
Ushauri wangu ni kwenu walimu msigome. Hamuwezi kushindana na serikali. Mkoba atawaponza ila kumbukeni anayewalipa mishahara ni serikali na hata huyo Mkoba anategemea makato toka mshahara huo huo. Gomeni lakini cha moto mtakipata!.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tannzania, Mahakamani ndipo mahali pekee pa kupatia haki. Na Mahakama ya Rufaaa ndio chombo cha Juu kabisa katika utoaji wa haki.
Ila kama bado unahisi uamuzi wa Mahakama ya Rufaa
Haujakutendea haki, unajenga hoja tena lazima iwe na nguvu kisheria kuiomba Mahakama hiyo kupitia tena maamuzi yake. Inaitwa Court Review. Mahakama ikijiridhisha una hoja ya msingi, wanaamua kuitisha Court Review. Kama hukumu ilitolewa na Jaji mmoja, Court Review wanakaa Majaji 3. Wakiamua kama hujaridhika unajenga hoja wanakaa Majaji 5. Kama bado hujaridhika unajenga hoja wanakaa Majaji 7 wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania. Hii inaitwa Full Bench. Uamuzi wake ni Wa Mwisho yaani Final. Hapo ndiyo mwisho wa haki kwa Tanzania.
Zaidi ya hapo hakuna hata Rais hawezi kusaidia. Mwisho wa uwezo wa rais ni kuamua kusaini hati ya kutekelezwa kwa adhabu ya kifo au kutoisaini. Na kutoa misamaha kwa wafungwa.
Nikirudi kwa walimu, wao wana haki ya kugoma kwa mujibu wa sheria. Serikali pia ina haki ya kuzuia mgomo ambao ni batili.
Naungana na walimu kuwa madai yao ni ya msingi na wana haki ya kugoma. Siungi mkono mgomo kwenye kipindi hiki cha kusahihisha mitihani ya taifa.
Naiunga mkono serikali kuuzuia mgomo huu wa walimu kwa sababu kwa mujibu wa sheria, hakuna mgomo usiokuwa na ukomo.
Mwisho ombi kwa Mkoba na walimu, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi Wa Umma, Mhe. Hawa
Ghasia yuko hapa New Dheli India kwa ziara muhimu kitaifa. Tafadhalini sana msije mkamtibulia ziara yake akalazimika kuikatisha wakati sie wengine tulioko huku ndio tunategemea kupata mwanya wa kumuona na kumpiga maswali yetu likiwemo hilo la kilio chenu.
Ushauri wangu ni kwenu walimu msigome. Hamuwezi kushindana na serikali. Mkoba atawaponza ila kumbukeni anayewalipa mishahara ni serikali na hata huyo Mkoba anategemea makato toka mshahara huo huo. Gomeni lakini cha moto mtakipata!.
Pasco are you serious?
Unadhani walimu wakigoma wao pekee ndio watapata cha moto?!
Hapa umejidanganya. Na nadhani umejidanganya kwa kuwa uko nje ya nchi.
Hapa walimu wakigoma serikali imekipata cha moto haswa.
Leo nilikuwa na mzazi mmoja anayejua matokeo ya mgomo kwa walimu kwani ana mwanae ambaye anaingia kidato cha nne. Na anao wawili ambao ni kati ya hao waliofukuzwa juzi Chuo kikuu. Huyu alikuwa mpenzi wa JK hujapata kuona. Lakini lugha niliyosikia akizungumza leo, sikuamini. Nakuaminia kuwa serikali itakipata cha moto na hakuna hata mwalimu mmoja anayeweza kufukuzwa. Nasema hili nikijua huu ndio ukweli.
Na kama inavyosema serikali kwamba haitawalipa kama wakigoma, nakuhakikishia huu mgogoro hautakwisha milele kama hawatalipwa. Na itabidi JK na kabineti yake waingie darasani kufundisha. Je, wataweza?
Basi tusubiri tuone kama mshindi hakuwa mwalimu!
Nakubaliana na madai ya waalimu ni genuine. Nakubaliana na haki ya kugoma ila mgomo halali. Pia nakubali walimi wakigoma uwe ni mgomo halali ama sio halali ni janga lisilopimika.
Hayo yote tisa, kumi serikali imelipa bilioni za walimu leo. Walimu wakachukue pesa zao Jumatatu.
Kesho Jumapili najua Mkoba aatatangaza tena waendelee na mgomo mpaka madai yao ylipwe yote.
Ttatizo la sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma. Kwa vile kisheria hakuna mgomo usio na ukomo. Walimu wakigoma serikali italia na serikali ikkitumia sheria walimu watalia. Who laugh last, Laugh most.