Serikali yajikanyaga yenyewe

Serikali yajikanyaga yenyewe

Emma.

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
19,932
Reaction score
5,566
Heshima kwenu wana JF.
Serikali yajikanyaga yenyewe

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaa tiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Dar es Salaam. Baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuna dawa za kutosha nchini, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi.

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaatiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Hata hivyo, kauli hiyo inakinzana na ya Samia aliyoitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa wodi ya wazazi Hospitali ya Mwananyamala.

Samia alisema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi, kwani Serikali inajipanga kuondoa tatizo vifaatiba.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu kuwa wamekuwa wakikabiliwa na upungufu wa dawa.

Samia amesema licha ya Serikali kujipanga kukabiliana na tatizo hilo, uongozi wa hospitali hiyo unatakiwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato.
#My take -hizi ndo hasara za kufanya mambo kwa kukurupuka watapishana sana kauli mwaka huu dawa ni kweli hamna hospital lakini sijui wanaficha nini?
Zile pesa za kununua ndege mngeenda kununua dawa ni aibu sana.
 
huyu ummy huyu,magu alisema fyatueni watoto mtakavyo yeye akaja kumlisha maneno eti alikuwa anawatania wandengereko,samia anasema hakuna madawa yeye anasema zipo
aangaliwe huyu,this is insubordination..anapenda kupingana na wakuu wa nchi!!!!!!
 
Wewe unaongea zaidi kwa mhemkoa ndiyo maana unatumia maneno ya kejeli ebu tuambie ni hospitali ipi ulienda ukakosa dawa?
 
Kwani mada kama hizi haziwezi kuunganishwa ili tupate mwendelezo wa mawazo?
 
hawa viongoz wanazidisha utani hadi ktk maisha ya watu...

hii tabia ya kuongea ktk media alafu kesho wanakanusha ipo siku itatugharimu sisi raia.
 
huyu ummy huyu,magu alisema fyatueni watoto mtakavyo yeye akaja kumlisha maneno eti alikuwa anawatania wandengereko,samia anasema hakuna madawa yeye anasema zipo
aangaliwe huyu,this is insubordination..anapenda kupingana na wakuu wa nchi!!!!!!
Ni Babeli Sehemu II (The ancient Tower of Babel and subsequent confusion)
 
Hivi nchi hii ni moja kama tunavyoaminishwa au vipo vinchi vingine vidogovidogo ninavyiviona sasa? Juzi kuhusu tukio la walimu tarajali kule mbeya vinchi vilijionyesha dhahiri. Jana na juzi navina tena vinchi vingine. Hali hii inaniaminisha kutokuwepo kwa collectiveness katika uongozi wa nchi.
Wanoitwa viongozi hawana mawasiliano chanya hata kidogo.
Haiwezekani makamu wa rais aseme uongo na waziri wa afya ndio awe mkweli.
Kuna haja ya kuwasiliana kwa viongozi wetu juu ya mambo yenye shida ili ikitokea umealikwa uwe na angalau la kuficha au kuanika kama sio kutetea.
Mama Suluhu, ukweli utakuweka huru. Kama kuna tatizo liweke bayana ili tujue namna ya kujibadilisha. Nikuombe umfukuze kazi huyo dadake Ally chemical wa enzi za Saddam kule Iraq kwa kuudanganya umma na kusababisha vifo vilivyowza kuepukika.
 
Mhemkoa? Kiluga au? We si unatibiwa Aghakhan hawezi experience hicho kitu.
Weka ushahidi basi manake ninavyofahamu mm siku hizi hakuna matibabu ya bure,ispokua kwa makundi maalum,(wazee wa umri fulani na watoto wa Chini ya Miaka 5) wengine waliobakia wanapata matibabu kwa kuchangia gharama za matibabu kwa mantiki hiyo ukiacha makundi niliyotaja na wale wa chanjo,mtu mwingine anaweza kwenda kutibiwa hospitali tofauti na za Serikali kwa kutumia kulipa cash au bima ya Afya.Hivi sasa bima ya inapatikana kwa waajiriwa na waliojiajiri kwa hiyo ni wakati mwafaka sasa kila mtanzania kujitahidi kuhakikisha anajiunga na bima ya afya ili awe na Uhuru wa kutibiwa sehemu tofauti na hospitali za umma iwapo kutakua na changamoto za uhaba wa dawa.
 
Back
Top Bottom