Serikali 'yaimegea' kampuni Nigeria gesi ya Mtwara

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

JUMANNE, JULAI 02, 2013 05:47 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema itaipatia sehemu ya gesi ya Mtwara Kampuni ya Nigeria ya Dangote inayojenga kiwanda cha saruji kwa ajili ya kuzalisha umeme wake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema kampuni hiyo inahitaji megawati 70 za umeme kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za utengenezaji saruji mkoani humo.

Profesa Muhongo alisema umeme utakaozalishwa na kampuni ya Dangote utakuwa ni mkubwa kuliko matumizi yake hivyo kuunganishwa katika gridi ya taifa kwa ajili ya matumizi mengine ya jamii.

Leo (jana) nimekutana na viongozi wa Kampuni ya Dangote ya Nigeria ambayo imepewa jukumu la kutengeza saruji katika Kijiji cha Hiyari mkoani Mtwara.

“Tumekubali kuwapatia sehemu ya gesi kuzalisha umeme wao, pia wamesema watatoa ajira nyingi kwa vijana hasa wa Kusini.

“Wamesema kwamba uwekezaji wa viwanda vya saruji utagharimu dola za Marekani milioni 500 na watakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka.

“Kama Serikali tutahakikisha tunawapa malighafi zote zinazohitajika, tumechunguza kampuni hii tumegundua ina zaidi ya viwanda vikubwa 20 barani Afrika na vinafanya kazi vizuri,” alisema.

Akizungumzia utendaji wa wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) alisema bado shirika hilo linahitaji kusafishwa kutokana na kuwapo watumishi wazembe na wasio na mipango endelevu.

Profesa Muhongo alisema miongoni mwa uzembe huo ndani ya Tanesco ni baadhi ya watendaji kushindwa kuwa na mipango ya endelevu ya kuhakikisha huduma zinatolewa wakati wote.

“Haiwezekani mteja akasubiria ndani ya miaka miwili hadi mitano kuunganishiwa umeme eti kwa sababu hakuna mita na nguzo. Hivi kuna haja ya kiongozi huyo kuendelea kuitwa mtumishi wa Tanesco.

“Hivi sasa tumeagiza nguzo kutoka nchi mbili ya Afrika Kusini, Zimbambwe na hapa nchini tunashughulikia, tumeagiza nje kutokana na kampuni za Tanzania kushindwa.

“Yamekuwapo na malalamiko ya Watanzania kwamba tunaagiza nguzo nje, binafsi nasema kama kuna kampuni ya kitanzania ina nguzo imara ambazo zinatosheleza mahitaji ya nchi nzima aje wizarani tuonane,”alisema.

Naye Mkurugenzi wa Dangote, Alhaji Aliko Dangote alisema lengo ni kukamilisha ujenzi wa kiwanga hicho ndani ya miezi 22 na kutengeneza saruji.

Dah...naanza kupata picha kamili sasa,hii serikali na mwekezaji Ddangote
 
Twatoana roho yaalabhi,kwa mali alizo acha baaba:music::music::music: karibuni tuimbe,maana mwenye mali hatuko nae tena,tumebakia na madalali tu
 
Hivi Serikali ilikosa kabisa dola 500 za Marekani kujengea kiwanda hicho; Marekani imeendelea kwa sababu ina miliki viwanda vyake yenyewe; ona sasa wamewapa na gas ili wazalishe nishati ya umeme wenyewe , Muongo aseme basi mkataba mzima umekaaje ?
 
marekani inamiliki viwanda vyake yenyewe?
 
Swali la msingi!

Je!Hiyo gesi atauziwa ama atapewa bure kwa kisingizio cha kuzalisha umeme???
 
Swali la msingi!

Je!Hiyo gesi atauziwa ama atapewa bure kwa kisingizio cha kuzalisha umeme???

wamesema watawapa siyo kuwauzia,soma vizuri,pia si unajua kwa miaka 5 awatokuwa wanalipa kodi yoyote kulingana na sheria zetu zinavyosema,sababu wanakuwa awajarudisha ela,vijana wa mtwara watakuwa vibarua tu na wajiandae kufa kwa TB,kutoka na ilo vumbi lake
 
tunachezea rasilimali tulizonazo wakati wenzetu wanatajirika kwa hicho kidogo walichonacho. poor tanzanian leaders
 
Kitu kikubwa kinachofanya Watanzania tuulizemaswali mengi ni kutokana na usiri uliopo wa mikataba hii na hii ndiyo inayowapa wasiwasi Watanzania kuona wanaibiwa mali yao ingawa inawezekana kabisa uwekezaji huu ukawa na manufaa na faida kwa nchi.
 
Muhongo na washirika wake hawana akili. Dongote wanatakiwa kununua umeme badala ya kuwapa gas bure. Laana hii jamani
 
Hivi Serikali ilikosa kabisa dola 500 za Marekani kujengea kiwanda hicho; Marekani imeendelea kwa sababu ina miliki viwanda vyake yenyewe; ona sasa wamewapa na gas ili wazalishe nishati ya umeme wenyewe , Muongo aseme basi mkataba mzima umekaaje ?

Wewe unataka serikali imiliki viwanda? Unataka kuturudisha kwenye matatizo ambayo tunajaribu kuyasahau? Serikali ya Marekani haimiliki viwanda bali ni watu binafsi
 
Sizani kama atapewa bure, hapa kilichokosekana ni namna ya kuwakilisha hoja lakini there's no way kwamba atapewa bure! Nazani kilichopo ni namna ya kupunguza gharama manake nimeshitushwa kwamba kiwanda kinahitaji 70 MW....huu ni umeme mwingi mno....ambae kwa mazingira ya Tanzania unaweza kukuta ni umeme unaotumika karibu mikoa miwili!!

So, nazani katika harakati za kupunguza gharama za uzalishaji, inawezekana ndio sababu ya Dangote kutaka raw material (gas) na kuzalisha umeme wake yenyewe!

Vyovyote iwavyo, jambo la msingi ni kwamba kama atapewa gas basi ainunue gasi hiyo na sio kupewa bure ingawaje sioni ni namna gani atapewa bure!!!

Pamoja na hayo, hofu yangu ni kwamba GAS atatumia lakini NISHATI atakayotumia atatumia at Zero or very small cost! HOW? Ni kwamba ananunua gas kwa bei ya chini kisha anazalisha umeme! 70MW ya produced electricity anaitumia kwenye kiwanda chake na kiasi kinachobaki kinaingizwa kwenye grid ya taifa!

Kimsingi, hicho kiasi sio kwamba kitaingizwa kwenye GRID kama msaada bali atakiuza kwa husika ambao watakiingiza kwenye gridi! So, kuna uwezekano mkubwa kabisa kwamba pesa atakazopata kwa kutuuzia umeme wa gas tuliyomuuzia kwa bei ya chini; pesa hiyo ikawa na uwezo wa ku-recover zile 70MW anazotumia mwenyewe pamoja na umeme aliouza na hivyo kuwa ni kama anatumia bure! It's like mtu mwenye shida na suruali 100 kisha ananunua pamba ya kutengeneza suruali 500, kisha zile 400 anakuuzia mwenyewe wakati gharama za kuzalisha suruali 500 (say) sh. 1000 na pamba alinunua kwa sh. 500 na hivyo kutumia sh.1,500/= wakati suruali moja anauza sh. 5 na hivyo suruali zake 400 anazokurudishia mwenyewe anakuta zimemuingizia sh. 2000 na hivyo kupata faida ya sh.500 na suruali 100 za bure!!!

WAJINGA NDIO WALIWAO!
 
Da suala la nguzo ni majanga kwa sisi tunaotaka kuunganishiwa umeme..nililpa hela ya kuunganishiwa umeme Arusha maeneo ya ngareseso tangu january mpaka leo hakuna kitu..
 
Licence yao siya kuzalisha saruji?
Kwa nini asinunue kutoka Symbion?
 
Sizani kama atapewa bure, hapa kilichokosekana ni namna ya kuwakilisha hoja lakini there's no way kwamba atapewa bure! Nazani kilichopo ni namna ya kupunguza gharama manake nimeshitushwa kwamba kiwanda kinahitaji 70 MW....huu ni umeme mwingi mno....ambae kwa mazingira ya Tanzania unaweza kukuta ni umeme unaotumika karibu mikoa miwili!!

So, nazani katika harakati za kupunguza gharama za uzalishaji, inawezekana ndio sababu ya Dangote kutaka raw material (gas) na kuzalisha umeme wake yenyewe!

Vyovyote iwavyo, jambo la msingi ni kwamba kama atapewa gas basi ainunue gasi hiyo na sio kupewa bure ingawaje sioni ni namna gani atapewa bure!!!

Pamoja na hayo, hofu yangu ni kwamba GAS atatumia lakini NISHATI atakayotumia atatumia at Zero or very small cost! HOW? Ni kwamba ananunua gas kwa bei ya chini kisha anazalisha umeme! 70MW ya produced electricity anaitumia kwenye kiwanda chake na kiasi kinachobaki kinaingizwa kwenye grid ya taifa!

Kimsingi, hicho kiasi sio kwamba kitaingizwa kwenye GRID kama msaada bali atakiuza kwa husika ambao watakiingiza kwenye gridi! So, kuna uwezekano mkubwa kabisa kwamba pesa atakazopata kwa kutuuzia umeme wa gas tuliyomuuzia kwa bei ya chini; pesa hiyo ikawa na uwezo wa ku-recover zile 70MW anazotumia mwenyewe pamoja na umeme aliouza na hivyo kuwa ni kama anatumia bure! It's like mtu mwenye shida na suruali 100 kisha ananunua pamba ya kutengeneza suruali 500, kisha zile 400 anakuuzia mwenyewe wakati gharama za kuzalisha suruali 500 (say) sh. 1000 na pamba alinunua kwa sh. 500 na hivyo kutumia sh.1,500/= wakati suruali moja anauza sh. 5 na hivyo suruali zake 400 anazokurudishia mwenyewe anakuta zimemuingizia sh. 2000 na hivyo kupata faida ya sh.500 na suruali 100 za bure!!!

WAJINGA NDIO WALIWAO!

Good Analysis. Nina wasiwasi sana na Hiki kiwanda na namna huyu mwekezaji anavyokumbatiwa na kupewa support ya kipekee kabisa kutoka serikalini.

Kumbuka mpaka sasa katika nchi yetu kuna viwanda takribani vi nne vinavyozalisha cement. Kama Goverment haitatoa the same support kwa viwanda vingine pia..ni dhahiri kwamba viwanda hivi vitashindwa kushindana na Dangote na vitashindwa kuendelea kuzalisha. Hii italeta madhara makubwa kiuchumi na kimaendeleo. I think the Goverment has to put a fair ground for the cement manufacturing companies to compete effectively.

Wasalaam.
 
Back
Top Bottom