Serikali 'yaimegea' kampuni Nigeria gesi ya Mtwara

Serikali 'yaimegea' kampuni Nigeria gesi ya Mtwara

Kumbe pamoja na usomi wa muhongo bado nae anagawa maliasili zetu kama wengine hakika viongozi wa nchi hii wana matatizo.Kwa staili hii migogoro haitaisha kwenye maeneo yenye maliasili maana wananchi wataendelea kudai usawa kwenye rasilimali zinazogawiwa bure kwa wageni.
 

JUMANNE, JULAI 02, 2013 05:47 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema itaipatia sehemu ya gesi ya Mtwara Kampuni ya Nigeria ya Dangote inayojenga kiwanda cha saruji kwa ajili ya kuzalisha umeme wake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema kampuni hiyo inahitaji megawati 70 za umeme kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za utengenezaji saruji mkoani humo.

Profesa Muhongo alisema umeme utakaozalishwa na kampuni ya Dangote utakuwa ni mkubwa kuliko matumizi yake hivyo kuunganishwa katika gridi ya taifa kwa ajili ya matumizi mengine ya jamii.

Leo (jana) nimekutana na viongozi wa Kampuni ya Dangote ya Nigeria ambayo imepewa jukumu la kutengeza saruji katika Kijiji cha Hiyari mkoani Mtwara.

“Tumekubali kuwapatia sehemu ya gesi kuzalisha umeme wao, pia wamesema watatoa ajira nyingi kwa vijana hasa wa Kusini.

“Wamesema kwamba uwekezaji wa viwanda vya saruji utagharimu dola za Marekani milioni 500 na watakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka.

“Kama Serikali tutahakikisha tunawapa malighafi zote zinazohitajika, tumechunguza kampuni hii tumegundua ina zaidi ya viwanda vikubwa 20 barani Afrika na vinafanya kazi vizuri,” alisema.

Akizungumzia utendaji wa wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) alisema bado shirika hilo linahitaji kusafishwa kutokana na kuwapo watumishi wazembe na wasio na mipango endelevu.

Profesa Muhongo alisema miongoni mwa uzembe huo ndani ya Tanesco ni baadhi ya watendaji kushindwa kuwa na mipango ya endelevu ya kuhakikisha huduma zinatolewa wakati wote.

“Haiwezekani mteja akasubiria ndani ya miaka miwili hadi mitano kuunganishiwa umeme eti kwa sababu hakuna mita na nguzo. Hivi kuna haja ya kiongozi huyo kuendelea kuitwa mtumishi wa Tanesco.

“Hivi sasa tumeagiza nguzo kutoka nchi mbili ya Afrika Kusini, Zimbambwe na hapa nchini tunashughulikia, tumeagiza nje kutokana na kampuni za Tanzania kushindwa.

“Yamekuwapo na malalamiko ya Watanzania kwamba tunaagiza nguzo nje, binafsi nasema kama kuna kampuni ya kitanzania ina nguzo imara ambazo zinatosheleza mahitaji ya nchi nzima aje wizarani tuonane,”alisema.

Naye Mkurugenzi wa Dangote, Alhaji Aliko Dangote alisema lengo ni kukamilisha ujenzi wa kiwanga hicho ndani ya miezi 22 na kutengeneza saruji.

Nipo curious kidogo.
Kwa nini wasiunguze gasi moja kwa moja kutengeneza sementi?
 
Huyu Muhongo mbona anataka kuchafua hali ya hewa.atampa dangote gas ataitoa wapi? Serikali yetu inakiwanda cha kuzalisha gas? Au watanunua na kumpa dangote bure.

Huyu dangote huyu,,mi toka akimbilie mtwara kuzima kelele za wanamtwara huwa najiuliza atalipwa nini na hawa madalali wetu?
 
Tatizo ni percent ngapi amewapa viongozi wetu serikalini.Na ndiyo maana mikataba yote ni mibovu kisa vijipercent ambavyo mwisho wa siku vinadidimiza uchumi wetu.Sioni ni kwa nini Rais wetu JK hataki kujifunza kutokana na makosa aliyofanya BM.Watanzania tutaishia kunawa tu.
 
Tutaibiwa mpaka lini? wanamtwara komaeni tupo nyuma yenu /begakwa bega
 
mbona tunakuwa tunalalamika sometime mambo yasiyo kuwa na Msingi.Asinge jitoteza mu wekezaji bado watu wangedai Taifa limekosa wawekezaji.!sometime tuwe tunashukulu Hich kiwanda cha saruji,jamaa angeweza ata ku allocate malawi.
 
Licence yao siya kuzalisha saruji?
Kwa nini asinunue kutoka Symbion?

Nadhani MUHONGO & CO watakuwa wameshampatia hiyo leseni mpya. Kumbuka hiyo ya umeme lazima ianze kwanza.
SASA MTZ WA KAWAIDA MWENYE UWEZO KIFEDHA ILA ASIYE KADA WA UFISADI AKAOMBE KUWEKEZA AZALISHE UMEME UONE KAMA ATAPEWA.

Mbona ile mitambo ya TANESCO iliyopo inatakiwa upgrading kidogo ili waweze kumlisha mteja huyu?
 
Hivi hizi deals huwa wanapeana wapi?
 
Nipo curious kidogo.
Kwa nini wasiunguze gasi moja kwa moja kutengeneza sementi?

Good!
Hii ni engineering perspective nzuri sana.
It is efficient to get heat energy direct from gas burning than " burning it to get electricity then converting electricity to heat".

Japo naamini tatizo litakuwa ni technology waliyokusudia
 
tunachezea rasilimali tulizonazo wakati wenzetu wanatajirika kwa hicho kidogo walichonacho. poor tanzanian leaders

Me naanza kuamini that we're possessed....

The way things are run is just impossible:.......impossible under a right mind
 
Hivi kwa nini wawekezaji wanwekeza 100% kwenye investment kubwa kama hizo? kwanini government haiweki angalau 40% hata kama siyo in term of finance it can use as valued land and capitalize it, convert into share.
Kama hilo gumu wanatuuzia sisi wananchi kwenye stock market, ili kukuza mitaji ya wananchi na kuongeza uwekezaji wa ndani.
nani ataweza kuona na kuestablish the real returns on such investment?
Tanzania economist this world economy is moving to state capitalism where are you? Dr Mpango hebu jitokezee, simama imara tuambie wewe na think tanks mnafanya nini.
Obama kaja hapo, wote tumeona anaongea kwa nini yupo afrika, government learn thst simple strategy
SP
 
Ujinga, rushwa, ubinafsi na wiz wa maccm vinatutesa. Tunachakula, tunapika, wanapakua wengine wanakula cc tunaosha sahan
 
Kiwanda ni cha CCM tulishaambiwa hapa hapa jamvini CCM aslimia 49 na Ndongate 51 ndio maana wanaendelea kubaka na kutesa na kuua wananchi huko
 
Hivi Serikali ilikosa kabisa dola 500 za Marekani kujengea kiwanda hicho; Marekani imeendelea kwa sababu ina miliki viwanda vyake yenyewe; ona sasa wamewapa na gas ili wazalishe nishati ya umeme wenyewe , Muongo aseme basi mkataba mzima umekaaje ?

Kunatofauti kati ya kujenga kiwanda na kukifanya kiendelee yaani running of industry. Kuendesha kiwanda kiweze kukidhi haja husika na matakwa yake ni gharama sana.
Pili swala la maendeleo la marekani na nchi nyingi za dunia ya kwanza kuna mlolongo mrefu sana na kamwe usidhani kuna nchi yeyote afica ama kusini mwa africa itaweza kuendelea kwa kufuata nyayo zile zile zilizofatwa na hizi nchi...
Kama kuendelea tutaendelea lakini kwa ubunifu na nadharia tofauti ya kimaendeleo kulingana nao.
 
Serikali ya Marekani inamiliki viwanda gani?tujuze ili isiwe upotoshaji!Suala la serikali kujenga viwanda halipo kwenye uchumi wa kisasa.Silaha za vita na ndege za kijeshi marekani zinatengenzwa na kampuni binafsi.
 
Back
Top Bottom