Serikali yagoma kumkabidhi CAG hesabu za Meremeta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yagoma kumkabidhi CAG hesabu za Meremeta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 24, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Serikali yagoma kumkabidhi CAG hesabu za Meremeta[​IMG]Na Ramadhan Semtawa

  LICHA ya Bunge kuitaka serikali iwasilishe hesabu za Kampuni ya Meremeta kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hadi sasa serikali imeshindwa kuwasilisha hesabu hizo kwa mkaguzi huyo.


  Agizo hilo la bunge ambalo lilitolewa Juni mwaka huu, lilitokana na ombi la Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma ambalo lilipinga kauli ya Waziri Mkuu kwamba Meremeta ni kampuni inayohusiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ).

  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam kwamba, bado serikali haijawasilisha hesabu za Meremeta.

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwahi kuapa bungeni kwamba yuko tayari kusulubiwa, lakini si kuzungumzia siri za Meremeta kwani zinahusu mambo ya Usalama wa Taifa.

  Kiapo hicho kinaonekana kufanyakazi, kwani kwa mujibu wa CAG Utouh, ni kweli aliwahi kupata taarifa ya Kamati ya Hesabu za Masharika ya Umma, lakini alitegemea kupata hesabu hizo kutoka serikalini.

  "Nitakagua nini brother (kaka) wakati sijapata hesabu zenyewe kutoka serikalini…, hadi sasa sijaletewa hesabu siwezi kufanya ukaguzi wowote," alifafanua CAG Utouh.

  Alisisitiza kwamba, siku zote amekuwa akikagua hesabu zinazofikishwa mezani kwake na kuongeza, kama serikali ikiwasilisha hesabu hizo zitakaguliwa.

  Tayari Naibu Msajili wa Hazina Godfrey Msella, ambaye ni mwanahisa mkuu wa mashirika yote ya umma, alisema Meremeta haijasajiliwa chini ya Ofisi ya Hazina kama shirika au kampuni kwani bado ni mradi chini ya wizara.

  Msella aliwahi kuiambia Kamati hiyo ya bunge mbele ya Mwenyekiti wake Zitto Kabwe kwamba, Meremeta hadi sasa inaweza ikawa ni mradi chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

  "Meremeta haiko katika orodha ya mashirika chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, ni mradi tu ambao uko chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa," alitua mzigo huo.

  Meremeta ni kampuni ambayo tayari imechota Sh 155 bilioni zilizolipwa na Benki Kuu Tanzania (BoT) kwa Kampuni Nedcor Trade Service baada ya udhamanini wa mwanahisa Kampuni ya Trinenex (PYT) limited, ya Afrika Kusini.

  Ingawa serikali imetangaza kumiliki hisa asilimia 100 za Meremeta, kwa sasa kupitia Kampuni ya Tangold, lakini vyanzo huru vya habari vinaonyesha utata, kutokana na kumbukumbu kuonyesha kampuni hiyo ilisajiliwa kisiwani Man,Uingireza mwaka 1997, ikiwa na hati ya usajili namba 3424504. Lakini, kumbukumbu za serikali zinaonyesha Meremeta ilisajiliwa ikiwa ni asilimia 50 kwa 50 za ubia kama mradi kati yake na Triennex (PTY) Limited lakini pia makampuni ya London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd, zote zinadai ni wanahisa
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,191
  Trophy Points: 280
  Zimeshachotwa hapo shilingi 155 billioni 22 bilioni more ukilinganisha na EPA ili kutofanya uchunguzi wa wahusika wa ufisadi huu wanaleta kisingizio kwamba ni usalama wa Taifa, mrafu wa kuchimba dhahabu na usalama wa Taifa wapi na wapi!! Si ajabu muda si mrefu ujao ufisadi wa bilioni 40 za Kagoda na Mgodi wa Kiwira nao utaingizwa kwenye kundi la "usalama wa Taifa" alias "usalama wa Mafisadi"
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,468
  Trophy Points: 280
  Just thinking aloud. "Wajameni, Meremeta tunapigia gitaa mbuzi, ni mambo ya Jeshi, pesa tulinunulia silaha za kivita na matumizi ya ulinzi na usalama ambayo ni out of bound ya CAG, na kama anaruhusiwa kukagua, then out of bond ya public ni SIRI-KALI. Hizo ndio pesa ya chakula ya wazee wa juu kabisa darini, nyingine ndizo zile za vijisenti, wazee wote walijipatia migao yao, wao wamehifadhia Uswisi, ni kosa lake mwenyewe iliyehifadhi Uingereza kwa wanoko!.
  Tuendelee kupiga kelele za mlango, ikitokea mwenyenyumba ameshtuka usingizini, then kelele hizo zitamcheleweshea kidogo usingizi, ili hazitamnyima usingizi wake".
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  upuuzi mtupu!
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Nchi hii ....
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wananchi hawa....
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  silaha zipi bana..acheni kututia hasira hapa
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  mafisadi wale!!!!
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wenyenchi hao!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Nov 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wakabidhi hesabu za Meremeta zikaguliwe wachekwe?
   
 11. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na tukitaka tucheke sisi ba si tumpe uraisi Slaa
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  MKJJ wachekwe na nani sisi wananchi??? hata kama wakikabidhi bado tu wanacnhi wataendelea kuwapigia kura ingawa twajua fika itakuwa scandal kubwa hapa nchini na magazeti yatauzaaa sana na tutapotezewa muda wetu wakuyasoma magazeti na kutizama TV na hakuna atakaye jiuzuru. na hata kama wakijiuzuru serikali ya CCM haitowafanya kitu mfano tu Richmond ni porojo na kupoteza fedha za walipakodi kila muda wabunge waendapo bunge na kushindwa timiza matatizo ya wananchi na wanakalia kuongelea self interest.

  Taabu kwele kweli

   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hivi serikali yetu kweli yajua nini maaana ya Usalama wa Taifa? au wanatupigia propaganda zao za siasa chafu hapa.

  Kwanza Usalama wa Taifa haupaswi ingiliana na mambo ya siasa lakini hapa kwetu siasa imejikita kwenye usalama wa taifa 99% either kwa kulazimishwa na serikali na si lolote.

   
 14. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii nchi viongozi wanafiki sana na waoga kupita kiasi
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kwani CAG sio serikali hawezi kutumia power yake? hao serikali ni kina nani hasa?
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wizi Mtupu!
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280

  mwanakijij ushawahi kusikia siku unaamua kukaa uchi upate upepo unakumbana na mkweo...ndio hicho ccm wanaogopa kufanya wakitoa sawa na kukutana na wakwe zao........,
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  hiyo ni expirment bado hypothesis
   
 19. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #19
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Mimi, wewe, yule na yeyote mwenye uraia wa TZ.......... Wanaokataa kuwasilisha mahesabu ni akina JK et el.... na si serikali
   
Loading...