Serikali yachangia ujenzi wa Shule Shikizi ya Kitongoji cha Nyasaenge cha Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

SERIKALI YACHANGIA UJENZI WA SHULE SHIKIZI YA KITONGOJI CHA NYASAENGE CHA MUSOMA VIJIJINI

Kitongoji cha Nyasaenge ni moja ya vitongoji sita (6) vya Kijiji cha Kataryo. Kijiji hiki ni moja ya vijiji vitatu (3) vya Kata ya Tegeruka ya Musoma Vijijini.

Mwaka 2017, wananchi wakazi wa Kitongoji cha Nyasaenge waliamua kushirikiana na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo kujenga Shule Shikizi ili kutatua tatizo wa watoto wao kutembea mwendo wa takribani kilomita 6-8 kwenda na kurudi kutoka masomoni kwenye Shule ya Msingi Kataryo.

Ujenzi wa awali wa gharama ya Tsh 49,086,500 (Tsh 49.01m) ulikuwa wa vyumba vya madarasa viwili (2), Ofisi ya Walimu moja (1), choo chenye matundu manne (4). Michango na nguvukazi ilitolewa na wana-Kitongoji cha Nyasaenge. Mbunge wao wa Jimbo alichangia Saruji Mifuko 100 na Mabati 108.

Baadae, Serikali litoa michango kama ifuatavyo:
*Mwaka 2021: EP4R: Tsh 46,600,000
*Mwaka 2023: BOOST: Tsh 81,300,000
Tsh 50,000,000 (nyumba ya mwalimu)

Shule ya Msingi Nyasaenge:
Shule Shikizi Nyasaenge imetimiza vigezo vyote vya kuandikishwa kuwa shule ya msingi kamili- ombi liko kwenye Halmashauri yetu (Musoma DC).

Ziara ya Chama & Mbunge:
Jana, Jumatano, 16.8.2023, Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ndugu Denis Ekwabi aliongoza Kamati ya Siasa ya Wilaya kushirikiana na Mbunge wa Jimbo kukagua mradi huu wa ujenzi kwenye Shule Shikizi Nyasaenge.

Vilevile, wananchi walipewa muda mwingi wa kuwasilisha kero na matatizo yao kwa viongozi hao - walipewa majibu yaliyowaridhisha sana.

Tafadhali wasikilize wana-Kitongoji Nyasaenge na viongozi wao kutoka kwenye VIDEO/CLIP iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 17.8.2023

 
Back
Top Bottom