Serikali yabadili uamuzi, yauza korosho ghafi kwa wafanyabiashara wa nje

Serikali imebadili uamuzi wake wa awali wa kubangua korosho zote ndani ya nchi na kuziuza zikiwa zimebanguliwa na badala yake imeamua kuuza korosho ghafi

Serikali ya Tanzania imeingia mkataba wa mauziano ya Korosho na kampuni ya 'Indopower Solution' ya Kenya, mapema jana Jumatano jijini Arusha.

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu Thika, nchini Kenya itanunua tani laki moja za Korosho ghafi zenye thamani ya shilingi 418 bilioni.

Waziri wa viwanda na biashara Joseph Kakunda amesema serikali inaendelea kuwakaribisha wanunuzi wa Korosho kutoka nje ya Tanzania kwa maslahi ya uchumi wa taifa na mkulima.

Mbali na uwepo wa Waziri Kakunda, Makubaliano hayo yameshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria,
Baadaye Kenya itakuwa ndo anaonekana mzalishaji Mkuu,maana wanaakili kuliko sisi
 
Serikali imebadili uamuzi wake wa awali wa kubangua korosho zote ndani ya nchi na kuziuza zikiwa zimebanguliwa na badala yake imeamua kuuza korosho ghafi

Serikali ya Tanzania imeingia mkataba wa mauziano ya Korosho na kampuni ya 'Indopower Solution' ya Kenya, mapema jana Jumatano jijini Arusha.

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu Thika, nchini Kenya itanunua tani laki moja za Korosho ghafi zenye thamani ya shilingi 418 bilioni.

Waziri wa viwanda na biashara Joseph Kakunda amesema serikali inaendelea kuwakaribisha wanunuzi wa Korosho kutoka nje ya Tanzania kwa maslahi ya uchumi wa taifa na mkulima.

Mbali na uwepo wa Waziri Kakunda, Makubaliano hayo yameshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria,
Sasa serikali imebadili uamuzi upi hapo? Kwa hesabu zako ulizoweka hapo juu, serikali imepata faida kubwa sana kupita maelezo. Yaani kwa hesabu hizo (sijui kama upo sawa) serikali imepata faida kuliko ingeuza za kubangua.
 
Serikali ya JMT imekubalili kuuza korosho ghafi kutoka kwenda nchini Kenya .Makubaliano husika yalithibitishwa na waziri wa viwanda na biashara wa Tanzania.Hakika mungu ni mwema kwa taifa letu haswa baaada ya wasioitakia mema Tanzania kupiga kelele za ukosefu wa soko.
Kenya mwanaume ujumbe ufike Lumumba.
 
Sasa serikali imebadili uamuzi upi hapo? Kwa hesabu zako ulizoweka hapo juu, serikali imepata faida kubwa sana kupita maelezo. Yaani kwa hesabu hizo (sijui kama upo sawa) serikali imepata faida kuliko ingeuza za kubangua.

FaizaFoxy kwa vile korosho na pesa ni swala la namba tunaweza kuziangalia zinasemaje.

Tani tajwa 100,000 ambazo bei ya kununulia ilikuwa Sh3,400 kwa kilo au Sh. 3,400,000 kwa tani moja. Hivyo tulitumia Sh 340b kufanya manunuzi.
Taarifa inasema tumepata 418b
Faida ghafi 78b
Ukitoa gharama zingine (usafiri, ghala, watunza ghala, posho na mishahara) sijui kinabaki kiasi gani hapo.

Nadhani serikali ingepata zaidi kwenye tozo mbali mbali kama ingeacha biashara ijiendeshe yenyewe. Bila shak JK alijua kanuni za biashara.
 
Serikali imebadili uamuzi wake wa awali wa kubangua korosho zote ndani ya nchi na kuziuza zikiwa zimebanguliwa na badala yake imeamua kuuza korosho ghafi

Serikali ya Tanzania imeingia mkataba wa mauziano ya Korosho na kampuni ya 'Indopower Solution' ya Kenya, mapema jana Jumatano jijini Arusha.

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu Thika, nchini Kenya itanunua tani laki moja za Korosho ghafi zenye thamani ya shilingi 418 bilioni.

Waziri wa viwanda na biashara Joseph Kakunda amesema serikali inaendelea kuwakaribisha wanunuzi wa Korosho kutoka nje ya Tanzania kwa maslahi ya uchumi wa taifa na mkulima.

Mbali na uwepo wa Waziri Kakunda, Makubaliano hayo yameshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria,
Hapa serikali inafanya kangomba, mlisema hamtaki kuuza korosho ghafi, na mmewadhulumu watu kwa kuwa watu wa kati kwenye korosho, nanyi mnakuwa watu wa kati. Lipeni mliowadhulumu, hata familia zao iwapo wamekufa walipwe, hakuna maombi yatakayakubalika kwa Mungu ukiwa mdhulimaji, itakuwa ngonjela tu. Jitafakari.
 
Hata ukitaka zote ziwe gharama na zibaki 1b tu ni faida kubwa sana.

1b wewe una mshahara kiasi gani? Itakulipa maisha yako mpaka kufa halafu unaiona ndogo?

Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.
 
4180-3300=880×1000×100,000=88,000,000,000 kapata faida ya sh bilioni 88
 
Back
Top Bottom