Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Waanzishe na kufufua mabasi ya usafirishaji ya mikoa kama Kauru, kaumu, kauta, kaudo na kadhalika maana hawa wafanya biashara wanapiga sana ela
hii mikoa iko nch gan?
 
Sioni vipi sekta binafsi inaweza shindana na serikali. Yale yale ya FastJet kujirudia.. but all in all kwetu walaji wa mwisho inaweza kuwa nafuu... let's wait and see
Kama zinavyokua nauli nafuu sasa hivi baada kufa kwa fast jet eeehhhh?
 
atakaye ona anabanwa atafunga shell zake
Ni wazo zuri sana ila sio kwa level za chini ivo hapo tulitegemea goverment ijihusihe na bulk to ya ilo wese tofauti na kuja uku grounds ambako tayari wafanya biashara wapo unafikiri nini kitatokea kwa vituo kama total ambapo gari za serikali hujaza mafuta
 
Wewe utakuwa ni mpumbavu sana, yaani una mamlaka gani uniambie nihame nchi hii? Nchi hii tuliachiwa na baba wa taifa marehemu mwl JK Nyerere.
Wewe ni pandikizi sio mTz halisi.Kindly ask your parents wakurudishe kwenu.
 
Hawataki kujifunza kwenye korosho
Total hapo wajiandae kisaikolojia ila hili swala la serikali kufanya biashara ni kuongeza mianya ya upigaji tu mana usimamizi wao unajulikana ulivyo wa chini, Mtu akiajiliwa serikalini ana relax sana na ivo hio sehemu kugeuka kuwa shamba la bibi kuna umuhimu wa kutengenezea sectòr binafsi mazingira ili wao ndio wafanye biashara
 
Wasisahau kufufua kampuni ya mabasi KAMATA nchi nzima,,watu wanapiga hela sana hii sekta,,serikali inaachia pesa nyingi tu..[emoji58][emoji58]
Kwahiyo hutaki watu wapige hela!? Akili za wapi hizi!?
 
Kitumbua kishaingia mchanga, Yale Yale ya fastjet.
 
View attachment 1472096

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.

Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.

Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.
eti mafuta na huduma vyenye ubora !! mmeshindwa kufanya hivyo kwenye TBC mtaweza kwenye mafuta?
 
UJENZI WA KITUO CHA MABASI CHA NGANGAMFUMUNI KUANZA RASMI
thumb_215_800x420_0_0_auto.jpg
Posted On: January 16th, 2019
MAYA.jpg
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imesaini mkataba na kampuni ya ukandarasi ya kimataifa ya CRJE (EAST AFRICA LTD), kwa ajili ujenzi wa kituo cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni.
Ujenzi wa kituo hiki cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni(Ngangamfuni International Bus Stand Terminal ) utaanza rasmi Januari 17 mwaka huu mbapo hadi kukamilika mradi huu wa ujenzi utagharimu zaidi ya tsh bilioni 27.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi wa Manispaa ya
Moshi, Michael Mwandezi alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho utatekelezwa kwa awamu tatu tofauti huku ukichukua muda wa miaka miwili hadi kukamilika.

Hata hivyo Mwandezi alisema kuwa mradi huo mpya wa kituo cha mabasi utaibadilisha Manispaa hiyo katika Nyanja ya kichumi pamoja na utekelekezaji wa malengo ya Serikali kuhakikisha miradi yake inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Moshi Rayamod Mboya alisema kuwa,ujenzi wa kituo cha Ngangamfumuni ulisubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa Manispaa ya Moshi na wadau wa usafirishaji hivyo kukamilika kwake kutaongeza hadhi pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi.

Alisema ujenzi wa kituo hicho cha mabasi utatekelezwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni kukamilisha eneo la maegesho ili kuweza kuanza kazi ambapo awamu nyingine ni pamoja na kuanza ujenzi wa jengo la gorofa tano ambalo litakuwa na Hoteli,maduka, migahawa pamoja na ofisi mbalimbali.

Kukamilika kwa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha ngangamfumuni kutaifanya Manispaa ya kuwa mojawapo ya Manispaa zitakazokuwa na kituo ya mabasi chenye ubora zaidi nchini na ukanda wa Afrika Mashariki

Source : UJENZI WA KITUO CHA MABASI CHA NGANGAMFUMUNI KUANZA RASMI
 
wamiliki wa vituo binafsi vya mafuta wajiandae kwa figisu figisu ili mtoto mpya ashike hatamu ya biashara nawaza kwa kuzingatia kilichowakuta kina fastjet na wenzake.
 
Ushaanza ujenzi?
 
hapa hata mm pamenipa ukakasi ikabid niikumbuke fast jet na issue za korosho
Kuna kitu ambacho serikali ime- overlook ni kuwa mishahara inayolipwa na sekta binafsi kwa watumishi wake ni midogo sana na ndiyo sababu bado zinadumu. Shirika la umma litalazimika kulipa mishahara ya serikali hivyo gharama za uendeshaji zitakuwa kubwa kulinganisha na sekta binafsi.

Aidha idadi ya watumishi katika sekta binafsi ni wachache kitu ambacho kwa shirika la umma haitawezekana. Kwa vyo vyote vile tutegemee uendeshaji wa shirika utakuwa na changamoto.
 
Back
Top Bottom