Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Ujenzi stendi mpya Mbezi wafikia pazuri ! Maendeleo ya Vitu badala ya Maendeleo ya Watu
January 27, 20200
maxresdefault-5-1024x576.jpg

Picha : ujenzi wa stendi ya mabasi Mbezi Dar es Salaam Tanzania
Wananchi wanahitaji kuona ujenzi wa Hospital nyingi kubwa kwa ajili ya Maendeleo ya Afya za Watu wao CCM Mpya wanashindanisha maujenzi ya Vituo Vikubwa vya Mabasi baina ya mikoa kweli CCM Mpya inajali Maendeleo ya Vitu kuliko Maendeleo ya Afya za Watu

21 Jun 2019
ULIPOFIKIA UJENZI WA STENDI MPYA MBEZI, DAR ES SALAAM, WAZIRI JAFO AKAGUA!

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jafo, leo Juni 21, ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa stendi mpya inayoendelea kujengwa Mbezi jijini Dar... Baada ya kukagua mradi wa ujenzi huo, Waziri Jafo, amewaomba wakandarasi wanaojenga stendi hiyo kuhakikisha wanamaliza stendi hiyo kabla ya uchaguzi mkuu mwakani ili waweze kumualika Rais Magufuli aje kuizindua

Source: Global TV online.
 
View attachment 1472096

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.

Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.

Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.
Hii sera ya serikali kufanya biashara wameiokota wapi ? inafahamika kwamba serikali ilikwishajiondoa kwenye mambo haya na kubaki msimamizi , huyu kalemani kaokota wapi mambo haya , au ni kweli kwamba serikali haina ajenda ?
 
Biashara ya mafuta imeshikiliwa na makampuni ya nje sio mbaya serikali ikafanya mana inapoteza pesa nyingi sana huko kwa kujaza mafuta magari ya serikali
 
Serikali kujihusisha na biashara hii wapi na wapi nani atakuwa regulator? Sera hizi mbovu ndio inafanya makampuni ya ukandarasi yanakufa.

Hii nchi inalenga kufukuza wawekezaji wa ndani na nje na ndio itakuwa mwanzo wa kuua kabisa uchumi huu unasuasua.

Huu utaratibu aliuanzisha Mwl Nyerere na ukafeli vibaya sasa tena watu wasiopenda ushauri wanalazimisha tena kuurejesha, kamwe hawatafaulu akiondoka ataondoka nao. Tuko hapa.
 
https://english.elpais.com › ... › News
Cuba's healthcare system: How does Cuba manage to achieve first-world health statistics ...

10 Feb 2017 · Cuba's healthcare system is a source of pride for its communist government. The country has well-trained, capable doctors, the sector

Hospitali Hospitali wananchi ndiyo kipau mbele chao ktk mikoa na wilaya siyo maujenzi ya Vituo vya Mabasi mfano wa Shopping Mall. Nilizungumza na Mzee mmoja akionesha masikitiko yake kwa serikali kutojenga mahospitali makubwa kabisa badala ya utitiri wa haya mastendi ya mabasi ya wapitao kwenda waendako.

Video Source : millard ayo
Mzee Akaniuliza maoni yangu kama kijana nami nikasema naama kama serikali ikiwasilikiza wananchi kwa kujenga hospitali kubwa kabisa Mpya zilizojaa vifaa tiba, madawa na wafanyakazi basi sisi tusingekuwa na hoja kuishangaa serikali na maamuzi yake maana ubora wa huduma za afya Tanzania ungefanana na Cuba ya Fidel Castro na nchi ingepata utalii wa wasaka huduma za afya kwa fedha za kigeni.
 
View attachment 1472096

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.

Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.

Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.

Ni vizuri sana maana hawa wauza mafuta ikitokea bei ya mafuta inapanda kama baada ya wiki wanaficha mafuta na kuisababishia nchi tafrani. Ni heri nao wakashindana na kuweka usawa.
Kongole kwa Raiss wangu
 
Hii sera ya serikali kufanya biashara wameiokota wapi ? inafahamika kwamba serikali ilikwishajiondoa kwenye mambo haya na kubaki msimamizi , huyu kalemani kaokota wapi mambo haya , au ni kweli kwamba serikali haina ajenda ?
Usikute ni madili yao hao
 
Wajifunze kupitia korosho
Biashara ya mafuta imeshikiliwa na makampuni ya nje sio mbaya serikali ikafanya mana inapoteza pesa nyingi sana huko kwa kujaza mafuta magari ya serikali
 
Hasara kwa taifa
Serikali kujihusisha na biashara hii wapi na wapi nani atakuwa regulator? Sera hizi mbovu ndio inafanya makampuni ya ukandarasi yanakufa.

Hii nchi inalenga kufukuza wawekezaji wa ndani na nje na ndio itakuwa mwanzo wa kuua kabisa uchumi huu unasuasua.

Huu utaratibu aliuanzisha Mwl Nyerere na ukafeli vibaya sasa tena watu wasiopenda ushauri wanalazimisha tena kuurejesha, kamwe hawatafaulu akiondoka ataondoka nao. Tuko hapa.
 
View attachment 1472096

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.

Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.

Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.
Materego kwao Mara. Kituo cha kwanza kujengwa kimejengwa Mara.

Huwa nasikia kabila fulani tu ndiyo wanapendelea kwao. Huyu naye sijui nisemeje. Au anaiga yale yanayoendelea Chato?
 
Biashara ya mafuta imeshikiliwa na makampuni ya nje sio mbaya serikali ikafanya mana inapoteza pesa nyingi sana huko kwa kujaza mafuta magari ya serikali
upeo huu wa akili unatakisha tamaa kabisa yaani,
 
Maajabu ya karne ktk sera za serikali ya CCM Mpya yajitoa ktk mazao ya ndani inajiingiza ktk bidhaa za kuagiza toka nje
June 7, 2020
Mwanza, Tanzania

Serikali yaacha kutoa bei elekezi ya pamba
Waziri wa Kilimo Mh. Japhet Hasunga awaambia wakulima, bodi ya Pamba na wadau wa zao la pamba nchini kuwa sasa serikali imeacha kutoa bei elekezi ya zao la pamba.

Waziri huyo wa Kilimo alibainisha kuwa mwaka jana serikali ikijaribu kuingilia soko kwa kuweka bei ekelezi ya Tshs 1,200 kwa kilo, wakaona uamuzi huo haukuwa sahihi maana walikiona cha mtemakuni na yeye kama waziri maamuzi hayo yalitaka kumtokea puani. Hivyo kuanzia sasa bei ya zao hilo itapangwa na Soko la Dunia hukuu Bodi ya Pamba ikisaidia wakulima kufahamu bei. Serikali itajikita kuweka mazingira wezeshi tu kilimo kifanyike na mazao kufika sokoni.

Uzalishaji mwaka jana wa pamba ulikuwa tani 348,000 na kwa mwaka huu uzalishaji unatarajiwa kupunguaz kufikia tani 150,000. Mwaka jana mazao ya kilimo yalichangia 28% ya mapato ya nchi.
Source : Azam TV
 
Back
Top Bottom