Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

Serikali yaanza rasmi Biashara ya kuuza mafuta nchini

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
815
Reaction score
733
1591622145884.png


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi biashara ya kuuza na kusambaza mafuta nchini kwa kufungua kituo cha kwanza kuuza mafuta ya Petroli na Dizeli cha Serikali kitakachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kupitia Kampuni yake Tanzu ya Mafuta ( TANCOIL). Aidha Dkt. Kalemani alisema kuwa kuzinduliwa na kufunguliwa kwa biashara hiyo ni kutimiza azma na nia njema ya Serikali ya kuboresha shirika lake la TPDC,kuwapatia na kuwasogezea karibu wananchi wake huduma ya kupata mafuta yenye viwango vya ubora unaotakiwa, bei nafuu, na yatakayopatikana kwa wingi muda wote.

Dkt. Kalemani alifanya Uzinduzi huo pamoja na kufungua kituo hicho wilayani Musoma, mkoani Mara Juni 6, 2020, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizochini yake. Alisema baada ya kuanza rasmi kwa biashara hiyo, TPDC kupitia TANCOIL itashirikiana na Halmashauri zote nchini kuhakikisha inafanikisha azma ya Serikali ya kufungua na kuweka vituo vya kuuza na kusambaza mafuta katika kila halmashauri nchini pamoja na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta.

Dkt. Kalemani aliwaeleza watanzania kuwa TPDC na TANOIL watashiriki katika biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta kama zinavyofanya kampuni zingine za mafuta nchini ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa kampuni za kizalendo kushiriki katika biashara ya mafuta, ambayo kwa sasa inafanywa na makampuni kutoka nje ya nchi tu. Alisema kuwa serikali kupitia TPDC itajenga vituo 100 kwa kipindi cha miaka 5 ijayo, tayari baadhi ya Halmashauri zimeanza kutenga maeneo yatakayojengwa vituo hivyo: Aidha itahakikisha kuwa nusu ya mafuta yote yanayoingizwa nchini yanasimamiwa TPDC.
 
Tunajenga taifa hodhi la ajabu sana. Kupanga ni kuchagua, vituo vya mafuta ni pety buss kwa sasa wapo wajasiliamali wengi wadogo na wa kati. Endapo lipo swala la usalama bora serikali ingejipanga kuagiza bulk pekee.
 
Waanzishe na kufufua mabasi ya usafirishaji ya mikoa kama Kauru, kaumu, kauta, kaudo na kadhalika maana hawa wafanya biashara wanapiga sana ela
Wasisahau kufufua kampuni ya mabasi KAMATA nchi nzima,,watu wanapiga hela sana hii sekta,,serikali inaachia pesa nyingi tu..
 
Walianza na korosho wakashindwa hadi leo hii zao hili bado halijarudi kwenye mstari wake
Tunajenga taifa hodhi la ajabu sana. Kupanga ni kuchagua, vituo vya mafuta ni pety buss kwa sasa wapo wajasiliamali wengi wadogo na wa kati. Endapo lipo swala la usalama bora serikali ingejipanga kuagiza bulk pekee.
 
Back
Top Bottom