Serikali yaajiri walimu hewa(?) Ushahidi huu hapa...

Halafu hii ofisi ya Tamisemi si ipo chini yake
 
Punguza ufukunyuku bana unaharibia watu kazi [emoji49][emoji48][emoji48][emoji49][emoji49]
 
Mimi haya ya majina nayaona karibia kila mwaka.

Kingine kilichonishangaza ni kitendo cha TAMISEMI Kuipatia wilaya ya Mbarali walimu wawili tu wa Sekondari tena wote shule moja ilihali kuna shule haina mwal wa Physics hata mmoja.

Wakati huo huo wilaya zingine kama Chato na Ruangwa zikipewa walimu wa sekondari zaidi ya 15 kila wilaya na ajabu zaidi kuna shule moja huko Chato imepewa walimu wa sekondary watano.
 
Mkuu nimefatilia nakupa salute,ni kweli jina hilo moja, namba hyohyo ya mtihani,shule hyohyo lkn cha ajabu moja kaajiriwa moshi mwingine mbeya
 
Naomba nichangie kama ifuatavyo......
1.Katika mfumo wa uombaji wa hizi ajira hakukuwa na uwezekano wa kufuta akaunti ya kuombea ajira mara baada ya kuifungua.
2.hakukuwa na uwezekano wa kudelete attachment kama vyeti vya sekondari au taaluma iwapo mtumaji anahisi ametuma kwa makosa.
3.mtandao ulikuwa unasumbua sana sana tena zaidi ya sana wakati wa kuomba isipokuwa siku chache kabla ya deadline kutimu.
Hivyo basi waombaji wengi walifungua akaunti zaidi ya moja huku wakiambatanisha document zilezile kwa sababu ya kuweka maombi yao kwa usawa zaidi,kumbuka kuwa hawakuwa na uwezo wa kufuta akaunt wala kufuta uploaded document.
Kubwa zaidi documents zilisumbua saaaaaana tena sana kuzi upload.watu wakatangaziana kufungua akaunt nyingine na zitakubali kisha zikakubali.

Wizara nao hawakuwa makini kwa upande wao wakati wa uchambuzi.
 
Hakuna umakini kabisa period!! Unakuwa kama unatetea hapa!! Soma vizuri hii post ya huyu Great Thinker of the year, idadi ya walioajiriwa ni hewa!!!
 
Vipi documents mtu kahitimu 1994, huku majina yanafanana number za mwisho zitofautiane, Ku create majina tifauti hakufanyi hyo issue itokee
 

Ila mkuu kwa ninavyofahamu, ukiingiza data kwenye database zinazofanana si ina ku alert. Hawakuliona hilo
 
So uko upande upi?
Kupanga hayo majina wanatumia no ya mtihani kidato cha nne. Hata uombe kwa kutumia akaunti 100 no ya mtihani ni ile ile.
 
Kwa hiyo unataka kushindana na chato? Kwani mbarali walipewa intaneshino eapoti? Benki ya gorofa? Taa za "njiani"? Utapata tabu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…