Jayfour_King
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 1,135
- 128
Ni lazima tufahamu kwamba historia haina reverse, kwa maana kwamba yaliyotokea yametokea lakini kwa vyovyote vile waliokuwa wakimpenda na wale wanaodhani kwamba walikuwa wakimchukia, wote watamkumbuka kama mtu aliye lipenda taifa lake pamoja na mapungufu yote aliyokuwa nayo kama binadamu.
Na kilichomponza ni nia yake ya kutaka kuunda USA ( Africa ). Hii iliyatisha sana mataifa ya ulaya kwa sababu Ulaya imefilisika na tegemeo la utajiri wa ulaya ni wizi unaofanywa sehemu mbali mbali za Africa uwe wa dhahiri au uliojificha. Wizi wa dhahiri ni kama iivyo kule Congo (RDC/DRC) na uliojificha ni kama huu wa hapa kwetu ambapo watu hujifanya hamnazo na kuingia mikataba mibovu kwa niaba ya nchi kwa makusudi.
Kwa wale watakaobisha kuhusu hili kwamba Gaddafi hakuwa na chochote kizuri kwa Libya watuambia kwa idadi na majina ni nchi gani duniani ambazo zinatoa huduma kwa wapiga kura wao kama alivyokuwa akifanya Gaddaffi.
Binafsi kama mtanzania ningefurahi kuwa na aina ya viongozi kama Gaddafi hapa kwetu na awe mwizi kwa kiwango cha Gaddafi ila pia atoe huduma za jamii kama alivyofanya Gaddaffi, hii watanzania wanaihitaji sana hasa katika gawio la keki ya taifa ili ifike kwa kila mwananchi bila kujali chama atokacho.
Tunapozungumzia demokrasia sijui tunamaanisha nini? Mfano kama hapa kwetu kiwango cha demokrasia ni kitu cha kufikirika kwa kuwa matokeo ambayo hutangazwa sio uamuzi wa wapiga kura ila tume ya uchaguzi ambayo ni ya chama tawala.
Mungu ibarika Africa yenye viongozi waoga ambao wanaweza kutochukua hatua yoyote mpaka kiongozi mwenzao akiuwawa na wakoloni ndipo huja na kulalamika wakati haina tija yoyote.
Rest In Peace my hero!