Nafasi za kazi za Uuguzi Saudia

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,438
1,388
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza ajira 500 za Wauguzi wa kike ambao wataajiriwa na Serikali ya Saudi Arabia mapema mwezi January mwaka 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na dhamira yake thabiti ya kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa za ajira zinazojitokeza kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali duniani.

Mhandisi Luhemeja amesema hivi karibuni mwishoni mwa mwezi November na mwanzoni mwa mwezi December, 2023, Serikali ya Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya kazi na ajira na Serikali ya Saudi Arabia pamoja na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Amesema hati za mashirikiano zilizosainiwa zinatoa fursa za ajira kwenye Mataifa husika kwa kada na sekta zenye kutumia ujuzi wa chini, ujuzi wa kati na ujuzi wa juu.

Amesema Watanzania wote wenye sifa na ujuzi uliobainishwa wanataarifiwa kuomba kazi husika kwa kujisajili NLMIS na kutuma wasifu binafsi (CV) kwa njia ya barua pepe esu@taesa.go.tz ambapo mwisho wa kutuma maombi ni December 27 2024.
---
VACANCY ANNOUNCEMENT

REQUEST FOR EXPRESSION OF INTEREST FROM QUALIFIED TANZANIAN NURSES FOR EMPLOYMENT IN THE KINGDOM OF SAUDI ARABIA UNDER THE BILATERAL AGREEMENT ON RECRUITMENT OF WORKERS

Background In November 2023, the governments of the United Republic of Tanzania and the government of the Kingdom of Saudi Arabia signed a Bilateral Agreement on Recruitment of Workers from Tanzania to the Kingdom of Saudi Arabia. The Agreement allows Tanzania labour force possessing various qualifications to be recruited to work in Saudi Arabia.

The Prime Minister’s Office – Labour, Youth, Employment and Persons with Disability through the Employment Services Unit (TaESA) has been mandated to spearhead implementation of the Agreement in terms of recruitment and facilitating migration of qualified candidates to the Kingdom of Saudi Arabia. The implementation of the agreement will be carried out in collaboration with other stakeholders including Public Institutions, Workers, Employer and Private Employment Services Agencies.

It is in this vein, the Prime Minister’s Office – Labour, Youth, Employment and Persons with Disability through the Employment Services Unit (TaESA) in collaboration with Dalba Consulting Group Company from Saudi Arabia on behalf of the Ministry of Health of the government of The Kingdom of Saudi Arabia wish to inform the general public that, recruitment of the first batch of 500 female Nurses targeted for recruitment under the Agreement are is in the process.

The Prime Minister’s Office – Labour, Youth, Employment and Person with Disability therefore invites interested and eligible candidates to register and compete for the opportunities as specified below:-



1702918458336.png

1702918494016.png


 

Attachments

  • TANGAZO - AJIRA ZA WAUGUZI SAUDIA.pdf
    159.8 KB · Views: 8
Serikali ya Tanzania Imetangaza Nafasi 500 Kwa Wauguzi wa Kike ambao Wataajiriwa na Serikali ya Saudi Arabia Ili kwenda kufanya kazi Nchini humo mapema mwaka 2024.

View: https://www.instagram.com/p/C1APjjyCoIf/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Wenye sifa ombeni maana mtaajiriwa na Saudia na kulipwa madolali.

Hivi hii nchi inaviongozi au Ina makapi ya viongozi? We watu unajua wanawanyanyasa watanzania kibao kwenye social media na bado uruhusu watu kwenda kufanya kazi hawajielewi hawa
 
Hivi hii nchi inaviongozi au Ina makapi ya viongozi? We watu unajua wanawanyanyasa watanzania kibao kwenye social media na bado uruhusu watu kwenda kufanya kazi hawajielewi hawa
Wewe ndio makapi,Mama Yako alinyanyaswa huko? Mpumbavu nini,watu wanaenda kwenye contract rasmi unaleta upuuzi wako hapa.
 
Doctors hawataki wanataka ma nurses.
Tena Kwa msisitizo wanataka wa kike.

Huu ni mtego Kwa dadazetu.
Hao wanaitwa MANESI, lakini wanakwenda kufanya kazi za kuwaosha wazee na vibibi visivyojiweza kwenye nyumba za kulelea wazee.

Wawe tayari kukamata mavi, mikojo na makamasi ya vigagula na vijeba
 
Kwani, hizo huduma nchini zimetosha hakuna uhitaji? Kwa nini wapambane kupeleka watu,na siyo watu kuja kufanya kazi huku?
Ina maana hata viongozi wana imani kwamba sasa uwezo hawana,wameamua kuwatesa raia!!! Nani alisema uarabuni watu wanaishi kwa raha? Je, ni kwamba waTanzania wana elimu nzuri kuliko wao?

Hii kitu mara mia serikali ingekubali ushauli wa walengwa,sidhani kama wapo ambao wamedhamilia kwenda.
Utakuta nchi bado ina uhitaji mkubwa,na haina watu,lakini waende tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom