Fursa za ajira Uarabuni, Saudi Arabia sekita ya afya.

Fursa za ajira Uarabuni, Saudi Arabia sekita ya afya.

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
13,682
Reaction score
41,162
Watanzania 500 Wauguzi Wanawake Kunufaika na Ajira Nchini SAUDI ARABIA. Sifa Diploma au Bachelor degree na awe Mwanamke Mtanzania. Tuma maombi au CV yako NLMIS au esu@taesa.go.tz Mwisho wa kupokea maombi 31Dec.2023. Watakaofanikiwa tarehe 10Jan.2024 watakutana na Waziri mama Ndalichako.
 
Watanzania 500 Wauguzi Wanawake Kunufaika na Ajira Nchini SAUDI ARABIA. Sifa Diploma au Bachelor degree na awe Mwanamke Mtanzania. Tuma maombi au CV yako NLMIS au esu@taesa.go.tz Mwisho wa kupokea maombi 31Dec.2023. Watakaofanikiwa tarehe 10Jan.2024 watakutana na Waziri mama Ndalichako.
Mods walifuta mada yangu ya Ajira za Saudia sijui Huwa Wana shida gani?
 
Asante kwa Bandiko Mkuu.

MAENDELEO HAYANA CHAMA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Wajiandae na utumwa! Maana mwarabu anaona mtu mweusi kama kijakazi tu
Wapi katika dunia hii mtu mweusi ana thaminika kama sio nchi yake ya asili, endelea kujidanganya na kudanganya wajuaji wenzako kwamba mkienda Ulaya mtaheshimiwa na kubembelezwa,
 
Ujinga uliokithiri, huku kwenyewe tuna shida ya wahudmu wa Afya hawatoshi, na hata waliopo tunawalipa kiduchu hakafu tunajitia ufahari wa kupeleka wahudumu wa Afya Saudia, TUACHE UJINGA.

Serikali iboreshe huduma za afya zitosheleza na ziwe za kisasa na hiyo ziada ndio iende huko Saudia na kwingineko.

India imejitoshereza kwenye suala la wahudumu wa Afya ndio maana wengi hutoka nje kutafuta mkate, Kenya kwa miaka mingi toka ya 1980 na 1990's imekuwa bora kwa kiasi chake kwenye huduma za Afya kiasi cha watu wengi kwenda kutibiwa huko kutokea TZ... ndio maana nao huruhusu madaktari wao na manurse kwenda huko.

Serikali iache kujificha kwenye siasa na kutafuta sifa za kisiasa huku ukweli ukituumbua, Taifa bado linahitaji wahudumu wa Afya tena walio competent na vifaa na kuboresha mishahara yao pia..

Ni Hatari kwa Taifa maskini kushindwa kulinda na kutengeneza ajira za watu wake ili wajenge Taifa lao na baadala yake eti kujifanya inatafutia watu wake fursa huku ukweli yenyewe imeshindwa..

China ilijijenga kwanza na kutengeneza uwezo wa watu wake kiasi cha kutosheleza mahitaji ya ndani ndio ikaacha milango wazi watu wake kutoka sass na kwenda kufanya ujanja kwingine na kurudisha hela ndani ~ tena kwa umakini mkubwa wanajitahidi kuhakikisha uchumi unachukuliwa kwingineko na kuuleta ndani..

Bado tunahitaji nguvu kazi kulijenga Taifa na kujenga mifumo imara, haya yote yanahitaji nguvu kazi imara na yenye maarifa.

Kama Saudia wameweza kutumia resources zao vizuri na kuwafanya watu wengine kuwa watumwa wao kiasi cha wao kufanya huduma bure za matibabu, shule bure mpaka University, kukopesha watu wao mikopo bila riba nk.. SISI TUMESHINDWAJE KUTUMIA RESOURCES ZETU NA KUBORESHA MAISHA YA WATU WETU?
 
Back
Top Bottom