Serikali ya Samia Imewezesha Mashirika ya Umma Yaliyokuwa yanaleta Hasara Kujiendesha Kwa Faida.Yamo TANESCO na TRC

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
79,084
Reaction score
84,976
My Take
Samia ataendelea kusalia kama Rais aliyefanikiwa sana kwenye nyanja ya Uchumi na biashara hapa Tanzania.

Mageuzi aliyoyafanya kwenye mashirika haya ya Umma yamefaulu ,hatutegemei tena hasara huko tuendko.

Bado mashirika machache sana mfano Air Tanzania na TTCL.

Pia soma Ojambi Masaburi: Rais Samia amebadili historia mbaya ya Tanesco kutoka kuleta hasara hadi kuingiza na kutoa gawio kwa Serikali | JamiiForums Ojambi Masaburi: Rais Samia amebadili historia mbaya ya Tanesco kutoka kuleta hasara hadi kuingiza na kutoa gawio kwa Serikali
================
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imesema imeridhishwa na hali ya uzalishaji wa umeme , ambapo sasa nchi ina uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 4,400 huku matumizi yakiwa ni megawati 2,071 hatua ambayo imeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme.

Hayo yamejiri Februari 20,2026 baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo imetembelea Kituo cha Kusafirisha Umeme kwenda Zanzibar cha Ras Kilomoni na Kituo cha kuzalisha Umeme kwa Gesi Asilia cha Kinyerezi I na II.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Subira Mgalu, amesema kumekuwa na maendeleo makubwa katika eneo la uzalishaji wa umeme, na sasa TANESCO inaendelea na jitihada za kujenga njia za kusafirisha umeme, ikiwemo ya kutoka Bwawa la Julius Nyerere hadi Chalinze, kisha Kinyerezi hadi Mkuranga, eneo lenye viwanda vingi vya uzalishaji.

“Tunaipongeza sana TANESCO kwa utekelezaji wa miradi ya umeme. Ile hali ya kukatika kwa umeme imepungua, na sasa hakuna mgao. Kamati inashauri kuwa nguvu kubwa sasa itumike katika kuhakikisha umeme unamfikia mlaji wa mwisho, hususani katika maeneo ya viwanda na migodi,” alifafanua Subira.
 
Kwani mkuu kama tanesco walikua wanapataje hasara ikiwa Luku watu wanaweka kila siku?wataalam wa umeme nipeni elimu
 
Subiria taarifa zao mwisho wa mwaka wa fedha.

Mfano Tanesco Toka mwaka Jana wanapata faida
Chawa unasema toka mwaka jana gani? Hizo story za tanesco kupata faida kila mwaka story zile zile. Utaongopea machawa wenzako na hao viongozi wako mabumunda

Hii ilikua 2012 mlisema mmepata faida
Screenshot_20260220-205532_1.jpg

Hii Ni 2021 mlisema mmepata faida
Screenshot_20260220-205715_1.jpg

Hii 2023 mlisema mmepata faida bilion 109 mkasema mmeweka rekodi wakati 2012 mlisema faida ilikua bilion 120
Screenshot_20260220-205604_1.jpg
 
Ukisikia hizo faida kwa mashirika ujue mwananchi ndiye anaumia wala siyo suala la kuchekelea labda kama mtu anaishi kwa shemeji yake!

Mfano:Ukihitaji nguzo moja kuunganisha umeme kwa sasa ni 520,000/= hii ni Jan 2026.

Ukiunganishwa leo Feb 20 basi ukinunua LUKU mara ya kwanza unakatwa kodi ya jengo ya toka mwaka huu wa fedha umeanza ie July 2025! Haijalishi jengo lilikuwepo au la!

NB: Mwanzoni tuliambiwa fulani hataki kodi za dhulma.
😁

BTW: ATCL nayo imeanza kutengeneza faida??
 
My Take
Samia ataendelea kusalia kama Rais aliyefanikiwa sana kwenye nyanja ya Uchumi na biashara hapa Tanzania.

Mageuzi aliyoyafanya kwenye mashirika haya ya Umma yamefaulu ,hatutegemei tena hasara huko tuendko.

Bado mashirika machache sana mfano Air Tanzania na TTCL.

Pia soma Ojambi Masaburi: Rais Samia amebadili historia mbaya ya Tanesco kutoka kuleta hasara hadi kuingiza na kutoa gawio kwa Serikali | JamiiForums Ojambi Masaburi: Rais Samia amebadili historia mbaya ya Tanesco kutoka kuleta hasara hadi kuingiza na kutoa gawio kwa Serikali
================
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imesema imeridhishwa na hali ya uzalishaji wa umeme , ambapo sasa nchi ina uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 4,400 huku matumizi yakiwa ni megawati 2,071 hatua ambayo imeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme.

Hayo yamejiri Februari 20,2026 baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo imetembelea Kituo cha Kusafirisha Umeme kwenda Zanzibar cha Ras Kilomoni na Kituo cha kuzalisha Umeme kwa Gesi Asilia cha Kinyerezi I na II.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Subira Mgalu, amesema kumekuwa na maendeleo makubwa katika eneo la uzalishaji wa umeme, na sasa TANESCO inaendelea na jitihada za kujenga njia za kusafirisha umeme, ikiwemo ya kutoka Bwawa la Julius Nyerere hadi Chalinze, kisha Kinyerezi hadi Mkuranga, eneo lenye viwanda vingi vya uzalishaji.

“Tunaipongeza sana TANESCO kwa utekelezaji wa miradi ya umeme. Ile hali ya kukatika kwa umeme imepungua, na sasa hakuna mgao. Kamati inashauri kuwa nguvu kubwa sasa itumike katika kuhakikisha umeme unamfikia mlaji wa mwisho, hususani katika maeneo ya viwanda na migodi,” alifafanua Subira.
Siyo kweli kuwa TRC inajiendesha kwa faida, kila mwaka TRC inaleta hasara, kwanini unadanganya, hata hiyo TANESCO ina hali mbaya licha ya ruzuku kutoka serikalini, Mbona huongei kuhusu ATC na mashirika mengine mizigo kwa nchi hii. Hata kama una mapenzi na kiongozi, usidanganye. Kuna mambo mengi ambayo hayaendi sawa katika uongozi huu, Mnampaka rangi huyo Samia lakini hasafishiki. Mnapoteza muda bure, watanganyika siyo wajinga, tunaelewa kila kitu. Usione watu wamenyamaza ukajidanganya kwamba ni wajinga. BTW mnalipwa kiasi gani kutetea uongo?
 
Umejuaje imepata faida kama taarifa za mwisho wa mwaka wa fedha bado hazijatoka??

Mwaka Jana TANESCO wamepata faida ya shillingi ngapi?
Kupoteza muda tu hawa machawa na viongozi wap wote mabumunda kichwani sifuri ndio maana bibi ana elimu mbalimbali
Toka 2012 stoet za tanesco kupata faida ni zilezile alafu yalivyo mehu yanasahau
Hii 2012 yalisema faida ilikua bilion 120
Screenshot_20260220-205532_1.jpg

2023 yakasema yamepata faida bilion 109 wamevunja rekodi ya faida, yashasahau kuwa 2012 yalisema yalipata bilion 120
Screenshot_20260220-205604_1.jpg
 
Umejuaje imepata faida kama taarifa za mwisho wa mwaka wa fedha bado hazijatoka??

Mwaka Jana TANESCO wamepata faida ya shillingi ngapi?
Kuna nyakati msiwe mnahangaika kujibizana na hawa wapumbavu wanaolipwa kusifia mafanikio hewa ! hawa tungewajua kwa sura zao mitaani tungemalizana nao kwa kugawanya viungo km Bibi vizee wachawi kule kanda ya Ziwa.
 
Chadomo mtapata tabu sana Kwa kubishia ukweli
 
Back
Top Bottom