Serikali ya Marekani yasutwa kuhusu Apple

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
o
160301031652_apple_brooklyn_624x351_afp.jpg


Kampuni ya Apple
Jaji mmoja mjini New York ametoa uamuzi kuwa serikali ya Marekani haiwezi kuilazimisha kampuni ya Teknolojia ya Apple, kupatia shirika la ujasusi la Marekani FBI uwezo wa kufungua simu za iPhone zilizotumiwa katika visa vya mihadarati.

Serikali ilitaka ipewe uwezo wa kufikia taarifa za simu hizo mwezi October ikiwa ni mwezi mmoja kabla jaji wa California kuamuru Apple kusaidia kufungua simu ya iPhone ya raia mmoja aliyeuwaua watu 14 .


160226022346_apple_iphone_protesta_624x351_getty_nocredit.jpg

Kesi ya Apple
Apple imesema FBI inataka mamlaka hatari na hatua ya kuvunja haki za kikatiba .

Kesi hiyo ya California ilizua mjadala wa kitaifa nchini Marekani juu ya uwiano kati ya usalama na haki ya mtu kuwa na mambo yake binafsi

Serikali ya Marekani yasutwa kuhusu Apple - BBC Swahili
 
Hizo nchi za wenzetu. Uhuru wa mtu hauruhusiwi kuingiliwa na yeyote hata nchi.

Ingekuwa Afrika, hao apple wangeshafukuzwa.
Hao Raia wa nchi hizo wana Nidhamu na kutambua mipaka ya sheria na kanuni. Sisi miAfrika ukitupa uhuru utajuta wiki ya kwanza tu.
 
Back
Top Bottom