Serikali ya Kikwete isiichezee Mahakama ya Rufani


Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
(Makala hii imetoka Tanzania Daima Feb 17, 2010)

NILIWAHI kuandika huko nyuma juu ya uhuru wa mahakama zetu. Somo hili bado halijawaingia wanasiasa wetu hususan wale waliokaa kwenye kiti cha madaraka.

Baada ya uongozi wa CCM kufanikiwa kuliingilia Bunge na kuligeuza kuwa "baraza la washauri wa serikali" naanza kuona kile ambacho nilikihofia miaka karibu mitatu iliyopita; kwamba CCM itajiinua kwa kiburi dhidi ya mahakama na mahakama zetu zitanyang'anywa uhuru wake.

Tukikubali kwamba serikali isitii uamuzi halali wa mahakama kwa kisingizio cha "kukosa muda" na kusema kuwa ni "suala nyeti" basi tutaruhusu jambo la hatari sana kwa demokrasia yetu.

Ndugu zangu, utawala wa demokrasia mojawapo ya misingi yake mikubwa zaidi ni uhuru wa mahakama. Kitendo cha Mbunge wa Mbulu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Phillip Marmo, kumjibu Jaji Mkuu na kupingana naye wazi ni kitendo cha hatari na kinachotakiwa kulaaniwa na kila Mtanzania kwani tukikubali hata kwenye usingizi tutakuwa tumewapa watawala wetu nguvu wasizokuwa nazo.

Nazungumzia nini? Mahakama ya Rufani ya Tanzania imeanza kusikiliza rufaa ya serikali kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ambao uliruhusu wagombea binafsi katika kesi iliyoletwa na Mchungaji Christoper Mtikila. Rufaa hiyo imekuja baada ya Mchungaji Mtikila kushinda mara mbili sasa kwenye mahakama zetu ambapo mara hizo zote mahakama zimekubali kuwa kulazimisha Mtanzania kugombea nafasi ya uongozi kwa kupitia chama cha siasa ni kinyume na Katiba.

Ni kutokana na hilo katika hukumu yao ya mwisho kwenye suala hili Mahakama Kuu iliamua kuwa hukumu ya awali ya Lugakingira (mwaka 1995) inaruhusu wagombea huru na wao (mwaka 2006) waliona zaidi ya kusema kuwa wagombea huru wanaruhusiwa tu (kama alivyofanya Jaji Lugakingira) bali pia ilitoa amri kwa serikali kuhakikisha kuwa inaandaa mpango na utaratibu wa jinsi gani wagombea huru watashiriki uchaguzi mkuu ujao (yaani wa 2010).

Sasa, serikali ikakusudia kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu. Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, ndiye aliyetekeleza maagizo ya viongozi wa kisiasa kukata rufaa.

Sababu kubwa ya watawala kukataa wagombea binafsi ni kuwa "Tanzania haiko tayari kuwa na wagombea binafsi" na pia hawawaamini Watanzania kuwa wanaweza kumchagua mtu anayewafaa bila kuangalia chama chake.

Hata hivyo ukweli ni kuwa endapo wagombea binafsi wataruhusiwa Chama cha Mapinduzi ndicho kitakachopoteza sana kwani hadi hivi sasa kinaendeleza itikadi ya uongo kuwa wabunge huchaguliwa kuwakilisha "chama" na siyo wananchi!

Ukweli ni kuwa tayari wananchi (wenye vyama na wasiyo na vyama) wamekuwa wakipiga kura kuchagua viongozi wao kwa miaka nenda rudi na ni wananchi hao hao ambao leo hii wanajikuta wanalazimishwa kuchagua viongozi ambao lazima wawe wamepitishwa na vyama vyao kugombea na hivyo Watanzania wengine ambao wanapenda kuwatumia wananchi wenzao lakini hawataki kuwa vibaraka wa vyama hivyo wanakatwa kugombea kwa sababu CCM haitaki wagombee kama watu binafsi!

Lakini zaidi wanachohofia ni uwezekano wa wana CCM ambao wataona kuwa hawawezi kusimama kugombea kwa sababu chama chao kimewaengua kwenye kura za maoni lakini wana CCM hao hawako tayari kujiunga na chama kingine cha upinzani lakini wanakubalika katika majimbo yao; sasa kwa nini hawa wasiruhusiwe kugombea kama watu binafsi na yule anayekubalika (aliye na chama au la) ndiye achaguliwe?

Nyerere aliunga mkono wagombea binafsi
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliunga mkono suala la wagombea binafsi waziwazi na pasipo kujiuma maneno. Katika hotuba yake (ambayo kila Mtanzania anapaswa kuisoma) aliyoitoa pale Uwanja wa Sokoine mwaka 1995 (kwenye siku kuu ya Mei Mosi) Nyerere alisema kuwa serikali haiwezi kufuta haki ya mwananchi kiholela hivyo.

Aliwakumbusha CCM kuwa wagombea binafsi ni haki ya msingi na inawezekana kufanyika tena Tanzania kwani tayari Tanzania imewahi kuruhusu huko nyuma. Nyerere alikumbushia jinsi TANU ilivyosimamisha mgombea asiyekubalika kule Mbulu (jimbo la Marmo!) lakini mgombea aliyekuwa akikubalika Chief Sarwatt akaenguliwa lakini akaruhusiwa kugombea kama mgombea huru. Chief Sarwatt alishinda!! Hoja ya Mwalimu ilikuwa nyepesi tu kuwa hatuwezi kuwanyima wananchi haki ya kumchagua kiongozi wanayemtaka hata kama kiongozi huyo hayumo ndani ya chama cha siasa.

Uamuzi wa Mahakama Kuu hata hivyo ulijikita zaidi katika hoja za Kikatiba. Mara zote mbili (uamuzi wa Lugakingira na uamuzi wa kina Manento) Mahakama Kuu imeshindwa kushawishika kuwa mabadiliko ya kulazimisha mgombea kuwa na chama hayakiuki haki za msingi za Kikatiba.

Jaji Lugakingira alipompa ushindi Mtikila na kurejesha timamu katika demokrasia yetu alitangaza hivi katika hukumu yake ile maarufu (ambayo natabiri itaendelea kusimama hata katika rufaa ya sasa)

"It shall be lawful for independent candidates along with candidates sponsored by political parties to contest, presidential, parliament and local council elections." Yaani, "itaruhusiwa kisheria kuwepo kwa wagombea huru pamoja na wale watakaosimamishwa na vyama vya siasa kugombea katika uchaguzi wa rais, Bunge, na serikali za mitaa".

Uamuzi wa kina Manento hata hivyo ulienda mbele zaidi; uliamua hivi:
"We shall also declare in the present case that in principle it shall be lawful for private candidates to contest for the posts of President and Member of Parliament along with candidates nominated by political parties. However unlike the learned late judge we will not just leave it at that. Exercising our powers under any other relief as prayed in the petition and cognizant of the fact that a vacuum might give birth to chaos and political pandemonium we shall proceed to order that (the government) between now and the next general elections, put in place, a legislative mechanism that will regulate the activities of private candidates. So as to let the will of the people prevail as to whether or not such candidates are suitable."

Yaani, "na sisi tunatangaza katika kesi hii kuwa kimsingi itaruhusiwa kwa wagombea binafsi kugombea nafasi za Urais na Ubunge pamoja na wagombea watakaosimamishwa na vyama. Hata hivyo, zaidi ya uamuzi wa Jaji Lugakingira sisi hatutaishia hapo tu.

Tukitumia madaraka yetu ya kutoa nafuu kama tulivyoombwa na tukizingatia kuwa tunaweza kuacha kuwe na ombwe ambalo laweza kusababisha vurugu na mgongano wa kisiasa tunatoa amri kwa (serikali) kati ya sasa na uchaguzi mkuu ujao kuweka utaratibu wa kisheria wa kusimamia wagombea binafsi. Wananchi ndio wataamua kama wagombea binafsi wanakubalika au la."

Ni kutokana na uamuzi huo hapo juu serikali ikaamua kukata rufaa. Tukumbuke kuwa uamuzi huo wa mahakama kuu ulichukuliwa Mei 2006. Hii ina maana kuwa serikali imekuwa na miaka karibu minne ya kuandaa utaratibu wa kisheria wa kuandaa sheria na namna wagombea binafsi wataweza kushiriki pasipo kuweka vikwazo ambavyo vitafanya wagombea hao kuwa na mzigo mkubwa kuliko ule wa wagombea wa vyama.

Rufaa hiyo ya serikali ndiyo imeanza kusikilizwa na kama tunavyojua ilipotajwa kwa mara ya kwanza Jaji Mkuu na majaji wengine sita wameamua kuisikiliza kutokana na uzito wake. Jaji Mkuu hata hivyo alifanya kitu ambacho ndicho hasa kinanifanya niamini kuwa CCM hawako tayari kutii Mahakama zetu na watafanya wanaloweza kuzidunisha mbele ya wananchi.

Jaji Augustino Ramadhani alisema hivi kumkumbusha Naibu Mwanasheria Mkuu: "Hata hivyo, ili kuondoa utata wowote tunapenda kumkumbusha Naibu Mwanasheria Mkuu na timu yake kuwa kukata rufaa haina maana uamuzi unaokatiwa rufaa umesitishwa mara moja. Hivyo, sheria ilivyo sasa na kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba ni kile ambacho Mahakama Kuu imeshaamua yaani wagombea huru wanaruhusiwa".

Ni kutokana na kauli hiyo ya Mahakama ya Rufani Waziri Marmo akaona kuwa mahakama ni ya kupuuzia; na amefanya hivyo bila kusahihishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wala na Rais. Kwa maneno mengine, Rais Kikwete, Baraza lake la Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wote wameamua kutotii uamuzi wa Mahakama Kuu! Yaani, kwao wako juu ya sheria!

Marmo (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia mambo ya taratibu za Bunge vile vile) alinukuliwa kusema kuwa "suala hili bado ni gumu sana na hata mahakama ikiamua hivyo, haitawezekana kwa sasa maana mpaka wananchi waulizwe kama watakubaliana na jambo hilo na liwekwe kwenye Katiba... Mtu akiachiwa nchi bila ushauri wa kikundi ni hatari sana."

Kauli hiyo ya Marmo na ambayo hadi hivi sasa naamini ndiyo kauli ya serikali kimsingi imemjibu Jaji Mkuu (mahakama yetu) kuwa haijalishi mahakama itaamua nini na itaagiza nini, msimamo wa serikali ni kuwa wagombea binafsi hawaruhusiwi mwaka huu.

Hii si mara ya kwanza
Endapo serikali itakataa kutekeleza uamuzi wa mahakama kama ilivyokwishaamriwa haitakuwa mara ya kwanza kufanya hivyo. Kwa wale wanaokumbuka mojawapo ya kesi ambazo zimezungusha sana taifa letu ni ile ya Valambhia ambayo serikali ilijaribu hata kubadilisha sheria ili isitekeleze agizo la mahakama.

Ndugu zangu, sasa hivi demokrasia yetu iko matatani na endapo kucha za watawala wetu zitakitwa kwenye migongo ya mahakama zetu basi ule uhuru kidogo tulionao ndiyo utakuwa umefikia mwisho. Endapo kina Marmo watakubaliwa wasitii mahakama zetu na waziwazi kuipinga mahakama katika kesi iliyoko mahakamani naamini ni ukosefu mkubwa wa nidhamu na kutokujua mipaka iliyopo.

Ndiyo maana natoa wito kwamba Watanzania wapuuzie kauli ya Marmo kwani ni kauli ya kipuuzi (namaanisha hilo). Ni ya kipuuzi kwa sababu kwanza tayari uamuzi wa mahakama kuu ulitolewa miaka minne iliyopita na walipewa nafasi ya kutosha kufanya mabadiliko ya sheria kuruhusu wagombea huru na walikuwa na nafasi ya kufanyia majaribio taratibu hizo katika chaguzi ndogo mbalimbali zilizofanyika miaka minne iliyopita.

Lakini hawakufanya hivyo kwa sababu hawakutaka kutii mahakama. Pili, ni ya kipuuzi kwa sababu tuna ushahidi wa kutosha wa serikali kufanyia mabadiliko sheria mbalimbali na mambo mengine makubwa ndani ya muda mfupi tu. Leo hii wameshakubaliana kuunda serikali ya mseto na tayari wameandaa kura ya maoni Zanzibar na tayari tunajua kuwa hilo litafanyika mwaka huu huu!

Lakini zaidi ni ya kipuuzi kwa sababu Marmo kama mtu wa Mbulu anajua kuwa Chifu Sarwatt ambaye jina lake linadumu kule Mbulu aligombea kama mgombea binafsi na akashinda na akachaguliwa hata kuwa Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki!

Sasa kama tulikuwa na utaratibu wa kumruhusu mgombea binafsi miaka ya sitini na akashiriki na kushinda na tukaheshimu uamuzi huo leo hii ni mwaka 2010 halafu watu wanaofikiriwa wako timamu wanadai eti haiwezekani!

Mahakama isikubali idharauliwe
Ni matarajio yangu kuwa kikao cha Mahakama ya Rufani kitakapokaa tena kuendelea na kesi hii mwezi Aprili kitachukua msimamo wa wazi kuiasa serikali kuwa kama imeshadhamiria kutotekeleza uamuzi wa mahakama hiyo kama ilivyosemwa na Marmo waseme wazi ili kesi iondolewe. Mahakama ya Rufani isikubali kuendelea na kesi ambayo maamuzi yake tayari yameshakataliwa na yule anayetakiwa kutekeleza na hasa tukizingatia kuwa wao ndiyo mahakama ya mwisho nchini mwetu!

Kama Mahakama ya Rufani itatoa uamuzi ambao unakataliwa kutekelezwa na chombo chenye nguvu kuna maana gani kutoa uamuzi huo isipokuwa Mahakama ya Rufani sasa naamini inalazimishwa mambo mawili; kwanza kutoruhusu wagombea binafsi na pili kuongeza muda ili uamuzi wowote usitekelezwe kwenye uchaguzi huu wa mwaka huu.

Lakini Mahakama ya Rufani itawezaje kuwa huru endapo wanasiasa tayari wameshaamua ni nini wangependa mahakama hiyo iamue? Tunaweza vipi kukimbilia Mahakama ya Rufani endapo pale maslahi ya CCM yanapoguswa basi watawala wanaweza kuamua kutoyatekeleza bila kujali kitakachokuwa?

Mimi naamini ni lazima utokee mgongano ambao ni muhimu kwa kukomaa kwa demokrasia. Karibu mahali pote duniani ambapo viongozi wa kisiasa wameshambulia mahakama wamejikuta wakishindwa.

Mfano mzuri zaidi ni kile kilichojaribiwa kule Pakistan wakati wa Gen. Musharraf pale alipoamua kumvua madaraka Jaji Mkuu na kusababisha maandamano ambayo yalichangia kuanguka kwake; hata kule Uganda kina Museveni walipojaribu kuingilia uhuru wa Mahakama wakajikuta kwenye matatizo ya kutosha tu! Tanzania tusikubali kina Marmo na viongozi wenzake wa CCM watunyang'anye mahakama yetu kama walivyofanya kwa Bunge.

Na kubwa zaidi ni kuwa Mahakama ya Rufani ni lazima itume ujumbe wa wazi, wa makusudi na usio na utata kuwa endapo uamuzi wake unakataliwa kabla haujatolewa au unapuuzwa baada ya kutolewa basi Mahakama nzima ya Rufani itajiuzulu hadi serikali itoe kauli isiyo na utata kuwa uamuzi wowote wa Mahakama ya Rufani utazingatiwa na kutekelezwa. Kuna wakati ambapo watu huyumba; na kuna wakati watu huchukua msimamo. Huu ndio wakati kama huo.
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
21,829
Likes
150
Points
160
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
21,829 150 160
Mwanakijiji... i wish ungekua unashauri haya kwa serikali makini!! hii iliyopo sidhani hata kama inatunza kumbukumbu ya matukio ya nchi hata monthly, achilia mbali kuheshimu mihimili yake yenyewe

Labda tutunze huu ushauri kwa serikali ya awamu nyingine... i am terribly disappointed na hali ya sasa... tunashindwa kufanya hata maamuzi madogo
 
E

echonza

Senior Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
163
Likes
2
Points
0
E

echonza

Senior Member
Joined Jun 25, 2009
163 2 0
Dawa ya kufanikiwa kuwakomesha serikali wanaoelekea kudharau mahakama ni kuwaelimisha wananchi haki yao juu ya hili. Kimsingi ni wachache tu tena walioko mjini wanaweza kununua gazeti na kuweza kusoma kilicho muhimu katika maisha yao, hasa inapokuja suala zima la manufaa yatokanayo na uchaguzi (wananchi kuchagua wawakilishi wao). Tukiweza hilo, hata kama serikali watagoma kutekeleza yaliyoamliwa na mahakama, basi wananchi watawachukulia hatua haraka sana maana uelewa watakuwa nao. Labda wana JF tujiulize, ni namna gani tunaweza sasa kwa muda huu mfupi uliobaki kuwaelimisha wale wasiopenda kusoma magazeti na wengine waliowengi waishio vijijini pasikofikiwa na magazeti hata hudu ya internet kama hivi.

Hakuna shaka juu ya haki hii ya msingi ambayo iko hatua ya mwisho kupokonywa na CCM kutoka kwetu kwa kutunyima haki mbili:
1. Kushiriki kwa wale wanaopenda kugombea uchaguzi mkuu ujao kama wagombea binafsi;
2. Kutopata nafasi ya kupata watu tunaowatarajia kutupa matumaini, maana watakaokuja kupitia CCM tutakuwa tumechaguliwa na vikao vya chama pasipo kuangalia sisi tunahitaji mtu mwenye sifa gani.
Tu wachache tunaofahamu madhara ya kutotekelezwa uamuzi wa mahakama hasa kwenye uchaguzi ujao kwa sababu za kijinga zilizotorewa na akina MARMO na wengine watokao CCM.

Hebu tujadili sasa yaliyo ya msingi kuhusu hatua za kufanya. Hilo lilikuwa wazo langu, naarika sasa wana JF kama wana mapendekezo ama mawazo mbadala walete tujadili mstakabali wa ustawi wa taifa letu.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
Patrick Kisembo

Lawyers plan to file a case in the Constitutional Court to postpone the October General Election if the government fails to amend the laws barring private candidates from contesting.
The Legal and Human Rights Centre Executive Director, Francis Kiwanga said in Dar es Salaam yesterday that activists were waiting to see whether the government would in the 19th Parliamentary Meeting bring amendments to the laws to allow independent candidates in the polls.
"We have received many calls and ideas from many lawyers and advocates to ensure that independent candidates participate at all levels of the General Election," he said.
Kiwanga further said that legal activists were planning to mobilise Tanzanians countrywide to push for the right.
"We urge the government to establish and hasten the preparations to have independent candidates contesting at all levels of leadership," he said.
Kiwanga said the Attorney General's Office through the Deputy Attorney General, George Masaju and State Minister, Prime Minister's Office-Policy, Coordination and Parliamentary Affairs, Philip Marmo contradicted the Court of Appeal's ruling on independent candidates.
"The statements completely infringe on the order of the Court of Appeal; they underrate democracy and are a contempt of a court which has the constitutional mandate as one of the three pillars to interpret and observe justice in this country," said the lawyer.
He said comments by the Deputy AG that the government cannot implement the High Court order because it was against section 14 (3) of the 1994 Act on implementation of basic human rights was to fail to interpret correctly the law thus misleading the public and to purposely refuse to abide with the Court's ruling.
He said Marmo's statement shows purposely that the government has rejected to abide by the Court of Appeal's order which was supposed to be respected and implemented immediately.
"To refuse to abide by the Court's order is not only to stump the country's rule of law, but is also a criminal offence and the government must be responsible for this," he said.
He said if a bill can take a day or two to be discussed and passed, he did not see why the government should fail to table a bill in June's parliamentary session on independent candidates.
Winding up the debate for the Electoral Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2009 in the National Assembly, Marmo said under the current legal framework it is impossible to have presidential candidates.
According to Marmo, before allowing private candidates, amendments have to be made to the country's Constitution.
A renowned lawyer, Mabere Marando said the Appeal Court ruling on independent candidates was binding and the government ought to respect it.
He cautioned the government against interfering with the court order, allowing independents to run for office in the October general elections.
Earlier this month the Court of Appeal clarified that the Attorney General's appeal against a High Court ruling did not bar independent candidates from contesting in the General Election slated for October this year.


THE GUARDIAN
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,183
Likes
29,866
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,183 29,866 280
Mzee Mwanakijiji, nilimsikia kwa makini Jaji Agustino Ramadhani akiaga rasmi kwa JK kuwa 31 Dec, anafungasha. Kwa mara ya kwanza alikuwa mkali kama upanga wa makali kuwili kuhusu kudharauliwa mahakama tangu kibajeti mpaka kimaamuzi, yaani msajili wa vyama vya siasa anapata bajeti kubwa kuliko ya mahakama!.

Kwa ukali huo, naombeni tutegemee shoka litaiangukia serikali kwenye suala hili, sina kumbukumbu tangu nchi hii ilipopata uhuru, haijawahi tokea kesi ya 'full bench', majaji 7, hiki ndicho kiwango cha mwisho kabisa cha uamuzi wa mahakama, hakuna zaidi ya hapo, hivyo naamini kwa dhati kabisa, watatoa uamuzi mkali na kipengele cha kukazia uamuzi huo as the only legacy atakayotuachia Watanzania.

Lets keep our hopes high, we hope for the best but also prepare for the worst!.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
Pasco.. hii ni mojawapo ya kesi nyepesi zaidi kwenda kwa mahakama ingawa ni sensitive; ni kesi nyepesi kwa sababu precedence ipo karibu nchi zote za commonwealth; unawezaje kuwa na wagombea binafsi Malawi, na Tanzania isiwezekane? Na kinyume na wengi kesi hii wala haitachukua muda mrefu; natabiri kabla ya Juni watakuwa wameshatoa uamuzi wao.
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,741
Likes
2,024
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,741 2,024 280
Mzee Marmo,kama baadhi ya makomrade wengi wenye itikadi za kihafidhina wanafikiri ni wao tu wenye kuamua nini na lini kitokee Tanzania. Wawe tayari kujifunza kwenye haya mambo ambayo tayari yameenda kinyume na matarajio ya wakuu wengi ili wasiingie kwenye vitabu vibovu vya historia.
Wakuu, hivi ukisoma sana zile mnaita "dossier" akili huwa zinaruka kichwani? Naanza kuona tabia za mazoea na kukosa umakini kwa hawa waheshimiwa waliokaa kwenye system kwa muda mrefu na pengine kuzisoma dossier nyingi sana kiasi kwamba hawaoni tena umuhimu wa kuheshimu utawala wa sheria.
What a sad story to them and their generations as well!
 
D

Donrich

Senior Member
Joined
Aug 27, 2009
Messages
106
Likes
1
Points
33
D

Donrich

Senior Member
Joined Aug 27, 2009
106 1 33
Walianza na Bunge,na sasa ni zamu ya Mahakama,sijui tanaelekea wapi,sina hakika hata kama wanaelewa vizuri ile dhana ya separation of power...anyway lets hope for the best,kwa kuwa jaji mkuu na wenzake hawavai sare za chama chochote cha siasa ninaamini haki inaweza kutendeka,maana hakuna kikao chochote cha chama kitakachomuita ili wamtishie kumvua uwanachama.
 
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
1,322
Likes
21
Points
135
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
1,322 21 135
Wakati wa Mswada wa Gharama za Uchaguzi nilisikia kuwa Marmo ni Mwanasheria. Hivi alishawahi kupractice as who?
 
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
30
Points
135
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 30 135
Kwani mahakama ya Rufani ya Tanzania inayo meno mbele ya Serikali? Majaji wote si ni wateule wa Rais? Utaweza vipi kumlaani mzazi wako na ikaw?
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
Kwani mahakama ya Rufani ya Tanzania inayo meno mbele ya Serikali? Majaji wote si ni wateule wa Rais? Utaweza vipi kumlaani mzazi wako na ikaw?
karibu dunia nzima majaji huteuliwa na marais wa nchi zao; la maana siyo uteule wao bali uhuru wao. So far.. kuanzia enzi za zamani mahakama zetu za juu zimekuwa huru sana kufanya maamuzi bila kuingiliwa na Ikulu au kudharauliwa.. angalia historia ya Mahakama Kuu wakati wa Nyerere...
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
21,829
Likes
150
Points
160
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
21,829 150 160
Mzee Mwanakijiji, nilimsikia kwa makini Jaji Agustino Ramadhani akiaga rasmi kwa JK kuwa 31 Dec, anafungasha. Kwa mara ya kwanza alikuwa mkali kama upanga wa makali kuwili kuhusu kudharauliwa mahakama tangu kibajeti mpaka kimaamuzi, yaani msajili wa vyama vya siasa anapata bajeti kubwa kuliko ya mahakama!.

Kwa ukali huo, naombeni tutegemee shoka litaiangukia serikali kwenye suala hili, sina kumbukumbu tangu nchi hii ilipopata uhuru, haijawahi tokea kesi ya 'full bench', majaji 7, hiki ndicho kiwango cha mwisho kabisa cha uamuzi wa mahakama, hakuna zaidi ya hapo, hivyo naamini kwa dhati kabisa, watatoa uamuzi mkali na kipengele cha kukazia uamuzi huo as the only legacy atakayotuachia Watanzania.

Lets keep our hopes high, we hope for the best but also prepare for the worst!.
Pasco, tuache kujipa moyo bana... huyo aliyezungumza kwa ukali alikua wapi wakati dharau zikitendeka?

  • Hao lawyers wa leo wako wapi wa kusimama na kuhoji wakati they in the system?
  • Juzi umemuona werema pale bungeni... unataka kuniambia kuna dalili ya changes
  • Kwa mfumo uliopo ambao siasa ina nguvu zaidi ya mifumo ya dola; canw e expect anything?

to be honest, i dont expect anything rather than lawyers kuchukua fomu za ubunge tu!!
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,183
Likes
29,866
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,183 29,866 280
Pasco.. hii ni mojawapo ya kesi nyepesi zaidi kwenda kwa mahakama ingawa ni sensitive; ni kesi nyepesi kwa sababu precedence ipo karibu nchi zote za commonwealth; unawezaje kuwa na wagombea binafsi Malawi, na Tanzania isiwezekane? Na kinyume na wengi kesi hii wala haitachukua muda mrefu; natabiri kabla ya Juni watakuwa wameshatoa uamuzi wao.
.
June ni mbali, April wanamaliza kila kitu na kufunga kazi. Issue ya kisheria sio uwepo wa mgombea binafsi, wanabishania legal techcalities on jurisdiction of the court over the constitution, kwamba mahakama kuu haina uwezo wa kutengua kipengele kwenye katiba kwa sababu hiyo mahakama ni subject ya hiyo katiba. Hoja za serikali ni bunge ndilo lenye mamlaka hiyo.

Hapa mtaona jinsi serikali itavyogaragazwa kwenye mafumbi na kuangukia pua, mgombea binafsi October yupo!, ila nadhani ataishia kwenye ubunge na udiwani, kwenye urais itakuwa fujo!.
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,556
Likes
2,368
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,556 2,368 280
Mkuu hawa jamaa ni kama mburura hata ukiwapigia ngoma hawawezi kucheza. Lakini nafasi bado tunayo tusifanye makosa mwezi wa kumi!
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
Pasco.. mahakama kuu tayari imeshaamua mara mbili wagombea binafsi ni mpaka nafasi ya Urais.. vinginevyo the whole argument ina collapse. Hii ni all or nothing!
 
R

Rafikikabisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2009
Messages
252
Likes
36
Points
45
R

Rafikikabisa

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2009
252 36 45
Katika kutoa maamuzi inabidi Majaji wawe makini maana wakitoa kinyume na matarajio ya serikali ya CCM kuna siku watajikuta wakiitwa NEC(DODOMA) hili kusutwa. Sasa sijui wataitwa wote saba au mmoja wao.
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
17,821
Likes
5,416
Points
280
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
17,821 5,416 280
Katika kutoa maamuzi inabidi Majaji wawe makini maana wakitoa kinyume na matarajio ya serikali ya CCM kuna siku watajikuta wakiitwa NEC(DODOMA) hili kusutwa. Sasa sijui wataitwa wote saba au mmoja wao.
Enzi za mwalimu......ukionyesha kupingana na serikali......... utapotelea kusikojulikana ..............au wewe mwenyewe utakimbia nchi........ Lakini siku hizi utaitwa DODOMA KUJIELEZA............ Hivyo sitashangaa hata hao majaji saba wakiitwa DODOMA. Tatizo ni kuwa serikali yetu haiko tayari kukosolewa.......... kwenye kila kitu wanaona wao ndiyo wako sahihi kuliko wengine..........Ndiyo maana kuna kuitana DODOMA ili urudi kundini ......Wakishindwa katika hilo........... watakuondoa kwa namna yoyte ile.............
HEBU WAKUMBUKE WAFUATAO..........
1. Kombe.......... eti aliuwawa kwa kufananishwa na jambazi.....
2. Kolimba............ mhnnnnnn thijui............
3. Amina chifupi..............mnhhhhh baada ya kusema kuwa angewataja ............
4. Kuna mtu alifadhiri safari ya Mrema Lyatonga Mwanza enzi hizo......... uliza kilichompata
5. Kuna yule mtoto wa kuuliza swali kule Mwanza......... thi tunajuwa baada ya hapo kilifuata nini.....
6. etc....etc
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
196
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 196 160
katika uelewa wangu, Kitendo cha SERIKALI , kuingilia uhuru wa mahakama nikiashiria cha serikali inayoelekea kufa tena kifo cha aibu.
wanatambua fika kuwa Uhuru wa mgombea binafsi kwao ni janga, nasema hivyo kwasababu, hakuta kuwa na mwanaCCM atakae ogopa kuikosoa serikali eti kwasababu jina langu litaondolewa na kamati kuu ya chama, kama ilivyowahi kutokea kwa Thomas Nyimbo. . .
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,183
Likes
29,866
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,183 29,866 280
Pasco.. mahakama kuu tayari imeshaamua mara mbili wagombea binafsi ni mpaka nafasi ya Urais.. vinginevyo the whole argument ina collapse. Hii ni all or nothing!
.
Nazungumzia practicability, unless sheria itamke wazi mgombea binafsi wa urais, atajigharimia,

Kwa sasa kila mgombea urais anapewa ulinzi 24/7, logistics na media access kwenye public media kwa fedha za umma, wakijitokeza watu 100 kwenye urais, we don't have the capacity to do all that for all of them.

Maadam safari ni hatua, basi japo tuanzie na kidogo cha udiwani na ubunge, mwisho tende kwenye kikubwa cha urais, tena mgombea binafsi ni Mangi, ndie anayemfund Mtikila kwenye hii kesi, not sure kama ni mpaka sasa, ila ndiye aliyelipia kila kitu kule mwanzo.
 
Shapu

Shapu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2008
Messages
2,010
Likes
331
Points
180
Shapu

Shapu

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2008
2,010 331 180
Kwani mahakama ya Rufani ya Tanzania inayo meno mbele ya Serikali? Majaji wote si ni wateule wa Rais? Utaweza vipi kumlaani mzazi wako na ikaw?
Hata kama ni wateule wa Raisi akisha wateua hawezi kuwafukuza. So they ought to be independent of the gvt kwani kutimuliwa kwao kuna-involve commonwealth judges and other procedures.
 

Forum statistics

Threads 1,235,907
Members 474,863
Posts 29,240,042