Serikali ya Daruso yavunjwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Daruso yavunjwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Serikali Daruso yavunjwa


  na Chalila Kibuda


  [​IMG] SERIKALI ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es es Salaam (DARUSO), imevunjwa juzi baada ya Rais wake, Mathias Kipara, kuitoa serikali hiyo katika Umoja wa Vyuo Vikuu na Taasisi Tanzania (TAHLISO) bila kupitia maamuzi ya bunge.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Spika wa Bunge wa DARUSO, Goodruck Mwangomango, alisema kutokana na rais kukiuka Katiba ya Daruso kunachangia serikali yake kuvunjika mpaka uchaguzi utakapofika kwa ajili ya kupata viongozo wapya.
  Spika Mwangomango alisema rais alitumia mamlaka yake vibaya kujitoa Tahiliso pasipo kushirikisha bunge ambalo ndilo lenye maamuzi; hii imechangia serikali ya Darsuso kuvunja uaminifu kwa wanafunzi waliowachagua.
  Alisema serikali ya Daruso ilijiunga kupitia bunge, hivyo hata kujitoa ilihitajika bunge kutoa maamzi yake kama chombo cha mwisho cha maamuzi.
  Aidha, alisema serikali hiyo kwa sasa itaongozwa na wenyeviti wa vitivo mpaka uchaguzi utakapoitishwa tena kwa ajili ya kuchagua viongozi wapya.
  Mwangomango alisema kuwa rais wa Daruso alijiunga Tahliso kwa kutumia bunge, hivyo hata suala la kujitoa bunge ndilo lingepaswa kutoa maamuzi.
  Aidha, alieleza kesho watatoa tamko rasmi juu ya kuvunja serikali hiyo ya wanafunzi wa Daruso na kukabidhi kwa wenyeviti wa vitivo.
  Serikali hiyo iliyokuwa na mawaziri 30, rais alikuwa Mathias Kipara, Waziri Mkuu, Paul Mapuri na Makamu wa Rais, Jacqueline Materu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Hi Daruso si ndiyo walimpa JK siku saba atengue kauli yake ya kuukwepa mkutano wa kikatiba katika kuiandika katiba mpya pale alipotangaza nia yake ya kujiundia Tume yake mwenyewe?

  Sasa kama uongozi wao umevunjwa wataandaaje maandamano yao ya kupinga Tume kuandika katiba mpya?
   
 3. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vyuo vikuu miaka hii imebaki tu majina, huko nyuma kitendo cha serikali kuua hata raia mmoja tu wasomi wa vyuo vikuu wangekua waachii nafasi hata ya kunywa maji wadhalimu walioko madarakani bila kuwajibika.

  Asiyefahamu hilo aulize kulichomfanya mzee mwinyi kujiuzulu miaka hiyo.

  Leo hii vyuo vikuu si taasisi za kutetea wanyonge tena.
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Is DARUSO still relevant? I doubt! As it stands it looks insignificant!
   
 5. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mmmh, Serikali ya wanafunzi tu mawaziri 30.,ama kweli mtoto wa nyoka ni nyoka
   
Loading...