DIT Yakabiliwa na Uchawa wa Kisiasa?

DIT Yakabiliwa na Uchawa wa Kisiasa?

amirmojaElimu

Member
Joined
Nov 23, 2024
Posts
9
Reaction score
6
KILIBA , TAHLISO, MAMA ASEMEWE
Iacheni DIT Kama TAASISI YA ELIMU YA JUU YA TEKNOLOJIA haiwezi Kuwa TAASISI YA KICHAWA


Majuma ya hivi karibuni yamekuwa na kipindi Cha ajabu Kwa sura ya Siasa ya Tanzania na DIT kwa ujumla, kwani tangu kuanze na Tukio la Michezo Ndani ya Taasisi kumekubwa na Upepo Mbaya Wenye kubadili sura ya Taasisi Kwa Mlengo wa UCHAWA na Wenye kudidimiza Taswira ya Taasisi na Utoaji wake wa Elimu ya Teknolojia.

Kumekuwepo na Matukio ambayo yameleta wasiwasi Kwa Taasis, moja wapo ni kuona VIONGOZI WA TAHLISO na TAASISI YA MAMA ASEMEWE wakitia Kambi Ndani ya DIT Kwa lengo la kubadili sura ya DIT na kuiweka katika Sura ya Taasis Ya CHAMA CHA MAPINDUZI na PA la propaganda ambazo zinaenda kuiondolea DIT uhai wake wa Kielimu na Kuwa Chombo Cha Elimu ya Propaganda kama Taasis ya Mwalimu Nyerere Memorial.

Tunatoa Rai Yenye nguvu bila Mashaka Kuwa Viongozi wa MAMA ASEMEWE na Viongozi TAHLISO wawajibike kwenye majukumu yao na kuiacha DIT kwenye Majukumu yake Muhimu ya kuzalisha Wataalam ambao sio CHAWA au sio sehemu ya PA za Propaganda za Siasa za Kihuni.

Leo tume shuhudia Kiongozi wa TAHLISO akiwa Ana hutubia Bunge la ISRC DITSO Kuwa mbinu za Wizi au Uporaji wa Uchaguzi ni halal Vyuoni kitu kinacho tufanya tuwe na Wasiwasi wa Kuingiliwa Kwa Nafasi ya kufanya maamuzi Kwa Wana Taasisi DIT na chombo chake Cha Serikali ya Wanafunzi DITSO.

Tume shuhudia Rushwa na Nguvu ya Taasisi za TAHLISO na MAMA ASEMEWE kwenye Siasa za Uchaguzi Ndani ya Taasisi ya DIT, Hali inayoweza kupelekea kubadilika Kwa Malengo ya Taasisi DIT na Kuwa kikundi Cha CHAWA waharibufu wa Mifumo ya ELIMU.

Tunatoa Rai Kwa KILIBA na timu yake Kuwa waache Wanafunzi Wa DIT wajiaamulie Taasisi Yao kuwaje.

DIT sio Chama Cha siasa, DIT sio genge la Wahuni , DIT sio ya kuleta CHAWA wa mifumo mingine kwenda kutawala sauti za Wanafunzi na Maamuzi Yao.

DIT Siyo ya Kufundishwa Uwizi wa Uchaguzi hii ni Taasis huru yenye Kujitegema haitowahi kuleta CHAWA kwenda kuharibu Taswira yake.


KATAA CHAWA KUINGIA DITSO
KATAA KILIBA NA GENGE LAKE KUINGILIA MIFUMO YA ELIMU NA MAHUSIANO YA DIT
.

DIT haiwezi Kuwa dekio la Wanasiasa au Dampo la Uchafu wa Wanasiasa Uchwaraa.
 
DIT solid ilikuwa zamani, sasa hivi michanganyo mingi na siasa kibao na huwezi kuondoa hiyo hali kwa sasa isipokuwa itazidi kuwa juu
 
Back
Top Bottom