Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 3,579
- 2,906
CHADEMA NJOONI MBISHE KAMA HAMJAPEWA PESA ZA NO REFORMS NO ELECTION NA SERIKALI YA CCM.
Rais Samia ameliwezesha Baraza la Vyama vya Siasa kufanya mikutano sita (6) na baraza hilo kutoa mawazo na ushauri uliowasilishwa Serikalini na kufanyiwa kazi.
Kufuatia mashauriano yaliyowahusisha wadau wote wa kisiasa, Bunge lilitunga Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 2024, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 2 ya Mwaka 2024, Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, na Sheria ya Gharama za Uchaguzi. Kwa mara ya kwanza, katika historia ya nchi yetu, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliundwa kwa sheria yake yenyewe.
Tulifanya ili kujibu rai ya muda mrefu ya wadau wa kisiasa nchini. Miongoni mwa maboresho kwenye Sheria ya Uchaguzi yalikuwa ni kuongeza takwa la kila mgombea kupigiwa kura hata akiwa mgombea pekee, hatua ambayo inafuta kilichojulikana kama mgombea kupita bila kupingwa.
Vilevile, utungaji wa Kanuni za uendeshaji wa uchaguzi ulifanyika, na Serikali imeendelea kuimarisha uendeshaji wa shughuli za vyama vya siasa nchini, ambapo hadi Juni, 2025, Serikali imetoa ruzuku ya Shilingi bilioni 87.81 kwa vyama vinavyostahili kupata ruzuku kama CCM, CHADEMA, ACT et el.