Serikali ya CCM na mnara wa babeli (Tanzania)

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,879
1,125
wadau tuijadili serikali ya ccm hapa ilipofikia.
nani anayebisha kuwa hatupo pale walipofikia waliokuwa wanajenga mnara wa babeli ili kumfikia mungu.
nani asiyeona uwezo wa kiongozi mkuu wa kuujenga mnara uwezo wake,jana akihutubia umoja wa vijana wa watoto wa wajenzi wa mnara alisema,nanukuu chama chetu kinasemwa vibaya na watu.
hapo ndipo alipofikia mjenzi mkuu.

nani alimtuma chenge atuletee magogo(RADA)wakati tulikuwa kwenye msingi?
nani alimtuma mramba udongo(NDEGE YA RAIS)wakati tunatumia mchanga na siment?
ni nani ameruhusu rasilimali za ujenzi wa mnara(MADINI NA WANYAMA) ziibiwe?
kwa nini foreman (RAIS)hatulii saiti?
kwa nini wazee wetu hawasimamii kumwagilia zege?
kwa nini mama zetu(UWT) tuliowapa jukumu la kutupikia ugali kwa ajili ya kazi ngumu wanatupikia uji saa 8?
Je watoto wa wasimamizi wa ujenzi(UVCCM)walioshuhudia na kuwapa wazazi wao sapoti ya kutuletea mkaa wakati tukihitaji siment wataweza kuwageuka baba zao na kuendelea na ujenzi?
Kwa nini vibarua wa ujenzi(WAISLAMU NA WAKRISTO)lugha zinaanza kubadilika,wengine wananawa na wengine wanakoroga zege?
Je huu mnara(TANZANIA)mungu hauhitaji ujengwe?
Je ni wakati wa kuangalia kiwanja tulichokitelekeza(TANGANYIKA) ili kujaribu kujenga mji badala ya mnara?
Je ni wapi walipopata mafunzo wasomi wetu kuwa ukimwagilia zege kwa kutumia pombe(MIKATABA MIBOVU) inakuwa imara zaidi ya maji?

Wadau kuna mengi tunayofanya na tuliyofanya na mpaka sasa kwa mtizamo wangu kuta zina nyufa kibao na kubomoa ni kazi ngumu sana kwa maoni yangu tungewatimua wasimamizi wa ujenzi(CCM)na kuutelekeza mnara(MUUNGANO)na kurudi katika nchi yetu(TANGANYIKA)na mungu atatusamehe.

Haya ni maoni yangu kama mwananchi mzalendo wa nchi,watu wake na rasilimali zake.
karibuni.
 
Ccm haina jipya,business as usual!wachina hong- kong wamekamata pembe za ndovu toka tanzania,govt inasema zitakua zimetoka zambia au drc sii kwetu bila hata ya uchunguzi
 
Duh!!! yaani hii nchi ilipofika kwa sasa, kama huna roho ngumu waweza kuwa unashinda unalia tuu. Sidhani kama kuna serikali mbovu kiasi hiki hapa duniani. Wizi wizi, rushwa rushwa, uongo uongo, matusi matusi, kutishana kutishana, kurithishana kurithishana, kubebana kubebana, makundi makundi, ufisadi ufisadi, dhuluma dhuluma, mbaya zaidi haya yanafanywa n a viongozi tuliowapa dhamana ya kuendesha nchi kwa kuzingatia katiba ya nchi. duh!!!!
 
Aisee hadi inatia kichefu chefu. Natamani uchaguzi ungekua kesho. Hawa viongozi wetu tuwasamehe bure wana laana wote.l
 
Kiama chao 2015,tuzidi kuelimishana na kupashana habari mpaka vijijini maovu wanayotufanyia,ili iweraisi kumngoa adui ccm.
 
mwizi akishaweza kumshawishi mke na watoto kuungana nae raia wema wamekwisha kazi yao.
 
"Wanangu msijali ninakwenda safari,nikirudi nitawaletea pipi"Bado tunasubiri pipi(maisha bora kwa kila Mtz)tulizoahidiwa zitakuja lini?au baba hajarudi? Ila inaonekana amerudi na ametuletea pipi zenye ladha ya ndimu na ukwaju ambazo ni mfumuko wa bei,migomo,maandamano,vurugu za kidini,madai ya watumishi hasa walimu,nk.natamani kulia ila nani anisikilize wakati baba yuko mbali?haya kwa ufupi ndiyo maoni yangu mwanajamii mwenzenu,KIHUNGA
 
Huu ndiyo ukweli Lugha imevurugwa ndani ya serikali na hii nchi na mnara hauwezi kujengwa kamwe.
Na Mungu amewachafulia lugha hawa jamaa kwa sababu malengo yao kwa taifa letu yalikuwa ni mabovu.
 
Nilimsikiliza mkulu wakati anafungua daraja la kigamboni,alisema watu wasitoe ahadi zisizotekelezeka.Nilicheka sana,rafiki yangu alicheka zaidi.Tukaulizana,mwasisi wa ahadi za uungo ndo anasema hv? Anyway ,yako wapi maisha bora aliyoahidi watanzania, rushwa papa aliyoahidi kupambana nayo imeshatokomea? Je mahakama ya kadhi aliyoichomeka kwenye ilani ya chama chake,ameshaileta? Wapi kasi zaidi,nguvu zaidi na ari zaidi?
 
Mi ameniacha hoi Naibu Waziri wa ELIMU tu. Sasa kama yeye ndio vile kweli elimu yenyewe duhh!!! Jamani this is too much wajameni.
 
wadau tuijadili serikali ya ccm hapa ilipofikia.
nani anayebisha kuwa hatupo pale walipofikia waliokuwa wanajenga mnara wa babeli ili kumfikia mungu.
nani asiyeona uwezo wa kiongozi mkuu wa kuujenga mnara uwezo wake,jana akihutubia umoja wa vijana wa watoto wa wajenzi wa mnara alisema,nanukuu chama chetu kinasemwa vibaya na watu.
hapo ndipo alipofikia mjenzi mkuu.

nani alimtuma chenge atuletee magogo(RADA)wakati tulikuwa kwenye msingi?
nani alimtuma mramba udongo(NDEGE YA RAIS)wakati tunatumia mchanga na siment?
ni nani ameruhusu rasilimali za ujenzi wa mnara(MADINI NA WANYAMA) ziibiwe?
kwa nini foreman (RAIS)hatulii saiti?
kwa nini wazee wetu hawasimamii kumwagilia zege?
kwa nini mama zetu(UWT) tuliowapa jukumu la kutupikia ugali kwa ajili ya kazi ngumu wanatupikia uji saa 8?
Je watoto wa wasimamizi wa ujenzi(UVCCM)walioshuhudia na kuwapa wazazi wao sapoti ya kutuletea mkaa wakati tukihitaji siment wataweza kuwageuka baba zao na kuendelea na ujenzi?
Kwa nini vibarua wa ujenzi(WAISLAMU NA WAKRISTO)lugha zinaanza kubadilika,wengine wananawa na wengine wanakoroga zege?
Je huu mnara(TANZANIA)mungu hauhitaji ujengwe?
Je ni wakati wa kuangalia kiwanja tulichokitelekeza(TANGANYIKA) ili kujaribu kujenga mji badala ya mnara?
Je ni wapi walipopata mafunzo wasomi wetu kuwa ukimwagilia zege kwa kutumia pombe(MIKATABA MIBOVU) inakuwa imara zaidi ya maji?

Wadau kuna mengi tunayofanya na tuliyofanya na mpaka sasa kwa mtizamo wangu kuta zina nyufa kibao na kubomoa ni kazi ngumu sana kwa maoni yangu tungewatimua wasimamizi wa ujenzi(CCM)na kuutelekeza mnara(MUUNGANO)na kurudi katika nchi yetu(TANGANYIKA)na mungu atatusamehe.

Haya ni maoni yangu kama mwananchi mzalendo wa nchi,watu wake na rasilimali zake.
karibuni.

Naomba kukukosoa !
Hawakujenga mnara wa babeli ili wamfikie Mungu, bali kuweka alama ya kukutania (RV) inayoonekana tokea mbali, kasome vizuri.
Pili suala la Muungano halina uhusiano na kukwama kwetu kimaendeleo.
Mwisho, CCM itakufa tu, tena kabla ya 2015.
Mengineyo upo sahihi.
 
Back
Top Bottom