Serikali ya awamu ya tano mnatuharibia nchi

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,058
2,000
Hapo vip!!
Watanzania wenzangu mnaomia kipindi hichi Poleni Sana, najua mpo wengi sana mnaotamani kusema ila mnazibwa mnomo kwa mkono wa dola.

Lakini siku itakuja hiyo dola itapeperushwa kama karatasi.

Serikali ya awamu ya tano,imekuwa inafanya maamuzi pasipo kuangalia maslahi ya Taifa na wananchi kwa ujumla ila maamuzi mengi yanafanyika kwa nia ya kulipiza visasi,kukomoa watu fulani au Kwa maslahi ya hao watawala waliopo madarakani na huku Sheria hizo zikiwaumiza wananchi na kuharibu maslahi ya Taifa.

Mfano, Sheria mliopitisha kudhibiti uhuru wa vyomba vya habari, je, hiyo Sheria inamaslahi kwa nani..?
Sheria ya kikokoteo cha mafao na haki za wafanyakazi, Je, hayo marekebisho katika hiyo Sheria yanamaslahi kwa nani?

Sheria mliopitisha kudhibiti vyama vya siasa inamaslahi kwa nani...?

Niwazi haya marekebisho yote Haya maslahi kwa wananchi ila ni kwalengo la kukomoa watu fulani na Kwa maslahi ya mtawala.

Jana mmepitisha Mswada wa marekebisho mbalimbali Namba 3,kwa lengo la kudhibiti asasi za kiraia,makampuni na vyama vya kijamii kwa maslahi ya mtawala huyu.
Serikali mmeshindwa kuleta maendeleo kwa wananchi bdo haitoshi mnaenda kuchokonoa asasi za kiraia ambao ndio wadau wakubwa wanaoleta maendeleo kwenye jamii.. Haya yote mnafanya kwa maslahi ya nani sasa?

Mnatia hasira Sana, shukuruni Tanzania kuna wajinga wengi sana.

Kama kweli hayo maamuzi mnayofanya yanamaslahi kwa wananchi, Kwanini kipindi hichi wananchi wanaoishi, chini ya dola moja kwa siku wanazidi kuongezea Kila kukicha. Kuna chanjo za bure zimepotea hospital, mfano,vituo vya angaza hakuna.

Biashara ndogo ndogo, zimekufa Sana kipindi hichi, ajira zimehadimika.Bank zinaukata wa pesa.

Jamani hii ni nchi sio familia, tusifanya maamuzi ya nchi kwa kutumia akili na hisia ya mtu mmoja ,anamka tu anamua kama anavyotaka no.

CCM ni chama kizuri Sana kwa sababu haina msingi ya dini na kikabila ila kuna watu wemefanya kionekane kibaya kwa sababu ya maamuzi yao ovyo, ovyo.
 

magomeni mapipa

Senior Member
Mar 13, 2019
115
250
Ubaguzi kama wanaukubali, wajitokeze watu wenye busara/ hekima huko CCM nadhani wastaafu wote waukemee wazi wazi.

CCM kuwa na upinzani sio dhambi, wala dini/ imani kuwa na wapinzani so dhambi, timu zinapokuwa uwanjani ni timu pinzani lakini hakuna dhambi wala kuchukiana. Wanachama na viongozi wa CCM Acha kuona wapinzani ni adui.

Hapa na JK lazima alaumiwe kuna mahala alisema mpinzani wako muombee mabaya, kuna watu ni ndugu wa damu lakini ni wapinzani wa imani , itikadi nk. Kwenye awamu ya tano mpinzani wa CCM ni adui asiye na haki, anaye stahili kuteswa, kukandamizwa, kupigwa, nk.

Hii sio sawa! Kwa mujibu wa sheria zote za ulimwenguni na mbele ya Mungu.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,335
2,000
Ni hivi hizi sheria zote zenye nia ovu zinapendekezwa na rais kwa kigezo cha kuwa ni mzalendo.

Na kwakuwa katiba inampa rais madaraka ya umungu mtu, hapo watunga sheria wanashurutishwa kutunga sheria zinazoendana na tabia ya rais ili ajira zao ziendelee kuwepo. Katika mazingira ambayo bunge ni rubber stamp, ni lazima sheria kandamizi zipite.

Ikumbukwe wengi wa wabunge huko bungeni wanapatikana bila ridhaa ya wananchi bali kupitia mianya ya katiba mbovu.
 

Diason David

Verified Member
Aug 2, 2018
7,567
1,995
Ushauri wa bure usitushauri chochote mkuu wacha tupotee shimoni tuli yataka wenyewe

tapatalk_1561680587770.jpeg
 

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,058
2,000
Ni hivi hizi sheria zote zenye nia zinapendekezwa na rais kwa kigezo cha kuwaokoa ni mzalendo. Na kwakuwa katiba inampa rais madaraka ya umungu mtu, hapo watunga sheria wanashurutishwa kutunga sheria zinazoendana na tabia ya rais ili ajira zao ziendelee kuwepo. Katika mazingira ambayo bunge ni rubber stamp, ni lazima sheria kandamizi zipite. Ikumbukwe wengi wa wabunge huko bungeni wanapatikana bila ridhaa ya wananchi bali kupitia mianya ya katiba mbovu.
Hivi na Kwa jinsi alivyokanyaga katiba, vip baadaye Nchi ikipata katiba bora na safi , hawezi kushtakiwa mahakamani,kwasababu kuna watu wengi wanasubiria kipindi kama hichi.
 

Msolopagazi

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
664
250
Nakumbuka mwaka 2017 tulivyoachishwa kazi katika mgodi wa Acacia kwa mbwembwe nyingi kwamba ni wezi tunaiba makinikia na serikali inakuja kulipwa matrilioni nchi nzima ilifurahi lakini kiukweli maelfu ya watu tulipoteza kazi na mabilioni ya kodi na mapato ya serikali na nchi kwa ujumla na mpaka leo hakuna kulichofanyika na serikali inazidi kuingia kila sekta watu wanazidi kuumia 2020 ccm watanitambua siyo mbali 😭😭😭😪💔
 

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,058
2,000
Nakumbuka mwaka 2017 tulivyoachishwa kazi katika mgodi wa Acacia kwa mbwembwe nyingi kwamba ni wezi tunaiba makinikia na serikali inakuja kulipwa matrilioni nchi nzima ilifurahi lakini kiukweli maelfu ya watu tulipoteza kazi na mabilioni ya kodi na mapato ya serikali na nchi kwa ujumla na mpaka leo hakuna kulichofanyika na serikali inazidi kuingia kila sekta watu wanazidi kuumia 2020 ccm watanitambua siyo mbali 😭😭😭😪💔
Hii Nchi kuna watu wanaona wapewaga na wengine nikama wapangaji tu.. Something which is far from the truth. Ipo siku mambo yaliyowapa wakina Bashiri na yule Rais wa misri itawapa mchana kweupe.
 

Moro¹One¹

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
505
1,000
Mungu Mkubwa na anajua zaidi, siwezi laumu, wala siwezi sifia.

Ila jamani kazi hakuna, mzunguko wa hela ili tuuze bamia pia hakuna. Mimi nawaomba wenye Nchi jamani tafuteni namna tutoke vijana, maana elimu mnayo, na Pesa mnayo.

Tusaidieni vijana, maana tumeshindwa cha kufanya, shamba pagumu, mjini hapafai. Waeshimiwa tusaidieni, Mambo yenu yaende na yetu yafae. Mnisamee kama nimewakwaza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom