Serikali/Waziri mkuu wameshindwa kusema pole kwa maafa ya Uwanja wa Uhuru Dar? Nimeogopa!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,388
Kila mtu anajua kilichotokea Dar wakati wa kumuaga JPM! Cha ajabu leo Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Mh. Waziri Mkuu amevipongeza vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kazi nzuri kipindi chote.

Jambo Hili limenishangaza watu wamekufa kwa uzembe Serikali inakaa kimyaa hata pole?

Sasa hio kazi nzuri ni ipi?

Ingekuwa nchi zilizoendelea Kuna mtu angeonesha uungwana kujiuzuru!

Hili linashangaza hakika!
 
Kweli hata mimi nimesikiliza wazungumzaji wote leo sikusikia hata mmoja aliyetoa pole kwa wahanga wa Dar. Hata Waziri Mkuu ambaye ndiye mratibu wa shughuli nzima ya mazishi amepuuza jambo hilo.

Na zaidi, kamati ya maafa iko katika ofisi yake, hivi ni kweli suala la vifo vya Dar katika mkanyagano wa kuangalia maiti ya JPM halijafika ofisini kwake?
 
Kweli hat amimi nimesikiliza wazungumzaji wote leo sikusikia hata mmoja aliyetoa pole kwa wahanga wa Dar. Hata Waziri Mkuu ambaye ndiye mratibu wa shughuli nzima ya mazishi amepuuza jambo hilo. Na zaidi, kamati ya maafa iko katika ofisi yake, hivi ni kweli suala la vifo vya Dar katika mkanyagano wa kuangalia maiti ya JPM halijafika ofisini kwake?
Ikiwa wameacha kutoa pole ya watu wote waliokufa kwa corona, haishangazi kutokufanya hivyo. Nchi zote duniani zimeweka record za watu wote waliokufa kwa corona na zinaazimisha siku walau ya kuwakumbuka, pia wanawashukuru sekta ya afya kwetu tunajifanya wajinga.
 
Ikiwa wameacha kutoa pole ya watu wote waliokufa kwa corona, haishangazi kutokufanya hivyo. Nchi zote duniani zimeweka record za watu wote waliokufa kwa corona na zinaazimisha siku walau ya kuwakumbuka, pia wanawashukuru sekta ya afya kwetu tunajifanya wajinga.
Tumeambiwa mambo yatayoendelea ni yaleyale. Tunalo!
 
Inasikitisha sana. Hapo wanaogopa na wanaoneana aibu kuwajibishana. Ila ujinga wetu Watanzania unatugharimu sana.
 
Ndio tatizo la kukimbilia Kila mikusanyiko!
Unaweza ukajiingiza kwenye matatizo ambayo Wala huklengwa wewe!
Inanikumbisha nikiwa mdogo ...wakati Ulokole na maombi ndio habari Mpya Mjini!
Kuna muhibiri alikuwa anatoa mapepo..jioni hivi giza limeingia!
Kunaa pepo likab anwa limtoke mtu...baada ya kuzidiwa lile pepo likasema nakubali kutoka lakini usiku huu huu niende wapi!???🤭🤭
...namuingia mtu yupo hapahapa!!😆😆
Kilichotokea pale hata angekuwepo Filbert Bayi au Gidmas Shahanga wangejiona cha mtoto...
 
Kuna tofauti kati ya mtu na binadamu. Wale wa Dar ni watu na yule wa Chato ni binadamu, na kiongozi mkuu ajaye wa Malaika...

Wa Dar ni marehemu, Wa Chato ni hayati...
Point blank, kuna tofauti kati ya hayati na marehemu.

Kama kufa toka msiba Dar wamekufa wengi sio tu uwanjani hata kwenye hospitalization na pressure za ghafla. Ni jambo ambalo tuliritarajia katika mshonano ule
 
Back
Top Bottom