Serikali wafuatilie huduma za mitandao nyingi ni utapeli

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,136
4,474
Kipindi cha nyuma kidogo nilijiunga huduma yao ya halo quiz mtandao wa halotel bila kuijui vizuri baada ya muda mrefu jan nikaweka salio ili nijiunge kifurushi natumiwa sms salio limekatwa basi nikaona hii huduma ngoj nijitoe

Sasa kilichonileta hapa mpaka naandika uzi huu jana niliingia menu ya hiyo huduma nikasibitisha kujitoa kilichonichosha leo tena nimeweka salio natumiwa sms tena nimekatwa kwenye huduma ambayo nilishajitoa nikabaki nashangaa
Nimepiga simu huduma kwa wateja naambiwa pesa haiwezi rudishwa

Naambiwa nitume neno OFF kwenda 15604 kitu ambacho nilikuwa sikijui kabisa hapa ndio nimekuja kushtuka kama hii huduma ni ya utapeli

Nachoshauri serikali kupitia wizara husika wapitie huduma Mana nyingi zinaonekana zimewekwa kwa lengo la utapeli Kama kampuni watakuwa wanakata Tsh 100 kwa watu mil 1 basi watakuwa wanavuna pesa nyingi kwa njia ya utapeli
 
Back
Top Bottom