Serikali Tatu: Ni mfano wa kutoka nchi gani duniani?

- Tumefuata mfano wa USA wa Serikali mbili tu!

Le Mutuz

Sometimes CCM ni watu wa ajabu sana! Ulichoandika hapa ni kituko. Iko hivi, kwanza US wanafuata mfumo wa majimbo ambapo kila jimbo lina mamlaka fulani ya kiutawala na kujiendeshea mambo yake ikiwa ni pamoja na sheria zake. Do you mean huu Muungano tulio nao ni wa majimbo? Kama ndivyo, hebu nitajie majimbo yanaoyounda muungano wa Tz.

Kule US Jimbo huongozwa na Gavana, kwa mfumo wa majimbo unaodai upo Tz, wakuu wa majimbo ni akina nani? Huchaguliwa na kusimikwaje?

Mkuu kama huna uelewa na kitu au hoja ni vyema kunyamaza kuliko kuropoka. Kwa hoja yako hii hata CCM wenzeo wakikusikia watakushangaa maana badala ya kujenga hoja ya maana unazidi kuwaharibia. No wonder ndio maana wanakupiga chini kwenye issues mbalimbali kama uwezo wako wa hoja ndio kama hivi.
 
Sometimes CCM ni watu wa ajabu sana! Ulichoandika hapa ni kituko. Iko hivi, kwanza US wanafuata mfumo wa majimbo ambapo kila jimbo lina mamlaka fulani ya kiutawala na kujiendeshea mambo yake ikiwa ni pamoja na sheria zake. Do you mean huu Muungano tulio nao ni wa majimbo? Kama ndivyo, hebu nitajie majimbo yanaoyounda muungano wa Tz.

Kule US Jimbo huongozwa na Gavana, kwa mfumo wa majimbo unaodai upo Tz, wakuu wa majimbo ni akina nani? Huchaguliwa na kusimikwaje?

Mkuu kama huna uelewa na kitu au hoja ni vyema kunyamaza kuliko kuropoka. Kwa hoja yako hii hata CCM wenzeo wakikusikia watakushangaa maana badala ya kujenga hoja ya maana unazidi kuwaharibia. No wonder ndio maana wanakupiga chini kwenye issues mbalimbali kama uwezo wako wa hoja ndio kama hivi.

Very well said
 
- Lincoln aliua wananchi wengi ili kuwa na Serikali mbili wazlionazo sasa! kama Gowon alivyoua Nigeria.

Le Mutuz

Hujaelewa swali.

Serikali ipi imeuawa Marekani kama sisi tulivyoua serikali ya Tanganyika?

Unasema "serikali mbili walizo nazo sasa" ni serikali gani hizo? Unaweza kuzitaja?
 
- Serikali za mikoa za USA zina madaraka makubwa sana ya kujiongoza ila mikoa yetu haina ndio maana nimeshauri tuirudie ile dhana ya Madaraka Mikoani ya Mwalimu maana ni na madhumuni yake ilikuwa kuipa nguvu mikoa kama USA.

Le Mutuz

Mkuu hebu rudi kwenye reli! Muungano unaozungumziwa hapa ni wa Tanganyika na Zanzibar na sio mambo ya "madaraka mikoani" unless unataka kuifananisha Zanzibar na mkoa! Naona kwa mbaali unadhana ya MAJIMBO lakini unashindwa namna ya kuielezea kwa sababu "sio sera" yenu.
 
- U know siasa ni kama Sheria mara nyingi huongozwa kwa mifano zaidi, hivi ni Taifa gani Duniani lina Serikali Tatu ambalo tunaweza kulitumia kama our Role Model wa hii idea ya Serikali Tatu? Mimi nilidhani tunahitaji kuiongezea nguvu za utawala Mikoa yaani kwa kuirudia ile dhana ya Madaraka Mikoani, lakini Serikali Tatu I mean I am lost maana kama nimeisoma vizuri sana Rasimu ni kwamba Tunatakiwa kuwa na Serikali Tatu, Marais Watatu, Mabunge Matatu, Benki Kuu tatu, Sarafu za Pesa Tatu, Mawaziri Wakuu Watatu!!

- I mean, si niliwahi kusikia kwamba Kamati ya Katiba Mpya inaongozwa na ma-genius now what is this Serikali tatu thing?

Le Mutuz

Hilo la sarafu tatu sijui umelitoa wapi mkuu! Maana haliwezekani kabisa kabisa na nashanga umelitoa wapi
 
Mh! Huyu jamaa kweli sio mzima. Mkuu Kiranga katoa hoja yake hivi:

By Kiranga

USA ina serikali mbili? Imeua serikali gani kama sisi tulivyoua Tanganyika?

Le Mutuz anajibu hivi:

- Lincoln aliua wananchi wengi ili kuwa na Serikali mbili wazlionazo sasa! kama Gowon alivyoua Nigeria.

Le Mutuz

Duh! Hii thread sichangii tena; kumbe imeanzishwa na "hamnazo". Mchana mwema wakuu.
 
William, muundo uliopendekezwa ni shirikisho ambalo kwa mazingira yetu utakuwa Na serikali tatu yaani serikali ya shirikisho Na serikali za washirika wawili. Mifano ya muundo wa shirikisho ni mingi. Baadhi ni Marekani, ujerumani, uswisi, kanada, afrika Kusini, Nigeria n.k

Haya ni mojawapo ya majibu sahihi aliyotakiwa kupewa bw. malecela. Mengine nayo yana aslimia fulani ya ukweli japokuwa yanatakiwa kufanyiwa mchujo. yana asilimia kubwa ya kebehi na chuki dhidi ya waanzilishi wa muungano hasa Nyerere. ni kweli muungano uliopo unazo kero zake lakini si kweli vile vile kwamba serikali tatu ndiyo suluhisho pekee. pengine bw. malecela alitaka tumpe mfano wa nchi yoyote yenye serikali tatu ( kwa sababu serikali mbili tayari tunazo na haihitaji kutafuta nyingine ya mfano) ili tufanye ulinganifu na hizi mbili tulizonazo kwa kero na faida zake na kisha baadaye tufanye uamuzi ulio sahihi kidogo. kilichofuata hapo ni ku-attack personality yake, not fair wakuu.

Bw. malecela ni mtu mzima, si lazima kila analofikiria liwe ni lile lililowahi kufikiriwa na mzazi wake.
 
Serikali tatu sawa, lakini Marais watatu, jamani, huu ni UPUUZI!
 
Nikweli mara nyingi huakisi katika taifa fulani na kutenda yetu,

Lakini kabla hujaenda mbali, nikuulize, Je kule ulikokulia USA hukuona kuwa wanatumia mfumo huo?


Je ni muungano gani duniani wenye kufanana na huu wetu wa leo? Yani wa nchi mbili Huru TANGANYIKA na ZANZIBAR zikaungana, katika muungano huo nchi moja IKAFA (Tanganyika) na nyingine ikabakia HAI/huru (Zanzibar) wakati huo muungano ukaendelea kuwepo kwa jina tulilokubaliana TANZANIA

Sio lazima tunachokifanya au kukusudia kufanya kiwe kipo/kiliwahi kuwepo duniani

Kwanini sisi tusiwe waanzilishi wa jambo hilo na wengine wakaiga toka kwetu?

Labda nikujuze mkuu,

Kwamjibu wa katiba ya ZANZIBAR ya 2011, Muungando umeshavunjwa, kilichobaki ni UDUGU tu, isome katiba hiyo ibara ya kwanza tu na vifungu vyake vyote kisha rejea kwenye tafasiri hai,

Serikali Tatu ni tiba ya kuondoa malumbano ya Muungano huu,

Tanganyika yetu ipo wapi? Zipi sababu za kufa Tanganyika ndani ya muungano huu ilihali Zanzibar ikawa hai/huru?

Nitarudi baadaye kama Le Mutuz atajibu hoja hizi makini. Kwa sasa niseme tu kuwa tatiozo ndugu zetu wanachama na washabiki wa ccm akiwemo Le Mutuz ni kuwa wanaona maslahi ya chama zaidi kuliko maslahi ya Taifa. Ukifuatilia kinachoendelea kwenye mabaraza ya katiba sasa hivi utaona wajumbe wengi wa ccm (kama sio wote) wanatetea msimamo wa chama na sio matakwa ya wananchi.
 
hata hizo sheria unazosema zinaongozwa kwa mifano hazikuibuka zote kwa pamoja kuna zilizoanza nanyingine zikaanza ku refer kwa zilizotangulia. Hivyo sio lazima Tanzania tuwe watu wa kuchukuwa mifano kwingine tunaweza tukaanza sisi na tukawa role model kwa wengine watakaopendezwa na mfumo wetu. Tusijishushe kiasi hicho kwamba sisi hatuwezi kuanzisha kitu mpaka tuwe tunaiga kwa wengine.
 
kwa sasa ni serikali tatu ndio tutaweza ondoa haya matatizo ya kila upande fotauti na hapo Muungano usiwepo kabisa,Tanganyika lazima irudi kuwa dola sawia na Znz,Suala la usalama ni kujipanga hasa kijasusi then mambo mengine yatafuata,
Hatuwezi lazimisha ndoa wakati Znz wanataka nchi yao,
 
- Rekebisha kauli yako USA kuna Serikali mbili tu Federal na State ila kuna madaraka mikoani, yaani State zina nguvu kubwa sana za kujitawala!

Le Mutuz

Mkuu pole sana,

Wahenga wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi, lakini wewe nadhani ulipitwa kuona mengi!

USA ina serikali 53

(1) Serikali KUU

(2) Na 52 ni Serikali za majimbo

Kila jibo lina utawala wake wa ndani,

Mfano: Jimbo la California haliendani kiutawala na jimbo la Chicago

Jambo lingine muhimu nikuwa rasmu ya katiba haijasema tutakuwa na marais watatu, hivyo usilaghai watu hapa!

Rasimu imependekeza tuwe na SERIKALI tatu,

Kasome upya mkuu!
 
Mkuu yericko nyerere jibu lako liko sahihi sana. Naomba nisiongeze chochote nisije chachua maelezo/jibu lako kwa mtoa hoja.
 
Mkuu pole sana,

Wahenga wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi, lakini wewe nadhani ulipitwa kuona mengi!

USA ina serikali 53

(1) Serikali KUU

(2) Na 52 ni Serikali za majimbo

Kila jibo lina utawala wake wa ndani,

Mfano: Jimbo la California haliendani kiutawala na jimbo la Chicago

Kasome upya mkuu!

- Chicago na California ni Mikoa iliyopo chini ya Federal Government inayoongozwa na Rais mmoja tu anaitwa Barack Obama, USA haina marais watatu, wala sarafu tatu, au benki kuu tatu kama Rasimu inavyotaka!!

- USA ina State 52 tu ambazo zipo chini ya Rais mmoja Obama, sio marais watatu na wala hawana mabunge matatu!

Le Mutuz
 
Umejibu kwa hoja mpaka naona raha. Mifano ni mingi. USA na UK pia. Unakuwaje na Tisa Desemba bila Tanganyika? Unakuwaje na Tanz na Zenj bila Tanganyika? Serikali tatu ni suluhu.

Sijaona alichojibu, nnachokiona na yeye kauliza. naona na wewe umeendeleza maswali.

Mitanzania ndivyo ilivyo.
 
- Serikali za mikoa za USA zina madaraka makubwa sana ya kujiongoza ila mikoa yetu haina ndio maana nimeshauri tuirudie ile dhana ya Madaraka Mikoani ya Mwalimu maana ni na madhumuni yake ilikuwa kuipa nguvu mikoa kama USA.

Le Mutuz

Mkuu nadhani hapa unakwepa swali ama kwa makusudi au kutokujua, unazungumzia mikoa wakati hapa tunazungumzia zilizokuwa nchi kamili
Sidhani hapa kama unataka mfano wa kopi na kupesti hapa tunaangalia zaidi ''the logic behind''

USA kabla walikua na serikali takribani 50 na wakaunda muungano kwa kutengeneza serikali kuu na serikali ndogo 50 zikiwa kama states, na hizi states zina malaka yake makubwa tu ingawa zinafanya kazi chini ya serikali kuu
Kimantiki inamaanisha waliamua kuungana kwa kila nchi kuwa state yenye mamlaka halafu wakaunda serikali kuu ambayo itasimamia hizi states
Hii ni sawa na kusema USA kuna viserikali vidogo 52 na serikali kuu moja, sasa kama USA zingeungana let say states 2 inamaana kungekuwa na serikali ndogo 2 na moja kuu, hivi ndivyo tunataka iwe
Usichanganyikiwe sana na majina kama huku tukiita serikali wao wakiita states, huku tukiita rais wa zanzibar wao wakiita gavana nk, angalia logic

The logic behind this ni kwamba nchi zote zilizomo kwenye muungano ziwe na mamlaka yake fulani kama ilivyo USA na kwa hapa kwetu tunataka Tanganyika na Zanzibar ziwe na mamlaka fulani(kama iliyonayo Zanziba) halafu kutakuwa na serikali kuu ya muungano

Angalau nimejaribu kueleza kwanini tunasema serikali tatu ni sawa na USA
Sasa hebu fafanua kama msomi kwanini unalinganisha serikali zetu mbili zilizo zika moja zikawa sawa na hizo serikali mbili za USA unazotuambia hapa
 
- Chicago na California ni Mikoa iliyopo chini ya Federal Government inayoongozwa na Rais mmoja tu anaitwa Barack Obama, USA haina marais watatu, wala sarafu tatu, au benki kuu tatu kama Rasimu inavyotaka!!

- USA ina State 52 tu ambazo zipo chini ya Rais mmoja Obama, sio marais watatu na wala hawana mabunge matatu!

Le Mutuz
Mkuu naona unanichosha tu,

Ili tuweze kujadiliana kwa hoja naomba kufahamu, umeisoma rasimu ya katiba kwa utuvu kabisa?

Niambie kipengele kinachosema "tutakuwa na marais watatu"

Nitajie pia kipengele kinachosema "kutakuwa na sarafu tatu"

Ili twende sawa!

Kama hata USA hujui kuwa majimbo yanaserikali zao tena zinatofautia kila jimbo, siamini kama utaelewa kilichomo katika rasimu mpya!
 
Back
Top Bottom