Serikali tatu, CCM hoi mpaka UN


kwa mara ya kwanza nasoma maneno mazima yenye logic kutoka kwako. Tafadhali usirejee tena ulikokuwa ni kubaya mno, kunakupotezea haiba na hshima yako mbele ya umma wa JF
 
Kibo10 una uhakika na unachokiandika au ni ushabiki wa Kibo na Mawenzi mivyojazana ujinga?
Km Gazeti la Tanzania Daima limeandika siwezi kubisha kwani ni la kishabiki na linajulikana

ingia kwenye Library ya UN yA Katibu Mkuu Dag-Hammars (RIP) aliyepokea makubalianao hayo ya Tanganyika na Zanzibar
UN|DPI â€" OD|Dag Hammarskjöld Library: Member States|On the Record

Kibo10 hivyo naomba kila mmoja wetu akumbuke kwamba, hati yetu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni UDONGO aliouchanganya Mwalimu Nyerere Tarehe 26/04/1964.
Naona UMANGI na uCHADEMA unakusumbua kwani ulizaliwa na kuja kuhadithiwa tu kuwa walichanganua UDONGO kwanini usitumie hata search engine vitu hivi viko wazi

Huo nao ni UDONGO?
MY TAKE
mm ni muumini w Serikali 3 na ninakubaliana kabisa hata ikiwezekana Zanzibar tuwaachie visiwa vyao (Unguja na Pemba) kwani huwezi mng'ang'ania Mke asiyekutaka anayekutolea Kashfa
kwani wenzetu wana uhakika hiyo Hati ilikuwa ni ya miaka 10 tu na kule haiko au imegushiwa siwaelewi ila ushahidi halali tumeandikishwa lakini kusema hata UN hakuna ushahidi wa huo Mungano!!! mm nakataa kabisa

Hati halali ya Muungano ni wa kipindi cha miaka 10 tu na hio haiko UN. - Mzalendo.net
Hati halali ya Muungano ni wa kipindi cha miaka 10 tu na hio haiko UN.
Attached Files
 
upo sahihi mkuu.

Karume alikubali muungano kwa kuwa lilikuwa sharti la Nyerere ili apewe nchi ya Zanzibar kwani mganda ndo alieongoza mapinduzi wakati Karume alikuwa anakula urojo mchambawima

Duh! Ni mataptapu au bange?
Ungekuwa karibu ningekunusa mdomo!
 
kwa mara ya kwanza nasoma maneno mazima yenye logic kutoka kwako. Tafadhali usirejee tena ulikokuwa ni kubaya mno, kunakupotezea haiba na hshima yako mbele ya umma wa JF

Huwa hunisomi tu.
 
Fix
Usiwe kigeugeu.Tunajua ww ni muumini wa CCM na mpiga debe wa Sirikali 2!Mbona wapingana na chama chako?
Tunaposema Serikali 3 ndio mwafaka lazima mkubali kuwa Muungano tulionao wa 2 ni kiini macho tu!

Tatizo huwa hamnisomi, rejea haya:

 


Uzuri wa nchi wa kwanza kabisa ni kuwa huru na kuweza kuyajadili kwa uwazi bila vitisho yale uyatakayo. Kamaufanyavyo leo hii. Thubutu wakati wa Nyerere uyaulize ya Serikali tatu, waulize G55 kwanini waliufyata? muulize Jumbe nini kilichomyoa manyoya na akabaki ana baridi na yuko nyumbani mpaka leo? ruksa yake ni kwenda hospitali na kurudi au kwenda Makkah kufanya ibada na kurudi, ushamuona mahala wewe? jiulize kwanini?

Blind Faith? Msome ludovick Kaijage kilichomkuta alipohoji ya Nyerere. Kambona uliwahikusikia? aliishia wapi alipohoji ya Nyerere? Kassim Hanga aliadhiriwa na Nyerere kwenye halaiki ya watu mnazi mmoja kisha akapotezwa mpaka leo hii, unajuwa kilicho kuta? huyo ndio Nyerere. Kaiharibu nchi vibaya sana.

Leo kuna neema tunaweza kuhoji serikali mbili, tatu, moja. Huru kabisa, hayo ndiyo maendeleo.
 
Faiza tunaomba msimamo wako kuhusu muungano. Mbili au tatu au usiwepo kabisa?

Nilishajibu hivi:

By FaizaFoxy

Sikiliza nikueleze, ni miaka mingi sana mimi napingana na fikra za Nyerere, rejea posts zangu za zamani humu JF au waulize waliopo zamani humu wanajuwa msimamo wangu.

Mimi Serikali mbili hazinipi shida, lakini ziwe mbili za ukweli ya Tanganyika na ya Zanzibar na maridhiano aka Mkataba.

Serikali tatu hazinipi shida ila naona ni ujinga usio na mfano, ziwe tatu basi hii ya Tanzania isiwe na executives powers ambayo tunarudi pale pale kwenye mbili na mkataba.

Au Muungano ufe kabisa kila mmoja kivyake. Kwangu ni vyema zaidi.
 

Kwahio alivyoharibu nchi (upande wa uhuru wa mtu) alivyoondoka nchi ndio imepona, au sasa hivi ndio nchi ipo safi haina matatizo ? au ni mzimu wake ndio unaharibu nchi ? au uharibifu wake ni beyond repair ?, kwahio kama yeye ndio aliharibu does it mean ilikuwa bora wakati wa ukoloni (watu walikuwa huru)?
 

Siku ukiwa hauna matatizo duniani ujuwe umesha kufa.

Leo unaweza kuongea matatizo yako bila bughudha, uliweza kuongea matatizo yako ya kiutawala wakati wa Nyerere?

Ulikuwepo wakati wa utawala wa Nyerere au unamsikia tu?
 
Siku ukiwa hauna matatizo duniani ujuwe umesha kufa.

Leo unaweza kuongea matatizo yako bila bughudha, uliweza kuongea matatizo yako ya kiutawala wakati wa Nyerere?

Ulikuwepo wakati wa utawala wa Nyerere au unamsikia tu?
Kwahio hakuharibu nchi zaidi alivyoikuta (uhuru kama unavyosema) na alivyoondoka na sasa amekufa (sio kwamba ameacha mizimu inayomfanyia kazi...), kwahio ni uharibufu gani huo ambao hauponi au watu hawautibu alioufanya Nyerere.., That's why I said kuanza kulaumu watu waliokufa kwa kinachoendelea sasa..... ni tabia ambayo hata msamiati wake haupo kwenye Kiswahili its beyond ridiculous
 
Nyerere hakuwa malaika, he did his best and he tried his best kwaajili ya manufaa ya wananchi wake. Kama kuna mahala alipokosea kujenga, tukae chini kuziba ufa, sio kupiga domo mpaka jumba hilo litudondokee...
Napita tu...
 
Nani kakwambia tunaenzi fikra ZOTE za Nyerere ? Nyerere ni binadamu na kuna makosa aliyoyafanya na mojawapo kwa mujibu wangu ni siasa za kijamaa na lingine ni kuweka muundo wa serikali mbili na kuna mengine ambayo watu wengine wanaweza kuyaona. Sasa kuna ubaya gani kurekebisha kosa alilolifanya, unapopata nafasi ya kufanya hivyo ?

Kama nilivyosema hapo juu, hatuenzi fikra zote za Nyerere ila tunaenzi fikra nyingi za Nyerere kwani alikuwa na fikra nzuri kwamba mambo mengi tu, lakini kwa yale aliyokosea kama hilo la muundo wa muungano, hatuenzi fikra zake !

Watanzania wengi wanaamini Nyerere alifanya mambo mengi mazuri sana kwa Tz. Hiyo haina maana kwamba hakufanya makosa !.

Hapo kwenye rangi nyekundu, umejidhalilisha tu ! Hivi kweli ulitegemea useme, hakuna lolote jema alilolifanya Nyerere alafu upate support ? Uelewa wako utakuwa wa chini sana kama ulitegemea kupata support kwa maneno kama hayo !

 


Ujamaa na sasa Muungano na pia kuiuwa Tanganyika si ndiyo?. Hayo ndiyo makosa uyaonayo ya Nyerere, Swadakta, hapo upo pamoja na mimi. Unaniunga mkono kwa kupinga fikra za Nyerere na nnafarijika sana kwa hilo

Nakuuliza na uchumi jee, unakubaliana nae kuitoa Tanganyika kutoka wasafirishaji wa kwanza wa mazao ya kilimo katika Afrika wakati anakabidhiwa Uhuru mpaka kufikia omba-omba wa chakula kwa miaka 7 tu. Vipi hapo napo?

Sasa unachotakiwa uanze kampeni ya kuwa tusikubali fikra ya Nyerere kuhusu muungano, aliiuwa Tanganyika na tunaitaka Tanganyika yetu amma tuipate amma muungano basi. Unaonaje hapo? upo tayari au una fikra zako zingine?
 
Kuhusu uchumi mwalimu alijitahidi kuweka msingi wa kujitegemea kama taifa..uzalendo na uaminifu ulikuwepo pamoja na dira..sasa tujiulize msingi wetu ni nini...uzalendo unadorora pia uaminifu unakua bidhaa adimu aidha tunahitaji dira/katiba ya wananchi kutukwamua hapa tulipo laa sii hivyo jahazi litaenda mrama
 
Kukosekana maendeleo ya wengi ndio kunafanya tuanze kujibishana serikali 2 mara 3...
 
sisi wazanzibari tulimaliza mchakato. Tulikwisha kwenda UN miaka iliopita na tunajuwa kila kitu. Tulipeleka signature 100000 za waznzibari UN kudai nchi yetu. Tuna kesi juu ya muungano katika kesi ya kimataifa. Tunasubiri tu. Haya yote wanayosema kina Nahoda na ma CCM wenzake, wanajidanganya bure sdabau huko wanako taka kutupeleka sisi tusharudi. Mwisho Dr. Shein alisema karatasi ziko ikulu zanzibar.wazanzibari wanamuangalia tu na ujuha wake.Huu muungano haona "documents" zozote kutokz upande wapili wa muungano na la mwisho pia baraza la mapinduzi halikukaa kuidhinisha muungano. Leo, jamaa zangu wameahidi kuleta hizi "documents" watakapo rudi kwenye kikao. Sisi tunawaangalia tu na hashuo lao. Jamani hatuna muungano tulilo nalo ni USANIII nchi kubwa kuiburuza nchi ndogo. Ukweli hausemwi. Muungano au mkataba ulikuwa wa miaka kumi ndio maana Karume aliuawa kabla ya kutimiza miaka kumi. Kazi tumemwachia Mh. Sitta na ujuaji wake na vibaraka wa CCM. Ushahidi haupo ila ni masumbuko na wizi.
 
Watuambie huo udongo uko wapi
 
Muungano wa kweli ni kuwa na Serikali moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nchi washirika 2 zenye Waziri Mkuu wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Tanganyika. Bendera moja na wimbo wa Taifa mmoja tu. Asanteni.
 
Tatizo la nchi yetu ni moja tu. Kuna kundi la watu wachache wenye fikra za kidhalimu wanadhani nchi hii ni mali yao na wana hati milki ya kufanya chochote wanachotaka kwa manufaa yao binafsi. Nchi hii ni mali ya Watanzania, maamuzi makubwa kama ya KATIBA MPYA yataamuliwa na Watanzania wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…