msemakweli
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 1,627
- 880
SERIKALI imesema Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shy-Rose Bhanji hajapigana nchini Kenya, na wanasubiri Tume ya EALA ili kujua ukweli wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.
Kwa muda sasa, Shy-Rose amekuwa katika mzozo na wabunge wenzake wa EALA, kwanza akituhumiwa kuwatukana wakiwa safarini Ubelgiji na juzi akituhumiwa kupigana na mwenzake kutoka Tanzania, Dk Nderakindo Kessy.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta awali alilieleza Bunge jana mjini hapa kuwa kiini cha mzozo wote ni mgogoro dhidi ya Spika wa EALA, Margaret Zziwa wa Uganda.
Sitta alisema yapo makundi mawili sasa ndani ya Bunge hilo, moja likitaka kumng'oa Spika huyo na lingine likimkingia kifua kwamba hapaswi kuondolewa.
"Katika hili (la kumng'oa Spika), Tanzania ni kikwazo, kwa sababu ili Spika aondolewe ni lazima akidi itimie, na akidi hiyo ni kupata kuungwa mkono kwa idadi fulani ya wajumbe wa kila nchi. "Sasa Tanzania wamefuta hoja ya kutaka Spika huyo aondolewe na hii ndiyo imesababisha chuki yote," alieleza Sitta kabla ya kujibu hoja kuhusu Shy-Rose.
Sitta alisema Shy-Rose hakupigana au kumpiga mbunge mwenzake kama ilivyoandikwa katika magazeti jana.
Chanzo:Nipashe

![]()
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy
Serikali imetoa kauli bungeni, ikisema Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shyrose Bhanji, hakumpiga Mbunge mwenzake Nderakindo Kessy (pichani), bali Bunge hilo lina mgogoro ambao, kiini chake ni Spika wa Bunge hilo,Magreth Zziwa.
Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akitoa taarifa bungeni baada ya Khatib Said Haji (Konde-CUF), kuomba mwongozo wa Spika, kuhusu kinachoendelea kwenye Bunge hilo.
Sitta alisema: "Kinachotokea katika AELA kwa kiasi kikubwa kinahusu mgogoro wa Spika mwenyewe, ndiye chanzo cha matatizo mengi ambayo yamegawa bunge hilo katika makundi makuu mawili."
Alitaja makundi hayo kuwa ni linalotaka spika huyo aondolewe kwa madai kwamba hafai, huku lingine likimtetea abaki.
Alisema Tanzania inaonekana kuwa kikwazo katika mkakati wa kumuondoa Zziwa.
Alisema ili Bunge hilo liamue jambo lolote, lazima akidi ipatikane katika kila nchi na kwamba awali Tanzania waliunga mkono aondolewe, lakini sasa, wamekuwa na msimamo tofauti na kusababisha kuwapo aina fulani ya chuki.
"Kilichotokea kati ya Bhanji na Kessy, siyo kinavyoelezwa kwani Bhanji anahesabika kuwa ni shabiki mkubwa wa Spika, kiasi cha wenzake kumuona kama kibaraka vile," alieleza Sitta.
Alielezea kuwa madai ya Kessy kupigwa yalitokana na Bhanji kugongana naye kwa bahati mbaya wakati akiwahi usafiri, akipita katikati ya wabunge wenzake,Alisema mgongano huo ulitafsiriwa na Kessy kuwa ni shambulio, ambaye alihamaki na kwa kusaidiwa na baadhi ya Wabunge wa Uganda, akaenda polisi na kumtuhumu Bhanji kwamba amemtendea kosa la jinai.
Alisema hata hivyo, kwa jitihada za uongozi wa EALA, mpaka jana suala hilo halimo mikononi mwa polisi tena bali limemalizwa ndani ya Bunge.
Sitta alizungumzia madai mengine dhidi ya Shyrose kwamba alifanya mambo ya ‘ovyo' takriban miezi miwili iliyopita kwamba bado yapo mikononi mwa Tume ya EALA, itakapomaliza kulishughulikia litatolewa taarifa.
"Kwa sasa hatuwezi kufanya lolote, mpaka tutakapopata taarifa kutoka EALA, nikizipata nitaziwasilisha kwa Spika wetu na hapo ndipo sisi kama jimbo la uchaguzi tutakapojadili kuona ukweli ni upi na kuamua hatua za kuchukua," alieleza Sitta.
Chanzo:Nipashe