Serikali/NECTA iangalie hili

mwitasa

Senior Member
Dec 28, 2013
199
476
Kwa nini hakuna Combination ya ECA kwenye special school za shule za wasichana?. Kwa kweli inakera na inakatisha tamaa kwa wanafunzi na wazazi. mtoto kapata div.1.7 akiwa na AAA kwenye hesabu Commerce na bookkeeping kapelekwa shule za kawaida wakati wenzake kwenye michepuo tofauti na point za chini wamepelekwa Special school hii si haki.

Mtoto tangu akiwa darasa la saba alikuwa na ndoto za kusoma special school lakini form one hakuchaguliwa huko nikampa moyo afanye bidii form apate A zote ili achaguliwe kwenda special school na katimiza hilo na alikuwa na ndoto ya kusomea masomo ya ECA ila sasa amepelekwa shule ya kawaida. Tumeangalia matokeo ya shule hiyo kwa miaka 4 nyuma hakuna mwanamfunzi aliyewahi kupata division 1 hata ya mwisho wala kupata alama B ya somo lolote kwenye mchepuo huo. Mtoto kakataa tamaa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano ECA na mzazi hana uwezo wa kumpeleka Private amesusa hataki shule bora awe mjasiriamali . Ameshauriwa kagoma inaumiza kichwa
 
ila acha tu kuishi ndani ya ndoto kazi sana kuna watoto ninao wanaziota hizo special yani basi tu wakizikosa wanaumiaga
 
Kwa nini hakuna Combination ya ECA kwenye special school za shule za wasichana?. Kwa kweli inakera na inakatisha tamaa kwa wanafunzi na wazazi. mtoto kapata div.1.7 akiwa na AAA kwenye hesabu Commerce na bookkeeping kapelekwa shule za kawaida wakati wenzake kwenye michepuo tofauti na point za chini wamepelekwa Special school hii si haki.

Mtoto tangu akiwa darasa la saba alikuwa na ndoto za kusoma special school lakini form one hakuchaguliwa huko nikampa moyo afanye bidii form apate A zote ili achaguliwe kwenda special school na katimiza hilo na alikuwa na ndoto ya kusomea masomo ya ECA ila sasa amepelekwa shule ya kawaida. Tumeangalia matokeo ya shule hiyo kwa miaka 4 nyuma hakuna mwanamfunzi aliyewahi kupata division 1 hata ya mwisho wala kupata alama B ya somo lolote kwenye mchepuo huo. Mtoto kakataa tamaa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano ECA na mzazi hana uwezo wa kumpeleka Private amesusa hataki shule bora awe mjasiriamali . Ameshauriwa kagoma inaumiza kichwa
Mwelekeze aelewe, mwambie kukosa special school sio mwisho wa ndoto zake, Mungu muda mwingine ndo anapanga maisha ya mtu yaweje, mueleweshe na ukae naye. Yeye ni mtoto haelewi vizuri haya mambo. Mwisho wa siku yeye na marafiki zake watakutana UDSM.
 
Mwite mawanao na umweleze kwa upole. Kwamba. 'Mwanangu, mtu mwenye kiu ya mafanikio, anandoto moja tu, MOJA TU, ya kupigania. Zikishakuwa mbili, lazima ujipotee'.

Huwezi kuwa na ndoto ya kusoma ECA, hapo hapo uwe na ndoto ya kusoma special school. Inamaana moja kati ya hizo ndoto ukiikosa, tayari, unakata tamaa kama yaliyomkuta huyo binti yako.

Laiti kama angekuwa na ndoto moja tu ya kusoma ECA, no matter anaisomea shule gani, ange soma na angetoboa hata kama ni kwenye shule inayotoaga zero tuu kila mwaka. Hujawahi ona kwenye shule dogo ana one peke yake halafu wengine wote wana four na zero?

Ama la, kama ndoto yake ilikuwa special school angefukuzia hizo combination zingine za huko special school akatimize ndoto yake. Lakini kubeba ndoto zote mbili obviously utakwama tu. Kufanikiwa uwa ni marachache sana. This is a general life lesson.

'Ni vigumu kuubadili mfumo uendane na wewe, ni wewe ndiye unatakiwa kubadilika uendane na mfumo' Mwambie hivo. Other wise kususa haijawahi kuwa njia ya kutatua tatizo😌
 
Mwite mawanao na umweleze kwa upole. Kwamba. 'Mwanangu, mtu mwenye kiu ya mafanikio, anandoto moja tu, MOJA TU, ya kupigania. Zikishakuwa mbili, lazima ujipotee'.

Huwezi kuwa na ndoto ya kusoma ECA, hapo hapo uwe na ndoto ya kusoma special school. Inamaana moja kati ya hizo ndoto ukiikosa, tayari, unakata tamaa kama yaliyomkuta huyo binti yako.

Laiti kama angekuwa na ndoto moja tu ya kusoma ECA, no matter anaisomea shule gani, ange soma na angetoboa hata kama ni kwenye shule inayotoaga zero tuu kila mwaka. Hujawahi ona kwenye shule dogo ana one peke yake halafu wengine wote wana four na zero?

Ama la, kama ndoto yake ilikuwa special school angefukuzia hizo combination zingine za huko special school akatimize ndoto yake. Lakini kubeba ndoto zote mbili obviously utakwama tu. Kufanikiwa uwa ni marachache sana. This is a general life lesson.

'Ni vigumu kuubadili mfumo uendane na wewe, ni wewe ndiye unatakiwa kubadilika uendane na mfumo' Mwambie hivo. Other wise kususa haijawahi kuwa njia ya kutatua tatizo
Asante kwa ushauri mkuu ngoja niendelee kumshauri maana alisusa siku 2 bila kula analia tu. Nadhani na utoto bado unachangia
 
Mwelekeze aelewe, mwambie kukosa special school sio mwisho wa ndoto zake, Mungu muda mwingine ndo anapanga maisha ya mtu yaweje, mueleweshe na ukae naye. Yeye ni mtoto haelewi vizuri haya mambo. Mwisho wa siku yeye na marafiki zake watakutana UDSM.
Pouwa mkuu
 
Mwite mawanao na umweleze kwa upole. Kwamba. 'Mwanangu, mtu mwenye kiu ya mafanikio, anandoto moja tu, MOJA TU, ya kupigania. Zikishakuwa mbili, lazima ujipotee'.

Huwezi kuwa na ndoto ya kusoma ECA, hapo hapo uwe na ndoto ya kusoma special school. Inamaana moja kati ya hizo ndoto ukiikosa, tayari, unakata tamaa kama yaliyomkuta huyo binti yako.

Laiti kama angekuwa na ndoto moja tu ya kusoma ECA, no matter anaisomea shule gani, ange soma na angetoboa hata kama ni kwenye shule inayotoaga zero tuu kila mwaka. Hujawahi ona kwenye shule dogo ana one peke yake halafu wengine wote wana four na zero?

Ama la, kama ndoto yake ilikuwa special school angefukuzia hizo combination zingine za huko special school akatimize ndoto yake. Lakini kubeba ndoto zote mbili obviously utakwama tu. Kufanikiwa uwa ni marachache sana. This is a general life lesson.

'Ni vigumu kuubadili mfumo uendane na wewe, ni wewe ndiye unatakiwa kubadilika uendane na mfumo' Mwambie hivo. Other wise kususa haijawahi kuwa njia ya kutatua tatizo
Asante kwa ushauri mkuu
 
Ni wazo zuri mkuu ngoja nimshauri pia
Ilo ndo la umuhim atatoka na diploma yake then degree itakuwa uhakika kuliko umpeleke huko atasoma kwa stress mwisho wa siku atakuja kupata zero au four advance haihitaji usome kwa stress ukisoma ivo zero hii hapa hata ka ulipata 1.7 huko o level
 
Asante kwa ushauri mkuu ngoja niendelee kumshauri maana alisusa siku 2 bila kula analia tu. Nadhani na utoto bado unachangia
😅😅😅🤣🤣hapo kwenye kulia umenikubusha. Mdogo wangu alichaguliwa shule ya kata, kipindi hicho ndo zinaanza anza. Yeye malengo yake yakiwa shule kubwa ya bweni. Alipojikuta shule ya kata akaanza kulia. Mshua akasema huu upuuzi siwezi kuuendekeza. Akaenda kugonga kamnyweso kidogo.

Akarudi usiku, akamkuta dogo kajikunyata kama anaumwa. Acha aanze kumfokea. Yaani umechaguliwa halafu unajiliza, sisi tukusaidieje. Unajikuta we ndo nani yan! Alifokewa haswa usiku ule. Mbona alinyoosha njia. Ikabidi aipende tu shule aliyochaguliwa na form four akaperform vizuri tu.

Nawewe sasa huyo binti akizidisha mideko, hebu vaa uhusika tu. Mara maana hamna namna. Siku mbili analia kwani kafiwa na mama yake mzazi huyo😠
 
Asante kwa ushauri mkuu ngoja niendelee kumshauri maana alisusa siku 2 bila kula analia tu. Nadhani na utoto bado unachangia
Mtoto wa mwisho wa bro alipata AAB PCM akapelekwa shule ya kawaida tena mpya haijamalizika hata kujengwa na ilikuwa na mwalimu wa Math peke yake Physics na Chemistry wanabebwa na lori la shule kupelekwa shule ya jirani. Hakuna cha maktaba wala nini. Lakini yeye na wenzake walipambana kwa kila hali wakapata first class nzuri tu haoo mlimani na mpaka ninapoandika yuko US na full scholarship anapiga Electrical Engineering....

Dogo asikate tamaa. Wakati mwingine Mungu Ana mipango yake!
 
Hivi bado kuna shule za vipaji maalum?! Nilidhani iliisha miaka hiyo...
 
Kumbe watu malengo yao ni kusoma special school tu
Special school kusema kweli ni shule bora sana!! Kuna ushindani mkubwa sana baina ya wanafunzi huko na hilo linawasaidia kupanda kitaaluma! Pia hakuna spoon feeding huko kama ilivyo private schools, hilo huwaandaa vizuri kwa masomo ya elimu ya juu ambako pia hakuna spoon feeding!! Ila kama mtu akikosa hiyo nafasi inabidi apatiwe ushauri nasaha na asonge mbele.
 
Back
Top Bottom