Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Sijawahi kujihusisha na habari za udaku hata siku moja na siwezi kuanza leo, labda uniambie kinachoandikwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ni udaku.

By the way Kikwete katika muda aliokaa madarakani wa miaka 10 alilipa kodi kiasi gani!? Magufuli na mshahara wake wa milioni 410 kwa mwaka tangu aingie madarakani amelipa kodi kiasi gani!?

Bro. Naumiza kichwa changu kutafakari-kwani watz walowengi wamezoea habari za udaku hata kwenye ununuzi wa magazeti pia, wanasiasa walifanya kazi kubwa sana, hasa ya kushika akili za watu na kusema uongo kuwa ukweli tokea janauri hadi desemba, kutoka kwenye hicho kufungo ni lazima ufanye maamuzi magumu bro. Leo utaambiwa fisadi na ushahidi wanao na kesho wanasema mwenye ushahidi na aende mahakamani-na unapiga makofi kwa shangwe kubwaaaaa!!!!!!!!!
 
JANGA JINGINE KWA MBOWE





Na OMARY MLEKWA-HAI

MIEZI takribani mitano tangu aondolewe Bilicanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, jana tena Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 13.5 ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame mkoani Kilimanjaro vinginevyo itafungwa.

Uamuzi huu mpya wa Serikali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analolimiliki Mbowe kutokana na kile alichosema kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.

Takribani miezi mitano iliyopita, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilivamia na kutoa vitu vyote katika jengo maarufu la Bilicanas lililopo Mtaa wa Mkwepu na Makunganya, Dar es Salaam.

Jengo hilo lililovunjwa wiki mbili zilizopita lilidaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Aikael Mbowe ambaye ni baba mzazi wa Freeman Mbowe.

Hata hivyo, NHC ilieleza kuchukua uamuzi huo kutokana na mteja wake (Mbowe) kushindwa kulipa kodi ya pango zaidi ya sh bilioni 1.172 ambayo ni malimbikizo tangu miaka ya 1990.

Ingawa Mbowe mwenyewe amepata kusema kuwa jambo hilo limefanywa kwa sababu za kisiasa, lakini alipolifikisha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, kesi yake ilifutwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.

Alisema hali hiyo imesababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.

Byakanwa alisema Serikali ya awamu ya tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbunge huyo ambaye ni mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo Kijiji cha Nshara, hajawahi kulipa kodi ya huduma licha ya kuandikiwa barua Januri 21, 2016 ya kumtaka kulipa kodi hiyo ambayo hakuijibu.

“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi.

“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.

Alisema deni hilo lilipwe ndani ya siku 14 na akishindwa atachukua hatua ikiwa ni pamoja na kufunga biashara.

“Ikiwezekana tufafunga biashara hii, kwa kuwa amekuwa na tabia ya kutokujali kama nilivyomwita ofisini kwangu na hakufika na wala kujibu barua, sasa na hili puuzeni tutachukua hatua,” alisema Byakanwa.

“Mnaweza kusema kuwa DC labda anamwonea, mimi nakwenda na vielelezo na hapa pia nina taarifa nyingine kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa hajapeleka taarifa ya mauzo ili aweze kukadiriwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Hai, David Mlay.

Gazeti hili jana lilimtafuta Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, lakini hakupatikana.

Jana hiyo hiyo MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na dada wa Mbowe aitwae Neel Mbowe, anayesimamia shamba la Veggies, ambaye alisema nyaraka na taratibu zote za umiliki wa shamba hilo anazo kaka yake huyo.

Kuhusu umiliki wa shamba hilo, Neel alisema lilikuwa likimilikiwa na babu yao tangu mwaka 1940 na baadae akampa baba yao, marehemu Aikael Mbowe.

Kwa mujibu wa Neel, walimua kulima katika eneo hilo ambalo lilikuwa pori kwa muda mrefu ili kuongeza ajira kwa vijana wanaolizunguka.

Kuhusu sheria ya mazingira na umiliki wa shamba hilo, alisema anayejua yote hayo ni kaka yake Mbowe.

Juzi Byakanwa alitoa amri ya kusitisha shughuli za kilimo katika shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara.

Byakanwa alimshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.

“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (juzi) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.

“Pia naliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hili na kuchukua hatua pamoja na kuniletea taarifa walizochukua. Maofisa maliasili wa wilaya wafanye tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14,” alikaririwa Byakanwa.

Usichanganye siasa na sheria za nchi. Mbowe anajiita ni kiongozi, anatuongoza, basi aonyeshe mufano awe kiongozi. Anatuongoza tusilipe kodi, anaotuongoza tufanye biashara kwenye majumba ya umma bila ya kulipa kodi. Hakuna anyemuonea Mbowe, ila alizowea kupiga deal, na serikali ilimufumbia macho, sasa hii serikali ni ya watu, hawezi kuwadhurumu watu ambao anawaongoza, Mbowe hafai tena hafai kuwa kiongozi. Fikiria chama chake kingeshinda, angenyakuwa kila kitu akawaacha anaowaongoza njia panda. Hafai tena hafai, alipe ama aflisiwe. We do not want selective justice, justice has to be applied to everyone. Masikini akiacha kulipa maji anakatiwa, pale pale, akiacha kulipa leseni duka linafungwa pale pale. Sheria moja kwa kila mtu, nchi hii ni yetu wote, hakuna Mtanzania bora kuzidi mwingine. Ukijenga ukuta na muchanga bila saruji, ukuta utapolomoka. Mbowe amejenga biashara zake kwa deal, sasa deal hakuna tena biashara zinaanza kupolomoka moja moja na bado, ataishi kama raia wa kawaida. Mbowe hafai kuwa kiongozi.
 
Hata Magufuli ni kiongozi pia kwanini haoni aibu kupata mshahara wa milioni 410 kwa mwaka na kutolipa kodi wakati wale wenye mishahara midogo wanalipa kodi!?

Aonyeshe mfano kwa kutokubali kulipwa mshahara mkubwa sana bila kukatwa kodi. Taifa letu linahitaji kila senti ili kuongeza mapato ya kodi.

Mshahara wa milioni 410 kwa mwaka ni sawa na 4.1 billion kwa miaka 10 halafu mtu anakwepa kulipa kodi na huku akijua fika matatizo mbali mbali ya nchi yetu. Huu ni UNDUMILAKUWILI wa hali ya juu.

Hivi na hawa Marais na Mawaziri Wakuu wastaafu wanalipa kodi katika marupurupu yao makubwa ya kila mwaka!?

Usichanganye siasa na sheria za nchi. Mbowe anajiita ni kiongozi, anatuongoza, basi aonyeshe mufano awe kiongozi. Anatuongoza tusilipe kodi, anaotuongoza tufanye biashara kwenye majumba ya umma bila ya kulipa kodi. Hakuna anyemuonea Mbowe, ila alizowea kupiga deal, na serikali ilimufumbia macho, sasa hii serikali ni ya watu, hawezi kuwadhurumu watu ambao anawaongoza, Mbowe hafai tena hafai kuwa kiongozi. Fikiria chama chake kingeshinda, angenyakuwa kila kitu akawaacha anaowaongoza njia panda. Hafai tena hafai, alipe ama aflisiwe. We do not want selective justice, just has to be applied to everyone. Masikini akiacha kulipa maji anakatiwa, pale pale, akiacha kulipa leseni duka linafungwa pale pale. Sheria moja kwa kila mtu, nchi hii ni yetu wote, hakuna Mtanzania bora kuzidi mwingine. Ukijenga ukuta na muchanga bila saruji, ukuta utapolomoka. Mbowe amejenga biashara zake kwa deal, sasa deal hakuna tena biashara zinaanza kupolomoka moja moja na bado, ataishi kama raia wa kawaida. Mbowe hafai kuwa kiongozi.
 
Tukiweka mbali mambo ya kisiasa, Mbowe anastahili kulipa kodi kama kiongozi ili kuonesha mfano kwa jamii. Pia alitakiwa kufata taratibu zote za mazingira kabla ya kuendelea na shughuli za kilimo kwenye shamba husika. Lakini naamini kama rekodi zake ziko sahii hapo ni porojo tu.


Mzee Ndesamburo mbona analipa kodi na ana biashara kibao kwani yeye sio mpinzani?
 
Hata mi nadaiwa million 1 nikalipe Kesho naenda kulipa na sipati faida

Yeye anadaiwa million 15 na billioni 1.3, na ni kiongozi, anatakiwa kuonyesha mfano. Biashara zake alikuwa akiziendesha kwa deal, sasa deal hakuna ni kulipa kodi ama kufunga, na msimutetea kusema anaonewa.
 
KIFO CHA MANYANI MITI YOTE HUTELEZA. ...KUVUNA MITI YA ASILI NI KITU CHA LAANA MBELE YA MOLA. .
 
Bro pita hapa uone undumila kuwili wa MACCM. Huyu analipa kodi kiasi gani kwa mwaka!? Rugemarila yule mwizi wa 321 billioni na washirika wenzie wanalipa kodi kiasi gani kwa mwaka!?


aziz_228.jpg


SIRI imefichuka. Kampuni ya Dowans Holdings SA inayodaiwa kusajiliwa nchini Costa Rica, haikuwa na “biashara nyingine yeyote duniani” wakati ikimpa Rostam Aziz mamlaka ya kisheria (Power of Attorney) ya kuiwakilisha nchini Tanzania.

Hii ndiyo kampuni inayodai TANESCO Sh. 94 bilioni kwa kukatisha mkataba wake wa kufua umeme ilioupata kutoka kampuni hewa ya Richmond Development (LLC).

Taarifa hizi zimepatikana katika hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Biashara (ICC) ambayo MwanaHALISI ina nakala yake.

Imefahamika kuwa hata wakati wa kumpa Rostam Aziz mamlaka ya kisheria (28 Novemba 2005) ya kusimamia biashara zake, kuingia ubia na kufanya shughuli zake nyingine, Dowans haikuwa na biashara yoyote Costa Rica au kokote duniani.

ICC inasema katika hukumu yake kuwa wakati Rostam anapewa madaraka, Dowans inayodaiwa kuwa ya Costa Rica haikuwa na shughuli zozote wala ofisi isipokuwa Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Kampuni inayotaka kulipwa mabilioni ya shilingi na serikali ya Tanzania, “…haina mali yoyote isiyohamishika, magari wala haikuwa imesajiliwa kama mlipa kodi” nchini Costa Rica imeeleza hukumu hiyo.

Aidha, Dowans hiyo haikuwa imewahi kufanya kazi nyingine yeyote, Costa Rica na, au duniani kwa jumla.

Taarifa hii inayotokana na hukumu ya ICC, inasaidia kujenga shaka juu ya uhalali wa Dowans ya Costa Rica, mamlaka ya Rostam ya kuwakilisha kampuni hiyo na uhalali wa TANESCO/serikali kulipa kiasi chote inachodaiwa.

Wakati huohuo ICC imebainisha kuwa wakati wa kusikiliza madai ya Dowans, mashahidi tisa na nyaraka karibu 3,000, zilionyesha kuwa Rostam alikuwa “mtu muhimu” katika suala lililopelekwa mahakamani.

Mashahidi waliofika mahakamani hapo, ni pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Dowans Tanzania Ltd., Guy Picard na Henry Surtees, mhandisi wa ujenzi wa kampuni ya Caspian ambaye pia ni mfanyakazi wa Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd (DTL) kwa karibu mwaka mmoja. Kampuni Caspian inamilikiwa na Rostam.

Wengine ni Stanley Munai, mhasibu aliyeajiriwa na DTL kama mdhibiti wa fedha na Johannes Lottering aliyekuwa mwajiriwa wa kampuni ya Net Group Solution ya Afrika Kusini.

Lottering, mkuu wa idara ya usambazaji umeme wa Net group Solution ndiye aliyetajwa na kampuni ya mawakili iliyotetea TANESCO – Rex Attorney – kwamba mahakama iliridhika kuwa alilazimishwa kuweka saini uhamishaji mkataba kutoka Richmond hadi Dowans.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo (uk. 8), ICC inaeleza ilivyokubaliana na kila ushahidi, isipokuwa ushahidi wa Henry Surtees ambaye ni mfanyakazi katika kampuni ya Rostam, Caspian Limited.

Siku tatu zilizopita Rais Jakaya Kikwete alikana kufahamu wamiliki wa Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Limited. Kauli yake imekuja miaka mitano baada ya kukiri hadharani kuwa rafiki wa karibu wa Rostam Aziz.

Mashahidi wengine katika shauri hilo la madai Na. 15947/VRO kati ya TANESCO na makampuni ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd., ni Subira Wandimba, mwanasheria wa TANESCO, Balozi Fulgence Kazaura, mwenyekiti wa bodi ya TANESCO na Dk. Idris Rashid, aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TANESCO.

Mashahidi wengine ni Jamhuri Ngelime, mkurugenzi wa fedha wa TANESCO na Boniface Njombe, mhandisi mkuu wa miradi wa shirika hilo.

“Jopo la majaji liliridhika kuwa mashahidi wote waliotoa ushahidi, walifanya hivyo kwa uaminifu na kwa kadri ya kile walichoweza kukikumbuka na ushahidi wao ni wa kuaminika,” inasema hukumu ya ICC.

Tofauti pekee ilionekana katika ushahidi wa Bw. Surtees ambaye jopo linasema alionekana wazi kukwepa kujibu maswali kuhusiana na maslahi na umiliki wa kampuni ya Caspian Ltd., na Dowans Tanzania Limited (DHL) na pia kuhusiana na utata wa nafasi ya ushirika wa Bw. Rostam Aziz katika historia ya mgogoro huu.

Mahakama inasema imeuchukua “ushahidi wake kwa tahadhari, kwa kuwa Bw. Surtees alikuwa pia anakwepa kueleza uhusiano wake na Dowans.”

Katika toleo lililopita la gazeti hili, tulichapisha taarifa mbalimbali zinazomhusisha Rostam na Dowans/Richmond – kampuni iliyopewa mkataba kwa upendeleo, huku ikiwa haina fedha, utaalam wala historia ya kufua umeme. Makampuni hayo yalibadilishana mkataba tarehe 23 Desemba 2006 kinyume cha sheria za nchi.

Hata hivyo, habari zinasema toleo la MwanaHALISI lililokuwa na taarifa hizo, lilihujumiwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa baadhi ya watu ambao hawajafahamika, kununua nakala nyingi na mara nyingi ili kuziondoa sokoni.

Maeneo ambayo gazeti lilipatikana kwa shida kutokana na watu wachache kununua nakala nyingi, ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza, Iringa na Mbeya.

Toleo hilo lilikuwa na taarifa juu ya mamlaka ambayo Rostam alipewa na Dowans. Hiyo ni pamoja na kuajiri mawakili, kudai, kushitaki na kupokea malipo yoyote ya fedha kwa niaba ya kampuni.

Kazi nyingine ambazo Dowans ilimpa Rostam, ingawa yenyewe haikuwa na shughuli zozote, ni kufunga na kufungua akaunti za benki za kampuni hiyo na kununua au kuuza hisa za kampuni pale atakapoona inafaa.

Nafasi ya Rostam katika “biashara” hii inamwezesha kudai, kufungua madai, kukazia hukumu, kutumia fedha kwa biashara, kuajiri washauri na maajenti kwa shughuli za kampuni.

Mamlaka ya Rostam yanahusu pia kutetea kampuni, kujibu au kupinga hoja au hatua zozote kisheria zinazogusa kampuni katika biashara zake za sasa na hata za baadaye.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, iwapo mahakama itaamua TANESCO ilipe Sh. 94 bilioni, ni Rostam atakayechukua malipo hayo na kupanga jinsi ya kuyatumia.

Maelezo kwenye hati ya mamlaka yanasema Rostam ataendelea kuwa na mamlaka hayo hadi atakapopewa taarifa ya kuyasitisha.

Pamoja na mamlaka ya Rostam kushitaki na kukazia hukumu ili kupata akitafutacho, wasuluhishi wa ICC wamekiri kuona kuwa alifanya ushawishi mkubwa katika kuhakikisha kampuni yake hiyo inapata zabuni ya kufua umeme nchini, nje ya utaratibu wa kisheria.

Kwa mfano, wakati wa kesi hiyo, ilielezwa jinsi Rostam alivyotumia mamlaka yake ndani ya serikali kushawishi TANESCO kutoa zabuni ya kufua umeme kwa kampuni ya Richmond ambayo haikuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo.

Rostam alijua, kwa sifa za kawaida za uchambuzi wa zabuni, Richmond isingeweza kupata zabuni hiyo ya kufua umeme mwaka 2006, imeeleza taarifa ya kampuni ya uwakili ya Rex Attorney iliyoitetea TANESCO.

Bali, mahakama ya ICC inasema, “Bw. Rostam Aziz alikuwa kwenye nafasi ya ushawishi mkubwa juu ya kampuni ya Dowans, hata kama haijulikani alikuwa na maslahi yanayoeleweka katika makampuni hayo.”

Hata hivyo, ICC imesema katika mazingira ya Dowans/Richmond na jinsi Rostam alivyonufaika binafsi, “…mahakama haiwezi kuchunguza.”

Wiki mbili zilizopita, gazeti hili liliripoti mwanasheria maarufu, mbunge na naibu waziri wa Miundombinu, Dk. Harisson Mwakyembe akisema aliyeleta balaa la Dowans ni Rostam Aziz.

Mwakyembe alinukuliwa akisema ndani ya mkutano wa wabunge wa CCM jijini Dar es Salaam, “…mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu; anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi.”

Bro. Naumiza kichwa changu kutafakari-kwani watz walowengi wamezoea habari za udaku hata kwenye ununuzi wa magazeti pia, wanasiasa walifanya kazi kubwa sana, hasa ya kushika akili za watu na kusema uongo kuwa ukweli tokea janauri hadi desemba, kutoka kwenye hicho kufungo ni lazima ufanye maamuzi magumu bro. Leo utaambiwa fisadi na ushahidi wanao na kesho wanasema mwenye ushahidi na aende mahakamani-na unapiga makofi kwa shangwe kubwaaaaa!!!!!!!!!
 
Huyu ROSTAM AZIZ HUYU. ..40 YAKE IMESHAFIKA. ..
 
Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
Mbowe lazima alipe Kodi
 
Ikiwa ni kweli anadaiwa, lazima alipe kodi ila hapa najaribu kuwaza tu kwa sauti, huyu DC aliemkalia kooni kuhusu kodi kwani mamlaka husika haipo katika kulisema hilo? Hapa napata ukakasi mbona
Atakuambia mamlaka ni uongozi wa wilaya...na yeye ni mkuu wa wilaya.
 
Ni sawa kuwa kodi inapaswa kulipwa na wafanyabiashara wote.

Ila kwa mtu mwenye akili lazima utajiuliza yafuatayo:~

■ Serikali zilizopita hazikuona hayo makosa mfano kulima karibu na chanzo cha maji?

Kuvuta maji mtoni kwaajili ya umwagiliaji kuna tatizo gani? Na ni yeye peke yake anayevuta hayo maji?

Na kulikuwa na conditions alizowekewa akakiuka?

■ Hiyo kodi ya Mil. 13 ndio inayokwamisha utimizaji wa ilani ya CCM?

■ JE , ni Mbowe pekee ndiye anayedaiwa kodi? Mbona ameandamwa sana na kuunganishiwa makosa mfululizo?


INASHANGAZA KWAKWELI.
 
...Na wewe kwa akili yako unaona ni sawa kwa Serikali kuweka juhudi kubwa kumfuatilia Mbowe mkwepa kodi lakini wakati huo huo inashindwa kuweka juhudi kama hizo kuwafuatilia mafisadi na wezi akina Lugumi, Escrow na ambao wamechota bilioni 37 na 321 billion na kugawa rushwa mpaka ndani ya Ikulu! na unakubali ujinga wa kuambiwa kwamba eti hafukui makaburi ya zamani! Ila hili kaburi jipya la Mbowe ndiyo la kufukua! ama kweli akili ni nywele kila mmoja ana zake.

Tia akili kichwani achana na kukurupuka na kuropoka kama kasuku.

Hata kukwepa kodi ni kuiba, kwa hiyo huyu.ni mwizi analiibia taifa na hana dalili za kubadilika.

Huyu ni sugu, historia inasomeka hivo
 
Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.
Kwahyo na mbowe naye risiti za malipo amepoteza?
 
Ahsante sana Mkuu mafisadi wa EPA $133 million, Rada $42 million, Meremeta $155 million, Richmond/Dowans $100 million, IPTL still counting, Symbions, Escrow 321 billion, ndege ya Rais, Wakwapuzi wa pesa za Wahanga bilioni 16, wakwapuzi wa nyumba za Serikali close to 1 trillioni, Wabunge wa MACCM waliochota 10 millioni kila mmoja, Lugumi kachota 37 billion, waliosaini mikataba ya kifisadi na rasilimali za nchi na makampuni ya nje na pia China wote hawa ni MACCM hakuna hata anayeguswa au kutishiwa mali zake kuuzwa lakini wamemshupalia Mbowe tu kila kukicha!

Hakuna asiyetaka Mbowe asilipe kodi lakini cha kushangaza hatuoni juhudi kama hizo za vyombo huska vya sheria kuwafuatilia mafisadi wote hawa ili wapewe mvua za uhakika na ikiwezekana wafilisiwe mali zao kwa ufisadi mkubwa walioufanya nchini. Magufuli mshahara wake kwa mwaka ni 410 million halipi kodi! lakini wanaenda kukamuliwa wenye mishahara ya laki mbili wakati huu mshahara ambao kwa miaka 10 ni sawa na 4.1 billion (kama hautaongezwa) haukatwi hata senti moja ya kodi! Huu ni UNDUMILA KUWILI wa hali ya juu! Msumeno wa MACCM unakata pale wanapohusika watu wa UKAWA tu lakini wa MACCM wanakingiwa kifua kwa visingizio kwamba hataki kufukua makaburi ya zamani!! Hivi ni kipengele kipi cha sheria za nchi au katiba ambacho kimemzuia kufukua makaburi ya zamani?

Ni sawa kuwa kodi inapaswa kulipwa na wafanyabiashara wote.

Ila kwa mtu mwenye akili lazima utajiuliza yafuatayo:~

■ Serikali zilizopita hazikuona hayo makosa mfano kulima karibu na chanzo cha maji?

Kuvuta maji mtoni kwaajili ya umwagiliaji kuna tatizo gani? Na ni yeye peke yake anayevuta hayo maji?

Na kulikuwa na conditions alizowekewa akakiuka?

■ Hiyo kodi ya Mil. 13 ndio inayokwamisha utimizaji wa ilani ya CCM?

■ JE , ni Mbowe pekee ndiye anayedaiwa kodi? Mbona ameandamwa sana na kuunganishiwa makosa mfululizo?


INASHANGAZA KWAKWELI.
 
Dah huruma inanijia kwa waliopo hilo shamba ukisikia eka 2 ni eneo dogo sana ila kwa Mbowe pana green house eneo lote na anazalisha mazao kama nyanya,hoho etc na anauza nnje ,kwa anaejua green house utaelewa na kuona eka mbili ilivyo eneo kubwa na limekula kiasi gani cha pesa je toka linaanza hawakuliona hilo !!?? Usiasa pembeni ila hii ni kumfilisi mtu nawafahamu watu ambao wameajiliwa hapo ndio wanakosa ajira tena wapo wataalam wengi sana wa kada ya kilimo achana mbali na vibarua sababu pale ni as kampuni kuna mpaka uongozi wake binafsi ,makampuni mengi ya madawa na mbolea huwa yanaenda pale kuuza bidhaa zao ila sasa dah pole yao wengi twamuona Mbowe ila kuna watu zaidi ya mia mbili wanaumia kwa hili
 
Dah huruma inanijia kwa waliopo hilo shamba ukisikia eka 2 ni eneo dogo sana ila kwa Mbowe pana green house eneo lote na anazalisha mazao kama nyanya,hoho etc na anauza nnje ,kwa anaejua green house utaelewa na kuona eka mbili ilivyo eneo kubwa na limekula kiasi gani cha pesa je toka linaanza hawakuliona hilo !!?? Usiasa pembeni ila hii ni kumfilisi mtu nawafahamu watu ambao wameajiliwa hapo ndio wanakosa ajira tena wapo wataalam wengi sana wa kada ya kilimo achana mbali na vibarua sababu pale ni as kampuni kuna mpaka uongozi wake binafsi ,makampuni mengi ya madawa na mbolea huwa yanaenda pale kuuza bidhaa zao ila sasa dah pole yao wengi twamuona Mbowe ila kuna watu zaidi ya mia mbili wanaumia kwa hili
Nimekuelewa vyema mkuu


Mafahari wapambanapo...nyasi ndio huumia.
 
Mbowe haishindwi kulipa sjui 1bl au izo 13ml
anamiliki biashara nyingi ndani na nje ya tz....
Swala ni je anadaiwa kihalali?
 
Back
Top Bottom