Serikali na mishahara ya Septemba 2011

Mpaka sasa watumishi wa sekta nyingi za serikali hawajalipwa mishahara yao, kitu ambacho si kawaida. Tumezoea kulipwa kati ya tarehe 22 - 25 ya kila mwezi lakini sasa tunaingia siku ya mwisho kabisa ya mwezi na hakuna hata dalili, napenda kujua wadau, AU NDO PESA ZETU ZIMEENDA IGUNGA? maana nasikia CCM wametumia karibu 10bl kwa ajili ya ukaguzi. Naomba majibu kwa atakaye kuwa nayo. Asante

Upo wapi serikali za mitaa au serikali kuu? Sisi wa mitaa tumeshamaliza mishahara ya Septemba, au unamaanisha mishahara ya Oktoba?
 
Kwani mawaziri walioenda Igunga ni wa serikali kuu au ya mitaa?
 
mishahara imeingia toka majuzi na kuisahau tumeshaanza uisahau, wewe unasema mshahara leo pole zako.
 
Watu walio olewa wanawaringia sana wenzao!!!!!! Aliyekupa wewe mume ndiye aliye mnyima yeye, sidhani kama kutokuolewa kwake yeye alipenda.

kweli naona una machungu, kuolewa ni bahati tu, japo hata hiyo bahati MUNGU anaweza akaikatiza, hivyo shukuru kwa kila jambo.
 
Maulamaa wanalipwa bei gani?
Mi nilijua ubwabwa kwa azam cola tu na kabaha ka kaki kaliko konda sana....yani 20k hivi basi.
mishahara imepelekwa igunga kwenye kampeni chafu za kuhonga maulamaa... halafu rostam kagoma kuwakopesha hela za kulipa mishahara
 
Usiishi kwa kutegemea mshahara kijana tafuta vyanzo vya mapeneee
Wakati mwingine inalazimu uishi kwa kutegemea salary. Fikiria unaamka asubuhi sana kwenda kazini, na unatoka kazini (ulikoajiriwa) jioni sana au usiku, hiyo kazi nyingine ya kukuingizia kipato utaifanya muda gani? Ukisema umuachie mtu asimamie shughuli yako nyingine, utaishia kupata presha, anaiba kweli kweli kwani naye ana njaa. Kwa masaa yetu ya kazi yalivyo na miundombinu ya barabara zetu, kuna mahali patalega tu, either kwako au ulikoajiriwa.
 
Mwita 25, unadanganya na kuwahadaa watu, si wafanyakzi wa serikali kuu wala serikali za mitaa waliopata mishahara, isipokuwa wanajeshi tu
 
Mkuu huyu ni wa kumpuuuza kwani hajwahi kuwa serious hata kwenye mambo ya msingi.
 
Kwa kifupi mwezi huu watumishi wote wa umma wataanza kupata mishahara mipya. Kazini kwetu tumeshapewa hilo tangazo kuwa mishahara ni tarehe 4 oktoba. Hiki ni kitu cha kawaida kila mwaka mishahara mipya inapoaanza kulipwa huwa inachelewa , wandungu poleni habari ndiyo hiyo
 
Mshahara mpya?Upi huo mkuu.
 
Mpaka sasa watumishi wa sekta nyingi za serikali hawajalipwa mishahara yao, kitu ambacho si kawaida. Tumezoea kulipwa kati ya tarehe 22 - 25 ya kila mwezi lakini sasa tunaingia siku ya mwisho kabisa ya mwezi na hakuna hata dalili, napenda kujua wadau, AU NDO PESA ZETU ZIMEENDA IGUNGA? maana nasikia CCM wametumia karibu 10bl kwa ajili ya ukaguzi. Naomba majibu kwa atakaye kuwa nayo. Asante

Pesa zimepelekwa Igunga na nyingie amesafiria Fisadi Papa Kikwete. Subirini mpaka TRA wazunguke mitaani
 
Hongera ndugu yangu Palalisote kwa taarifa yako ni kweli wengi wa wafanyakazi wamekuwa katika dilemma kuwa nn tatizo?
 
Kwa kifupi mwezi huu watumishi wote wa umma wataanza kupata mishahara mipya. Kazini kwetu tumeshapewa hilo tangazo kuwa mishahara ni tarehe 4 oktoba. Hiki ni kitu cha kawaida kila mwaka mishahara mipya inapoaanza kulipwa huwa inachelewa , wandungu poleni habari ndiyo hiyo

This is Crap, pesa yote mmeenda kuifanyia kampeni huko Igunga
 
poleni wapendwa vpwa igunga nao hawajalipwa?? au ndio maana wanapewa sukari, unga, mchele na vijisent kupunguza makali ya njaa
 
Upo wapi serikali za mitaa au serikali kuu? Sisi wa mitaa tumeshamaliza mishahara ya Septemba, au unamaanisha mishahara ya Oktoba?
Hatushangai kwasababu mshahara wako unaupata kupitia kwa Nape Nnauye aliyekuajiri kuleta lijisura lako humu JF. Siajabu hata mshahara wa mwezi wa Octoba 2011 ulishamaliza.
 
Back
Top Bottom