KijanaHuru
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 1,822
- 2,332
Habari ya jioni wana JF
Poleni na kazi za kutwa,
Salamu zangu chache kwa serikali, kuweza kutatua suala hili mapema lisije likawa kama mv nyerere na matukio mengine ambayo huenda yangechukuliwa hatua mapema tusinepata maafa makubwa kama hayo.
Kuna hii barabara ya kutokea chanika au gongo la mboto kuelekea Kariakoo,Mnazi,Kivukoni,mbagala,Ubungo nk hiii barabara iko vizuri sana napia naipongeza serikali kwa kuiweka kuwa pana vya kutosha ila shida iko moja tu ukifika Banana Unapokuwa unatokea Ubungo,Buguruni,Kariakoo,Mnazi Mmoja,Kivukoni,Temeke,Mbagala,Makumbusho,Masaki,Tegeta na unaelekea Kuja Gongo Lamboto ama Chanika,
Unapofika pale banana ile stand haijajengwa ni dimbwi limejichimba kiasi kwamba gari inapopaki kushusha abiria gari linainamia ama kuegemea upande wa kushoto sasa kwakuelekea gongo lamboto kiasi ambacho ni hatarishi mno kwa maisha ya abiria
Siku hizi naogopa kabisa kupanda daladala naona bora nikapanda bajaji ama nikadandia bodaboda gari pale nirahisi mno kupinduka hasa kuanzia mchana wakati watu wanarudi kutoka makazini basi pale pana hatarisha mno na kadri siku zinasogea lile shimo linaongezeka
Serikali na viongozi wengine mnaohusika naombeni kwakweli mtusaidie watumiaji wabarabara za huku kote vituo viko salama ila shida ni upande mmoja wa hapo banana karibu na jengo la hali ya hewa.
Kwa wengine ambao mmepita hapo mnaweza kuongeza hoja kwa jinsi panavyohatarisha maisha ya raia.
Salamu zangu zifike kwenu waheshimiwa mtuhurumie
"Tuzibe Ufa Mapema Tusije Kujenga Ukuta"