Asalaam alekyum wana ukumbi!
Jana nimeshuhudia walimu mbalimbali wilaya ya Nyamagana wakipaza sauti zao kwa pamoja; kupinga makato ya sh 10,000/= kwenye mishahara yao kwa lengo la kujenga maabara sekondari.
Kujenga maabara ni jambo jema sana tena sana! Lakini kitendo cha kukata pesa bila kuwashirikisha walimu ni uonevu na ukiukwaji na utawala wa kisheria.
Mbona pesa za kuwalipa wajumbe wa bunge la katiba hazikuleta shida zilipatikana na mabilioni yaliteketea Dodoma? Kwa nini serikali isitafute pesa kama ilivyofanya kwenye bunge la katiba ili maabara zijengwe? Inakuwaje mtumie ubabe kwa njia kandamizi wakati wachache ndiyo wanafaidi keki ya Taifa walio wengi wanaumia!
Ukienda vijijini wananchi wanakamatwa eti hawakwenda kwenye maendeleo ya shule za kata na ujenzi wa maabara; hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila raia mpenda haki; na maendeleo, kwani ccm wanatumia nguvu za wanyonge kujinufaisha wenyewe.
Nawaomba msiwanyanyase walimu laana itawaumbua nyie wote mlio shika madaraka! Kwa nini hamkuwakata wajumbe wa bunge la katiba! badala yake wakatwe watumishi wa umma wakiwemo walimu ambao mishahara yao inaishia kwenye kulipa riba kwenye mabenki?
Watanzania acheni kulala usingizi fanyeni maamuzi magumu! Hii ni vita pambaneni haki itendeke kwani pesa zinatumika vibaya hili halikubariki.
Chanzo taarifa ya habari ITV.