Watu mnahasira sana! Tuwaombee walimu jamani wainusuru nchi yetu kwani wao wakiamua changes will come!
Karumbeta ndugu yangu, siyo hasira aisee. Mi naomba nitofautiane Na wewe kuhusu suala la kuwaombea. Naomba tusimhusishe Mungu katika hali hii tunayoiona kwa waalimu.
Maarifa wanayo lakini hawataki kuyatumia, hata Kama wamefungwa akili sisi tunaoona tunwaambia wabadilike hawataki. Sisi tutasemaje Karumbeta? Mungu alishawafanya wakawa wengi, silaha ambayo hutumika kufanya mazuri Na mabaya (rejea katiba mpya). Nao basi watumie huo wingi wao wafanye kitu cha kuwakomboa.
Aisee wanakatwa kwenye mshahara????sio wanaambiwa wachange???Ikulu ilishatoa maelezo kuwa ni hiyari kwa mtumishi wa umma kuchanga pesa kwa ajili ya mirad ya maendeleo. Sio lazima-kama wanakatwa wanaweza kushtak maana mkataba wa ajira hausemi hivo na KATIBU MKUU KIONGOZI ALISHALITOLEA UFAFANUZ HILO
Ngugu! Ni hatariii!! Ungeona jana mama mmoja (mwalimu) alipokuwa akipaza sauti akitoa machozi ungelia ndugu! Tuwe na busara katika kufanya maamuzi hii ni nchi yetu sote tusikubali hata kidogo.
Mtwara manispaa walimu wanalazimishwa kuchanga
30,000 ya maabala.
13,000 ya mwenge
5,000 mfuko wa Elimu. HII NDIO SERIKALI SKIVU DUNIANI
Acha wakatwe hata hiyo hela ni kidogo sana, walimu wengi ni wajinga ukubali au ukatae habari ndio hiyo kwani na mimi nilikua mwalimu kwa miaka miwili nilijionea mwenyewe ujunga wa walimu japo wamesomea lakini usomi wao walio wengi ni bure, kwanza hawajiamini hata kidogo hata mfagiaji wa ofisi ya mkurugenzi anawatisha mpaka wanapiga magoti walimu wenye degree zao. Kuwa mwalimu inakubidi uwe mjinga wa kupitiliza vinginevyo kazi itakushinda kama sisi tulivyoamua kuacha kazi tukaja mtaani ku burn CD. Ualimu ndio kazi ya mwisho kabisa ambayo kila mtumishi anajifunzia kutoa makaripio na kupiga biti. Acha walimu wakome kwanza ndio siku moja watajua nini maaana kuikataa CCM
ni kweli, mtaji wa CCM siku zote ni kwa watu wasiojielewa kama hawa - CCM hawana makosa acheni wawatumia wanavyotaka.Mkuu, waalimu Ni jeshi kubwa lisilojitambua. Hawana umoja Na sijui Kama wanao huo mpango wa kuwa wamoja siku moja. Mi nadhani hawajapewa kitu inauma. Madhila wanayopitia halafu unakuta May Day wanajitoa ufahamu badala ya kuonyesha hisia zao wanabaki wanachekacheka halafu yakiwafika wanakimbilia JF.
Mi nadhani wawakate mishahara pasu kwa pasu Ili kisu kiguse mfupa. Vinginevyo mwenyewe huwa anasema kelele za mlango hazina madhara kwenye usingizi. Watapiga kelele bila kuchukua hatua Na kukatwa mishahara watakatwa, wakitangatanga watapigwa Ili watulie tuliii......
mdau hili suala linazungumzika,hakuna sheria inayolazimisha mtu kuchangia hii kitu,huyo mama analia bure tu yeye aende mahakaman,halafu naona CWT wapo kimyaaa kwenye hili
Mwaka huu BRN itapeleka mpaka div 60. Ndo mkakati wa sasa. Jipange waalimu kwq matokeo makubwa sasa bila big salary ghafla. Oyeerrrrr waalimu.
Hii nchi kwa kweli inashangaza sana, kwann hiyo fedha ya kujenga maabara za shule za sekondari wasikatwe wale wajumbe waliopitisha rasimu ya katiba mpya kwa mabavu!!!! kwani yale mabilioni yaliyoteketea kule dodoma kwenye mchakato wa bmk yalitoka wapi!!!! mbona hatukuchangishwa wananchi wote manake ile katiba ni ya wananchi wote wa tanzania, kwani hizo maabara watakaofaidika nazo ni watoto wa walimu tu!!! huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa walimu wa tanzania na watumishi wote..
Mkuu, waalimu Ni jeshi kubwa lisilojitambua. Hawana umoja Na sijui Kama wanao huo mpango wa kuwa wamoja siku moja. Mi nadhani hawajapewa kitu inauma. Madhila wanayopitia halafu unakuta May Day wanajitoa ufahamu badala ya kuonyesha hisia zao wanabaki wanachekacheka halafu yakiwafika wanakimbilia JF.
Mi nadhani wawakate mishahara pasu kwa pasu Ili kisu kiguse mfupa. Vinginevyo mwenyewe huwa anasema kelele za mlango hazina madhara kwenye usingizi. Watapiga kelele bila kuchukua hatua Na kukatwa mishahara watakatwa, wakitangatanga watapigwa Ili watulie tuliii......