Serikali mnawanyonga Walimu!

Serikali mnawanyonga Walimu!

Wakatwe tu kwani hawauoni mfumo huu ni mmbovu na bado wanaukumbatia !!!!.
 
na ukifika uchaguzi wao ndio wa kwanza kuisaidia ccm kuiba kura, acha wakatwe tu labda 2015 watatusaidia kwenye mapambano ya kuitoa ccm.

Mkuu, waalimu Ni jeshi kubwa lisilojitambua. Hawana umoja Na sijui Kama wanao huo mpango wa kuwa wamoja siku moja. Mi nadhani hawajapewa kitu inauma. Madhila wanayopitia halafu unakuta May Day wanajitoa ufahamu badala ya kuonyesha hisia zao wanabaki wanachekacheka halafu yakiwafika wanakimbilia JF.
Mi nadhani wawakate mishahara pasu kwa pasu Ili kisu kiguse mfupa. Vinginevyo mwenyewe huwa anasema kelele za mlango hazina madhara kwenye usingizi. Watapiga kelele bila kuchukua hatua Na kukatwa mishahara watakatwa, wakitangatanga watapigwa Ili watulie tuliii......
 
Asalaam alekyum wana ukumbi!

Jana nimeshuhudia walimu mbalimbali wilaya ya Nyamagana wakipaza sauti zao kwa pamoja; kupinga makato ya sh 10,000/= kwenye mishahara yao kwa lengo la kujenga maabara sekondari.

Kujenga maabara ni jambo jema sana tena sana! Lakini kitendo cha kukata pesa bila kuwashirikisha walimu ni uonevu na ukiukwaji na utawala wa kisheria.

Mbona pesa za kuwalipa wajumbe wa bunge la katiba hazikuleta shida zilipatikana na mabilioni yaliteketea Dodoma? Kwa nini serikali isitafute pesa kama ilivyofanya kwenye bunge la katiba ili maabara zijengwe? Inakuwaje mtumie ubabe kwa njia kandamizi wakati wachache ndiyo wanafaidi keki ya Taifa walio wengi wanaumia!

Ukienda vijijini wananchi wanakamatwa eti hawakwenda kwenye maendeleo ya shule za kata na ujenzi wa maabara; hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila raia mpenda haki; na maendeleo, kwani ccm wanatumia nguvu za wanyonge kujinufaisha wenyewe.

Nawaomba msiwanyanyase walimu laana itawaumbua nyie wote mlio shika madaraka! Kwa nini hamkuwakata wajumbe wa bunge la katiba! badala yake wakatwe watumishi wa umma wakiwemo walimu ambao mishahara yao inaishia kwenye kulipa riba kwenye mabenki?

Watanzania acheni kulala usingizi fanyeni maamuzi magumu! Hii ni vita pambaneni haki itendeke kwani pesa zinatumika vibaya hili halikubariki.

Chanzo taarifa ya habari ITV.

Kichwa cha post yako ni kinzuri "serikali mnawanyonga walimu" lakini kimanti ingekuwa "serikali inajinyonga yenyewe endapo tu serikali inamaana ya watu (wananchi) hata hivyo ina maana pale tu wananchi wana maamuzi lakini kwa nchi yetu serikali ni "mchwa" huu ni msamiati mpya kutoka kwa mkuu wa kaya aliyoitoa wiki iliyopita akimaanisha watumishi wa serikali ambao ni serikali yenyewe. Sasa neno "Mchwa" lina maana nyingi kwakuanza tu hawa sio watu ni "wadudu" .............. endelea na nyingine.

Kimsingi hata kumshirikisha tu mwalimu kukatwa mshahara wake ilikuchangia ujenzi wa maabara ni kosa kwani walimu kama raia wengine wa nchi hii wana mitaa yao hivyo walitakiwa kupitia serikali za mitaa yao wachangishwe kama wananchi wengine. Tambua hata kama watashirikishwa walivyowanyonge wangeweza kukubali hata kama hawapendi kwani wengi wao ni waoga hata kwenye haki zao.

Wa kulamiwa na kulaniwa ni yule aliyetoa tu wazo an wote waliosapoti na wanaoendelea kusapoti kwani jambo hili lina madhara makubwa kuliko hata kawaida. Busara ya walimu na silaha yao kuu kwa miaka ya hivi karibuni ni migomo baridi (passive resistance) ambayo hata hivyo wanaoumia ni masikini wenzao na wenyewe. Hasira za walimu zitaishia kutofundisha, je madhara yatakuwa kwa nini? Kimsingi suala hili haliwahusu walimu tu japo wao ndiyo waathirika wa mojakwamoja lakini sisi masikini ni waathirika wa pili ambao ndio tutakao pata madhara makubwa.

Watanzania tunapaswa tusilifumbie macho jambo kama hili kwani lina madhara makubwa. Hivi watanzania wenzangu, tumesema Richmond, EPA, Katiba ni jambo la wanasiasa(UKAWA) Mwangosi, ulimboka ya waandishi wa habari, kubomolewa nyumba ya wale wanaojenga barabarani, kunyang'anywa viwanja kwa wasiojua sheria, kukatwa mishahara la walimu, sasa lipi la kitaifa?, lipi litatokea sisi watanzania tutasema hiki ni kilio cha wote??. Nahisi kama tanzania sio "Taifa?"

"Kwa mwanaume mwenye akili timamu hatapenda hata kushirikishwa kama mwanaume mwenzake anapenda wawe na uhusiano wa kingono kwani jambo lenyewe tu ni baya"
 
Hilo litakuwa jambo jema, Walimu watapata akili maana bado wamelala na ndiyo wamesaidia kukwamisha mabadiliko ya kisiasa nchini!! Walimu wana nguvu sana huko vijijini............... kama wangekuwa wameamka CCM wasingekuwa wanawachezea.
 
Mimi ni mwalimu na nimekataa kata kata kutoa.. tuliambiwa elfu 20.. na wakikata mshahara wangu hata kumi.. mtasikia nimeondoka na komputa ya mkurugenzi ..shwain!
 
Mimi ni mwalimu na nimekataa kata kata kutoa.. tuliambiwa elfu 20.. na wakikata mshahara wangu hata kumi.. mtasikia nimeondoka na komputa ya mkurugenzi ..shwain!
Wape changamoto wenzio, ila omba wasikugeuke Na Mungu awape ujasiri. Kila la Kheri.
 
Bnafsi sidhani kama walimu wetu Tz wanajitambua, wapo weak saa ktk kutetea maslahi yao, ni waoga na hawajiamini mie huwa sielewi ni kwanini, unaesemaje hukushirikishwa wakati hilo ni jukumu la serikali yenyewe kuhakikisha mahtaji yanayofanya shule iitwe shule yanakuwepo??? ina maana mngeshirikishwa mngeridhia? walimu to be honest mmezidi kuwa waoga, hizo shule ni za serikali ambayo ktk mshahara wako pia unakatwa kodi na katka mahtaj mbalimbal ya nyumban pia unakatwa kodi...!!
 
Naam naam!! Nakubaliana na wewe bila chenga ndugu! Walimu wamuunge mkono mwalimu Nyerere haya wanayofanya ccm hasa katiba mpya hayafai hata kidogo! Walimu wanatuangusha naunga mkono hoja yako.
Subiri, limits of acceptable tolerance will be reached very soon. Na siku hiyo hatua ikifikiwa itakuwa Kama ilivyo gari ya kusukuma ikisha waka, total madness!
 
Mwalimu Kaijage badala ya kugombania hela za walimu wenziwe zinazokatwa pasipo kujua, yeye anagomaba na UKAWA. Shem on you Mwalimu Kaijage

Hayo nayo ya Kaijage yametoka wap tena? back to the topic! bange mbaya kweli. Hili ni jukwaa la great thinker tu! Kwa hoja zako nenda fb. Halafu tar 3 November 2014 utakua na mtihani wa NECTA, kaa utulie ujisomee.
 
Hilo litakuwa jambo jema, Walimu watapata akili maana bado wamelala na ndiyo wamesaidia kukwamisha mabadiliko ya kisiasa nchini!! Walimu wana nguvu sana huko vijijini............... kama wangekuwa wameamka CCM wasingekuwa wanawachezea.

Sasa mkuu ni sawa MAGAMBA wana wakandamiza raia wake! na hawafai kuendelea kuwa madarakani; na nadhan hata walimu wanalitambua hilo. BUT unafikiri ni chama gani kitawatendea haki wananchi? ktk nchi hii wababaishaji ni wengi sana, waliowengi wanapambana ili waingie kwenye mfumo wapate fursa ya kuwanyonya watanzania.
 
Bnafsi sidhani kama walimu wetu Tz wanajitambua, wapo weak saa ktk kutetea maslahi yao, ni waoga na hawajiamini mie huwa sielewi ni kwanini, unaesemaje hukushirikishwa wakati hilo ni jukumu la serikali yenyewe kuhakikisha mahtaji yanayofanya shule iitwe shule yanakuwepo??? ina maana mngeshirikishwa mngeridhia? walimu to be honest mmezidi kuwa waoga, hizo shule ni za serikali ambayo ktk mshahara wako pia unakatwa kodi na katka mahtaj mbalimbal ya nyumban pia unakatwa kodi...!!

Mkuu tatizo ni kuwa wengi wao wameipata hiyo ajira kimagumash hivi mtu aliyepata ajira kwa kutumia vyeti vya mtu mwingine anao ujasiri wa kutetea haki yake? wengi hukubali yaishe ili mkono uende kinywani ndio maana kule Kagera
walichapwa na hawakufanya lolote. tukubali hii fani imejaa mamluki wengi ni shiiideer
 
Subiri, limits of acceptable tolerance will be reached very soon. Na siku hiyo hatua ikifikiwa itakuwa Kama ilivyo gari ya kusukuma ikisha waka, total madness!

Yap! Tuombe Mungu tuzidi kuwa wazima na kitaeleweka.
 
Mimi ni mwalimu na nimekataa kata kata kutoa.. tuliambiwa elfu 20.. na wakikata mshahara wangu hata kumi.. mtasikia nimeondoka na komputa ya mkurugenzi ..shwain!

Very good teacher! Bunge la katiba lilitumia pesa vibaya iweje leo walimu wakatwe? Huu upuuzi unaofanywa na serikali ya ccm haufai hata kidogo! Kataeni huu ni usanii wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom