Serikali mnawanyonga Walimu!

Serikali mnawanyonga Walimu!

Sasa mkuu ni sawa MAGAMBA wana wakandamiza raia wake! na hawafai kuendelea kuwa madarakani; na nadhan hata walimu wanalitambua hilo. BUT unafikiri ni chama gani kitawatendea haki wananchi? ktk nchi hii wababaishaji ni wengi sana, waliowengi wanapambana ili waingie kwenye mfumo wapate fursa ya kuwanyonya watanzania.

ndugu ccm ile ya mwalimu Nyerere ilikwisha kufa! Ukubali ukatae poa! Chama kimebaki na majambazi huo ndiyo ukweli; na mara nyingi mfumo wowote duniani unapokaa muda mrefu ufanisi na makusudi ya huo mfumo hutoweka polepole kwa maana ya kwamba, wanaanza kuingia na watu wabaya na kuharibu malengo yote!

Hivyo basi! Niushauri wangu kwako na wote wanaopitia bandiko langu; kuamini kwamba! Ni lazima kubadili chama kingine cha siasa ili kichukue dola na kukipima kama tunavyowapima viongozi wa sasa na mwalimu Nyerere wanaonekana kupwaya na Nyerere anawafunika.

Tuwape UKAWA nafasi hii wainusuru nchi ndugu nchi imeuzwa na wahuni wachache haiwezekani tukae kimya even for Chadema let it be!
 
Asalaam alekyum wana ukumbi!

Jana nimeshuhudia walimu mbalimbali wilaya ya Nyamagana wakipaza sauti zao kwa pamoja; kupinga makato ya sh 10,000/= kwenye mishahara yao kwa lengo la kujenga maabara sekondari.

Kujenga maabara ni jambo jema sana tena sana! Lakini kitendo cha kukata pesa bila kuwashirikisha walimu ni uonevu na ukiukwaji na utawala wa kisheria.

Mbona pesa za kuwalipa wajumbe wa bunge la katiba hazikuleta shida zilipatikana na mabilioni yaliteketea Dodoma? Kwa nini serikali isitafute pesa kama ilivyofanya kwenye bunge la katiba ili maabara zijengwe? Inakuwaje mtumie ubabe kwa njia kandamizi wakati wachache ndiyo wanafaidi keki ya Taifa walio wengi wanaumia!

Ukienda vijijini wananchi wanakamatwa eti hawakwenda kwenye maendeleo ya shule za kata na ujenzi wa maabara; hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila raia mpenda haki; na maendeleo, kwani ccm wanatumia nguvu za wanyonge kujinufaisha wenyewe.

Nawaomba msiwanyanyase walimu laana itawaumbua nyie wote mlio shika madaraka! Kwa nini hamkuwakata wajumbe wa bunge la katiba! badala yake wakatwe watumishi wa umma wakiwemo walimu ambao mishahara yao inaishia kwenye kulipa riba kwenye mabenki?

Watanzania acheni kulala usingizi fanyeni maamuzi magumu! Hii ni vita pambaneni haki itendeke kwani pesa zinatumika vibaya hili halikubariki.

Chanzo taarifa ya habari ITV.

Jamani! Pesa zote zilizoteketea BMK zingetumika kujenga maabara tungeisifu sana ccm lakini pesa zimetumika kupitisha katiba feki ya chama cha magamba! Say no! Haiwezekani walimu wao ndiyo waishi maisha ya kuunga unga haiwezekani! Huu ni ubabaishaji wa ccm na msipofanya maamuzi mtakatwa kweli! Serikali mmechoka wapisheni UKAWA waendeshe nchi tumewachoka mafisadi wakubwa nyie!
 
Jamani! Pesa zote zilizoteketea BMK zingetumika kujenga maabara tungeisifu sana ccm lakini pesa zimetumika kupitisha katiba feki ya chama cha magamba! Say no! Haiwezekani walimu wao ndiyo waishi maisha ya kuunga unga haiwezekani! Huu ni ubabaishaji wa ccm na msipofanya maamuzi mtakatwa kweli! Serikali mmechoka wapisheni UKAWA waendeshe nchi tumewachoka mafisadi wakubwa nyie!

Ndugu! Nakushukuru sana kuchangia vizuri kwenye bandiko langu hakika dalili zinaonesha walimu wananyanyaswa na wajiandae kukemea manyanyaso kwenye chaguzi mbalimbali kwa kuikataa ccm!
 
mkuu halmashauri ndizo zinafanya upuuzi huo, na kama utachunguza ni hapo kwenu tu

na kama makada wangegundua wangefukuza wakurugenzi hao wanaokata mishahara ya watu. ni wizi na uporaji
 
Mama yangu anamiaka 75 wanamfuta atoe 12000 ya maabara ,nimemwambia asitoe ,na wakija kukudai waambie mm ndo nimekukataza .
 
Hawa ccm hawana huruma wanakula mpaka jasho la wasiojiweza wamelaaniwa
 
Back
Top Bottom