Serikali Mbona Inaogopa Kuliunga mkono Jiji Kuipata UDA yao?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,798
Shirika la mabasi ya UDA ilikuwa moja ya miradi ya jiji ambayo kama ingekuwa sio ubadhilifu wa viongozi waliokuwepo huko nyuma lingeleta mapato makubwa kwa jiji na kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wake.

Imedhihirika kuuzwa kwake ni utapeli na wizi mtupu. Mali hiyo ya umma inachukuliwa kijanja na serikali iko kimya.

Baada ya CAG Kudhibitisha kuwa UDA kisheria ni mali ya umma Jiji limeanza kupigania kurejesha mali yake.

Ajabu mbona serikali ya Magufuli kupitia msajili wa Hazina wako kimya? Mbona hawapiganii mali hii ya wanadar irudi?

Au Magu na Msajili kuna mtu wanamuogopa?
 
Mali ya uma walijimilikisha wastaafu waliomuweka Magu madarakani, atapata wapi ubavu wa kuwanyang'anya mali yao? Aonekane hana shukrani? Magu mjanja kuamua UKAWA wapewe jiji ilikuwa kukwepa hizi lawama, sio mimi ni HALMASHAURI ya jiji ikifika wakuu wamekaliwa kooni.
 
Maana ni kama vile Jiji wanapigana pekee yao.
Katika hili msajili wa hazina asipoliingilia litakuwa gumu na watu wataendelea kutafuna. Wanachonufaika nacho kikubwa hawa kina Simon Kisena ni kutumia assets za Uda Kukopea
 
Shirika la mabasi ya UDA ilikuwa moja ya miradi ya jiji ambayo kama ingekuwa sio ubadhilifu wa viongozi waliokuwepo huko nyuma lingeleta mapato makubwa kwa jiji na kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wake.
Imedhihirika kuuzwa kwake ni utapeli na wizi mtupu. Mali hiyo ya umma inachukuliwa kijanja na serikali iko kimya.
Baada ya CAG Kudhibitisha kuwa UDA kisheria ni mali ya umma Jiji limeanza kupigania kurejesha mali yake.
Ajabu mbona serikali ya Magufuli kupitia msajili wa Hazina wako kimya? Mbona hawapiganii mali hii ya wanadar irudi? Au Magu na Msajili kuna mtu wanamuogopa?
Hili suala la UDA lita wang'oa wafadhili wengi wa ccm
 
Maana ni kama vile Jiji wanapigana pekee yao.
Katika hili msajili wa hazina asipoliingilia litakuwa gumu na watu wataendelea kutafuna. Wanachonufaika nacho kikubwa hawa kina Simon Kisena ni kutumia assets za Uda Kukopea
unajua kuna kitu wadau hawakijui kuhusiana na UDA , lengo kuu la hawa matapeli halikuwa mabasi ya UDA au labda biashara ya usafirishaji , hii ni kuzugia tu , Hawa lengo lao kubwa ni kupora mali za UDA na kuzitumia kama dhamana .
 
Wananchi wanahitaji usafiri wa kueleweka sio blah blah za ukawa na maigizo ya kwenye tv
 
Maana ni kama vile Jiji wanapigana pekee yao.
Katika hili msajili wa hazina asipoliingilia litakuwa gumu na watu wataendelea kutafuna. Wanachonufaika nacho kikubwa hawa kina Simon Kisena ni kutumia assets za Uda Kukopea

Tatizo serikali ya CCM inakuwa kama ililazimishwa kukubali demokrasia ya vyama vingi. Bado wanasua sua sana kufanya kazi kwa ushirikiano na vyama vya upinzani.....!!
 
Wenyewe ndio wameuza sasa we unategemea waunge mkono si watajiumbua wenyewe
Meya wa jiji fanya kazi yako vizuri
 
Mali ya uma walijimilikisha wastaafu waliomuweka Magu madarakani, atapata wapi ubavu wa kuwanyang'anya mali yao? Aonekane hana shukrani? Magu mjanja kuamua UKAWA wapewe jiji ilikuwa kukwepa hizi lawama, sio mimi ni HALMASHAURI ya jiji ikifika wakuu wamekaliwa kooni.
Magufuli aliteuliwa tu na chama chake kupeperusha bendera kugombea uraisi na ujue hawakuwa na msafi mwingine aliekuwa msikivu kwa wenye mamlaka na kulinda hadhi na maslahi yao.Aliielewa nguvu ya mgombea wa Chadema na mapungufu/udhaifu mkubwa ndani ya chama chake kilichomteua na akabuni mbinu mpya kabisa.Katika kampeni zake na kote alikofanya mikutano ya hadhara alikwepa mara nyingi kulitamka jina la chama chake na alikuwa akijinadi kwa kusema haya. Wananchi nawaombeni mchagueni Magufuli mimi ni mtendaji zaidi ya kuwa mwanasiasa.Nimekua kiongozi kwa miaka ishirini serikalini nayajua maovu yote na nitatenda kadri ya ahadi ninazowapeni na siogopi mtu nitatenda kadri ya matakwa ya wananchi mnavyoniagiza na sheria zinavyotaka ili mpate haki zenu.Serikali yangu itakuwa ya watendaji wachache na itakuwa HAPA NI KAZI TU.Mnanifahamu utendaji wangu na nina nguvu nyingi ya kuwatumikia na mazoezi ya push ups yakifanyika majukwaani.Kwa kweli kauli hizi zilimjenga na kurudisha imani ya wananchi.Ila mnavyojua asili ni asili tu bado uccm damu kindaki ndaki upo.Sisemi hana anachofanya hapana anakubalika sana hata kwa wapinzani ni ile asili tu.Kwa maelezo hayo na ulemavu wa miaka yote baada ya kifo cha mwalimu Nyerere usitegemee serikali kuisaidia ukawa kupata sifa hata kama kinachogombewa kurudi serikalini ni mali ya umma.Watadai hatuwezi kuujengea sifa upinzani. Ni kama unavyoona bunge kutoonyeshwa live yote ni hofu hiyo hiyo ya kuwajenga wapinzani ilihali wanao uwezo kwa kila jambo.Wewe ushangae wanataka kuipeleka bajeti ya jiji bungeni hata kabla haijafanyiwa masahihisho na ukawa walioiandaa na ndicho mh.Kubenea na wenzake.wanachokataa.Nia na lengo lao ni kusomwa bungeni kama ilivyo na wao waifanyie masahihisho wanayopenda wao na kuituma kwa mkurugenzi wao(mteule wao) kwa utekelezaji na ukawa kuonekana hawawezi lolote.Yapo mengi wanayoweza kulazimisha wakiwa kama waongoza nchi.Upinzani muongeze wabunge wa majimbo muwe na sauti bungeni.Acheni makosa ya kuruhusu wagombea wawili wawili kwenye jimbo tena wote wakiwa ukawa kwani ni kugawa kura na kuruhusu ccm kushinda.Angalia alivyofanyiwa Mtatiro n.k.
 
Mali ya uma walijimilikisha wastaafu waliomuweka Magu madarakani, atapata wapi ubavu wa kuwanyang'anya mali yao? Aonekane hana shukrani? Magu mjanja kuamua UKAWA wapewe jiji ilikuwa kukwepa hizi lawama, sio mimi ni HALMASHAURI ya jiji ikifika wakuu wamekaliwa kooni.

Nadhani hii ni pointi muhimu - kwamba swala la UDA linaihusisha kwa karibu familia ya JK, hivyo kwa serikali ya JPM kulivalia njuga moja kwa moja ni kama JPM kumkabili mtangulizi wake head-on! Busara za JPM: Acha jiji waibuke nalo na waanike yaliyo nyuma ya pazia, na fate ya swala zima itakuwa dhahiri bila lawama kwa JPM moja kwa moja! Natumaini serikali haitaingilia kati kuwazuia jiji kuchimbua uozo huu na mingine itakayo kuwepo!
 
Wananchi wanahitaji usafiri wa kueleweka sio blah blah za ukawa na maigizo ya kwenye tv
Lione hili nalo! UDA kwani ya Ukawa au ya watu wa Dar?
Kwa taarifa yako UDA ilikuwepo kabla hata hiyo CCM yako haijakuwepo.
From DMT to UDA na sasa watu wanataka Mali yao
 
Nadhani hii ni pointi muhimu - kwamba swala la UDA linaihusisha kwa karibu familia ya JK, hivyo kwa serikali ya JPM kulivalia njuga moja kwa moja ni kama JPM kumkabili mtangulizi wake head-on! Busara za JPM: Acha jiji waibuke nalo na waanike yaliyo nyuma ya pazia, na fate ya swala zima itakuwa dhahiri bila lawama kwa JPM moja kwa moja! Natumaini serikali haitaingilia kati kuwazuia jiji kuchimbua uozo huu na mingine itakayo kuwepo!
Kwa suala la nyumba za serikali zilizouzwa kwa usimamizi wa jpm akiwa waziri enzi za utawala wa jk unashauri nini kifanyike, manake kosa bado lipo pale pale, mkosaji wetu tunamfahamu.
 
Kwa suala la nyumba za serikali zilizouzwa kwa usimamizi wa jpm akiwa waziri enzi za utawala wa jk unashauri nini kifanyike, manake kosa bado lipo pale pale, mkosaji wetu tunamfahamu.

Nafikiri nyumba unazozizungumzia ziliuzwa wakati wa utawala wa BWM na sio JK, ila nazo ni wajibu wa upinzani, vyombo makini vya habari, wanaharaka na wadau wengine mbali mbali kuliibua upya na kuendesha mijadala ya kitaifa kuhusiana na hili! Hapa sio swala la nyumba tu bali maeneo zilikokuwa hizo nyumba! Nyingi zilikuwa kwenye Plots za "Prime areas", na zilinunuliwa bei ambayo haiakisi thamani halisi ya Plots husika!
 
Asante kwa rekebisho, nami nikupe angalizo kuwa tusiongelee bei, maana tukiongelea bei kutahalalisha wazo la kuuza kwa wafanyakazi wa serikali hali ya kuwa hizo nyumba ni mali ya walipa kodi wote, kama ilibidi kuuzwa zingeuzwa kwa mnada aina ya bahatinasibu ya taifa, ili kila mtanzania awe na fursa ya kufaidi uhondo wa taifa lake.
 
Ikubukwe pia tabia ya kulindana hakuianza JPM pekee. Mnakumbuka issue ya Kiwira JK alifumba macho asimwumbue aliye mtangulia. Hivyo JPM naye hayamkini anafuata nyayo au anangoja timing.
 
Back
Top Bottom