barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kauli ya jana ya Rais kuwa hataweza kuitumbua kampuni ya Simon Group ambayo ni mali ya kada wa CCM na mshirika wa kibiashara wa "familia ya kwanza iliyopita" inazua maswali mengi sana.
Rais anasema amekubaliana na Simon Group kuwa na hisa za 51% na hivyo sasa Jiji la Dsm halina chake.
Huyu Simon Kisena ndiye yule ambaye Rais akiwa kule Mwanza kwenye ziara, alitangaza hadharani kuwa Simon Kisena "amekifilisi" chama cha Ushirika Nyanza kwa mabilioni ya shilingi na aakaagiza TAKUKURU na vyombo vingine vifanyie kazi ufisadi huu wa Simon Group wa kiwanda cha New Era.
Huyohuyo aliyeagiza huyu mtu atumbuliwe kule Nyanza leo huku UDA anampa nafasi la kuendesha shirika la usafiri ambapo ununuaji wake umejaa utata mtupu.
Hapa ndio wakati mwingine Ngosha anatuchanganya,huyu mtu report yake ya "ufisadi" kule Nyanza haijatoka,inakuwaje mnampa tena UDA ambalo nalo kuna figisufigisu nyingi?
UKAWA ndio wenye jiji,kuanzia Meya na Madiwani.Moja la jambo walilopewa kura na wakazi wa Dsm ilikuwa ni ahadi za kuifanya UDA irudi mikononi mwa jiji na si mtu mmoja.
UKAWA waliitisha kikao na waandishi wa habari,wakatuambia ndani ya Simon Group kuna wana hisa ambao ni Mama wa awamu iliyopita,Mwana wa kwanza wa awamu iliyopita na mtu wa tatu ni mbunge aliyekuwa jimbo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Magdalena Sakaya kule Tabora.
Hawa ndio UKAWA walituambia wanamiliki hizo 51% za hisa.Sasa inakuwaje leo wale UKAWA waliokataa kupokea hizo bilion 5 toka Simon Group waseme zimepokelewa?
Yaani UDA kweli na assets zake zina thamani ya bilion 5?UKAWA na Sizonje hapa mmetuangusha sana sana.Au ndio kweli kuwa UDA ni moja ya "makaburi" ambayo hayafukuliki??
Katika moja ya mkutano wa UKAWA na waandishi wa habari,Kubenea alisema,mkutano uliokabidhi UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne tu
Watu hawa ni Marehemu Dk. Didas Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa mwenyekiti; Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena ambaye alikuwa katibu; Mwanasheria wa jiji, Isaac Nassor Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip Mwakyusa.
Kubenea alinukuliwa akisema "Kwanza tunataka mtambue halmashauri haikuuza UDA kwa kuwa, Simon Group Limited wametumia hati ya UDA – mali ya wananchi kufanya biashara. Haturudishi fedha hizi mpaka tufanye hesabu, tujue kampuni hii imepata faida kiasi gani.
“Hata katika mradi wenyewe wa UDA-TR, kumesheheni utapeli. Unaoitwa mkutano mkuu maalum wa wana-hisa wa tarehe 10 Juni 2011, uliosimamiwa na Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji kuidhinisha pamoja na mengine, uuzaji wa hisa za UDA, haukuwa halali"
Sasa inakuwaje leo Waziri Simbachawene mbele ya hadhara atuambie kuwa UDA ilishauzwa hizo 51% kwa Simon Group na wakati mchakato ulikuwa batili?
Inakuwaje UKAWA wapo kimya na wakati walituambia kuwa UDA iliuzwa kinyemela na kwa usanii?Na watairudisha mikononi mwa jiji?
Inakuwaje Rais akubaliane na kuuzwa kwa UDA hizo 51% na aachane na dhamira ya "kuitumbua" Simon Group wakati kuna taarifa kuwa mchakato ulikuwa na usanii?
UKAWA na Rais wetu mpendwa,ni kama "mmeshirikiana" kuiuza UDA ya wananchi ktk mazingira ya kuhuzunisha na kushangaza.Hii UDA ni dhahiri kuwa ni moja kati ya yale makaburi yasiyofukulika.