Boniface Jacob: Zijue sababu za UKAWA kukataa fedha za kuuzwa kwa UDA

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Kifupi jana 27 january 2017 ilikuwa ni mara ya pili kwa baraza la jini DSM kupinga maamuzi ya uuzaji wa hisa za UDA

BARAZA LA CCM LILILOUZA UDA
lilifanyika 2012/2013 kufuatia taarifa iliyokuwa inaonyesha UDA inaendeshwa kwa hasara sana na hata muda mwingine fedha za mapato yanayokusudiwa haziji halmashauri ya jiji
Baraza hilo chini ya marehemu DIDAS MADABURI wa CCM na Majority CCM huku chadema wakiingia madiwani wawili tuh.

BARAZA LA 2015/2016 UKAWA Chini ya mstahiki meya ISAYA MWITA wakapitisha hoja ya kutengua na kutokutambua maamuzi ya kuuza UDA mnamo tarehe 2 may 2016
Jana ni mara ya pili baada ya miezi takribani saba ikipita hoja hiyo hiyo yenye mlengo uleule na watu wale wale walipaswa kufanya marejeo ya hoja ya je wanaafiki UDA kuuzwa au Hawataafiki? Na je kwa maana hiyo fedha zilizowekwa benk na "Purchaser" zikubaliwe kutumika kama njia ya kumaliza biashara ya uuzaji wa UDA.

HOJA ZA KUPINGA UUZAJI WA HISA ZA UDA KWENYE BARAZA MAY O2 2016 NA JANA PIA

1.Hapakuwa na maridhiano ya wanahisa kukubaliana kuuza kampuni ya UDA ambapo jiji na mwanahisa mwingine ni msajili wa hazina(Kwa niaba ya serikali kuu)

2.Hisa za halmashauri ya jiji ziliuzwa bila kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma ,ambapo simon Group waliuziwa kinyume na sheria inavyotaka,
hawakutangangaza wazi ili pawe na ushindani bali alialikwa binafsi tuh na wakamalizana naye bila ushindanishaji wa wanunuzi kama wenye nia wengine walihitaji.badala yake atunui alipataje taarifa kama Hisa za UDA zinauzwa.sababu hakuna tangazo lilotolewa rasmi.kama sheria inavyotaka

3.Hapakufanyika uthamini wa mali za UDA kujua kabla ya kuuza Hisa za UDA viwanja kama mbagala,gerezani kariakoo,kurasini,,majengo yote ya ofisi za UDA,mitambo ya UDA,na magari ya UDA,Brand ya neno"UDA",kafakana zote za kutenezea UDA,Kujua yalikuwa na thamani gani?

4.Mauzo ya hisa za halmashauri ya jiji hayakupata ridhaa ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa "TAMISEMI" kama sheria inavyotaka,kuwa kwanza ni lazima waziri husika alipaswa kuridhia.

5.kampuni ya UDA ilikuwa chini ya PSRC kama "specified companies" hivyo kabla ya uuzaji wa UDA palipaswa kufanywa mawasiliano na CHC (CONSOLIDATED HOLDING COOPERATION) hawa ndiyo wasimamizi wa mashirika ya UMMA kujua kama nao walikuwa na ripoti kuwa UDA ni hasara au la,badala yake wakarukwa na mauziano yakafanyika bila masiliano nao.

HIVYO MAAMUZI YA BARAZA YAKAWA KAMA IFUATAVYO

1.MAAMUZI YALIYOFANYWA NA BARAZA LILILOPITA KUHUSIANA NA UUZAJI WA HISA ZA JIJI JUU YA KAMPUNI YA UDA YAMETENGULIWA

2.FEZA ZILIZOINGIZWA KWENYE AKAUNTI YA HALAMASHAURI YA JIJI DSM KEA AJILI YA BIASHARA YA MAUZIANO YA HISA ZIRUDISHWE

3.KAMA SERIKALI KUU WATAHITAJI FEDHA HIZO KUZICHUKUA NA KUZITUMIA WACHUKUE TUH NI MAAMUZI YAO LAKINI BARAZA LA SASA LISITUMIE KABISA PESA HIZO KAMA KUHALALISHA BIASHARA HARAMU YA MALI ZA UMMA

MENGINEYO
1.Hii yumeisaida serikali inayopingana UFISADI lwamba hakuna ufisadi mzuri na mbaya wote ni UFISADI Kuwamakini na waandamizi au washauri wa Rais kwa maana wengine wanamslahi tofauti na UMMA

2.Kuweka KUMBUKUMBU sahihi kwa heshima waliyotupa wananchi kwa kuwa moja ya sababu ya watu wa Dar es salaam kuchagua UKAWA ilikuwa ni kukasirishwa kuuzwa kwa shirika lao la miaka MINGI kwa hila na UFISADI.

3.Ni heri kama serikali kuu watazitumia hizo fedha basi dhambi ya UDA haitokuwa juu yetu na vizazi vyetu

4.Sikweli kama fedha hizi zingejenga kituo cha mabasi mbezi,kwa kuwa kituo cha mabasi mbezi ilikikamilike kinahitaji billioni zisizopungua 31 wakati Fedha haramu za UDA ni kiasi cha billioni 5.8 ,hivyo kuzikataa fedha hizi hakuhusiki na ujenzi wa stendi ya mabasi,isipokuwa halmashauri ya jiji inakopa kiasi kikubwa cha fedha na kushirikiana na LAPF

5.Sikweli kwamba palikuwa na mpango wa kila halmashauri ipate mgao wa fedha za UDA ,hiyo haiwezi ikawa ni msimamo wa Baraza kwakuwa jambo hilo lilikuwa nimaoni binafsi ya mjimbe mmoja naye ni MEYA WA CCM, kama njia ya kuzima hoja kwa kutumia fedha,wala si kauli ya baraza zima la madiwani

6.Hivyo maamuzi ya jana yalikuwa ya baraza na kwa pamoja UKAWA tukapiga kura dhidi ya CCM waliokuwa wanataka kufunika kombe,dhidi ya UDA Zikawa kura 7 dhidi ya 6.mambo ya ukawa kuvutana ni media spinning tuh kwakuwa kikao cha ndani ya chama hakuna mtu asiye mjumbe wala waandishi walioingia.

"KAZI MLIYOTUTUMA TUNAENDELEA KUIFANYA"

Na
Senior Councilor Ubungo
BONIFACE JACOB
MJUMBE WA DSM CITY COUNCIL
 
Uchambuzi mzuri na asante kwa kutuambia kuwa madiwani wa ccm bado wanataka kupiga dili juu ya dili.

Samahani unaweza kufafanua kidogo kuhusiana na hiyo bajeti ya b.34 hiyo stand ingekuwa na ukubwa gani pamoja na vitu gani. Na je katika pitia pitia yenu vitu alivyopewa simon vilistahili kuwa kiasi gani
 
Jacob:

Unabeba dhamana kubwa sana katika nchi hii.Nina imani taarifa hii umeiandaa Kwa kutumia Computer.Ni vizuri ukawa unachukua muda kupitia tena(proof read) maandiko yako kabla ya kuyafikisha Kwa wasomaji.Ninafahamu una kazi nyingi lakini kufanya hivyo kutakusaidia kukujengea heshima Kwa wasomaji wako kuwa u mtu makini.
 
Utakatishaji Fedha bado upo na huu ni mfano wa kuhalalisha jambo lililokiukwa. Inauma kuona hata WAKUBWA wanabariki ufisadi
 
Safi sana Bro......

Naona familia ya aliyepita bado inaendelea kuwatesa watanzania kwa wizi na ufisadi.............

Uku UDA uku IPTL..........

Naona ukawa mliwekewa mtego ili ajenda 2020 ije iwe nyie ndio mafisadi mumeuza uda wakati serikali hisa zake zipo...........

Hongera sana wakuu kwa kugundua .......
 
Chadema tokea msafishe fisadi Lowasa hamna atakayewamini tena.

Kila kitu mnataka mchakato ili kuchelewesha maendeleo ya wananchi makusudi.
Mnapinga kila kitu hadi maendeleo ya wananchi!!!
 
Weka ukada pembeni angalia maslahi ya taifa. Kwa hiyo sababu mlifanya uzembe basi umezewe mate
 
Hili ni tatizo kubwa la upinzani wa nchi yetu. Ufisadi upo katika nchi yetu na suala la UDA ni miongoni mwake. Ukawa hamuwezi huo mchakamchaka. Kuna vita mnapoteza muda tu. Hivi hao wananchi hayo ni kipaumbele? Ukawa ya sasa hivi si ya ufisadi. Pambaneni na immediate needs za wananchi. Ajira, njaa, gharama za maisha na Uhuru wa habari. Mengine, hamna uwezo wa kupaza sauti.
 
Mambo mengine ukiyawaza ni kujipa depression na ma stress bure . Hii nchi viongozi ndio chanzo cha matatizo huku wakiendelea kulipana hela nzuri.. To mwisho watu wanazidi kukata tamaa
 
Chadema tokea msafishe fisadi Lowasa hamna atakayewamini tena.

Kila kitu mnataka mchakato ili kuchelewesha maendeleo ya wananchi makusudi.
Mnapinga kila kitu hadi maendeleo ya wananchi!!!
Wewe kweli hebu jibu hizo hoja za mh. meya!
Anayechelewesha ni nani kama sio hao ccm waliouza UDA kwa Simon group?
 
Hili ni tatizo kubwa la upinzani wa nchi yetu. Ufisadi upo katika nchi yetu na suala la UDA ni miongoni mwake. Ukawa hamuwezi huo mchakamchaka. Kuna vita mnapoteza muda tu. Hivi hao wananchi hayo ni kipaumbele? Ukawa ya sasa hivi si ya ufisadi. Pambaneni na immediate needs za wananchi. Ajira, njaa, gharama za maisha na Uhuru wa habari. Mengine, hamna uwezo wa kupaza sauti.
Njaa ipi mkuu wakati anayepaswa kutangaza Njaa na baa la njaa amesema hakuna njaa?
Sio kila kitu wanaachiwa UKAWA,hivi sisi kama wananchi tunachukua jukumu gani kukabiliana na hayo matatizo?

Uhuru wa Habari tumeambiwa kwa sasa hauna maana,mpaka nchi inyooshwe,sasa kipimo cha kunyooka nchi anacho mtu mmoja tu.

Tatizo ni kuwa sisi wananchi tumeachia kila kitu kwa UKAWA.

NB:Meya jitahidi sana kuhariri taarifa zako kabla hujazituma mitandaoni,haya makosa madogo ya spelling yanapunguza heshima.Hariri habari ndio uilete,Unaweza kuwa na ujumbe mzuri lkn ukashindwa kueleweka sbb ya "mwandiko"
 
Safiii sanaaa UKAWA kwa hili.. mm ni CCM, ila hili, madiwani wa CCM wa Dar hawako kwa maslahi ya umma, ila kwa maslahi ya mafisadi..

Hayo ndio nilitegemea toka kwa Mh. Rais afanye.. bahati mbaya sana sana, juzi kaniangusha vibaya sana sana.. UKAWA, pongezi sana, huu ndio UTAIFA, nilisema mm sio CCM wa NDIOOOOO... never ever...

UDA, sikuamini hata Mh. Rais kashindwa kulirudisha ktk mikono ya jiji hizo 51%, yaani Kisena alipe tshs. 5.8 bil apewe 51% ya JIJI..? How..? Kama maelezo ya Boniface Jacob hapo juu, HICHO NDICHO KILITAKIWA NA KILA MWANANCHI... kuwa HISA ZA JIJI ZOTE 51% ZISIUZWE, ZIRUDISHWE JIJI... NA HIZO TSH. 5.8 Bil.. apewe Simon Group, Kisena ni msukuma, hadi nikawaza kuna ukabila nn hapa..? sbb thinking is not ILLEGAL, hiki ndio kilio cha watanzania, ndiko hasa tulitaka mali ya UMMA, UDA, irudishwe mikononi mwa JIJI 51%.. sbb zile 49% bado ziko upande wa serikali... sio Kisena kulipia hisa..

Juzi Kkoo, ktk uzinduzi, sikujua vema, nilishtuka sana, kusikia Mh. Rais anasema hela hizo tsh. 5.8 bil manispaa za Dar, zinavutana kutumia, kuwa Kisena kalipa, TATIZO SIO KULIPA, TATIZO HISA ZOTE ZIRUDI JIJI 51%, wananchi hawataki UDA kuuzwa, hiyo ndio ISSUE..!! Jamanii, jamanii, nchi yangu hii..!!

UKAWA kwa hili nawapa pongezi, kwenye UKWELI DAIMA NITAPONGEZA, naomba UKAWA KWA HILI MTUTOE KIMASOMASO, mtuokoe, piganeni hadi hatua ya mwisho, ili UDA 51% ya JIJI zirudi, na hizo tshs. 5.8 bil arudishiwe Kisena.. piganeni kufa na kupona, tunaomba sana UKAWA.. kwa hili CCM mmeniangusha vibaya sana, sikutegemea hasa awamu hii, kweli ufisadi ni zaidi ujuavyo, ni kama kumuona malaika anageuka kuwa shetani..!! SIJALISHI MM NI CCM.. TAIFA KWANZA..!! TAIFA KWANZA..!! TAIFA KWANZA...!! TAIFA KWANZA..!!
 
Njaa ipi mkuu wakati anayepaswa kutangaza Njaa na baa la njaa amesema hakuna njaa?
Sio kila kitu wanaachiwa UKAWA,hivi sisi kama wananchi tunachukua jukumu gani kukabiliana na hayo matatizo?

Uhuru wa Habari tumeambiwa kwa sasa hauna maana,mpaka nchi inyooshwe,sasa kipimo cha kunyooka nchi anacho mtu mmoja tu.

Tatizo ni kuwa sisi wananchi tumeachia kila kitu kwa UKAWA.

NB:Meya jitahidi sana kuhariri taarifa zako kabla hujazituma mitandaoni,haya makosa madogo ya spelling yanapunguza heshima.Hariri habari ndio uilete,Unaweza kuwa na ujumbe mzuri lkn ukashindwa kueleweka sbb ya "mwandiko"
Jukumu la upinzani ni lipi?. Hawa ndio wanatakiwa wawe na Sera mbadala bahati mbaya ni afadhali ya jana. Hivi outcome ya hilo wanalotaka watapata? Pesa zitapangiwa matumizi.
 
Kifupi jana 27 january 2017 ilikuwa ni mara ya pili kwa baraza la jini DSM kupinga maamuzi ya uuzaji wa hisa za UDA

BARAZA LA CCM LILILOUZA UDA
lilifanyika 2012/2013 kufuatia taarifa iliyokuwa inaonyesha UDA inaendeshwa kwa hasara sana na hata muda mwingine fedha za mapato yanayokusudiwa haziji halmashauri ya jiji
Baraza hilo chini ya marehemu DIDAS MADABURI wa CCM na Majority CCM huku chadema wakiingia madiwani wawili tuh.

BARAZA LA 2015/2016 UKAWA Chini ya mstahiki meya ISAYA MWITA wakapitisha hoja ya kutengua na kutokutambua maamuzi ya kuuza UDA mnamo tarehe 2 may 2016
Jana ni mara ya pili baada ya miezi takribani saba ikipita hoja hiyo hiyo yenye mlengo uleule na watu wale wale walipaswa kufanya marejeo ya hoja ya je wanaafiki UDA kuuzwa au Hawataafiki? Na je kwa maana hiyo fedha zilizowekwa benk na "Purchaser" zikubaliwe kutumika kama njia ya kumaliza biashara ya uuzaji wa UDA.

HOJA ZA KUPINGA UUZAJI WA HISA ZA UDA KWENYE BARAZA MAY O2 2016 NA JANA PIA

1.Hapakuwa na maridhiano ya wanahisa kukubaliana kuuza kampuni ya UDA ambapo jiji na mwanahisa mwingine ni msajili wa hazina(Kwa niaba ya serikali kuu)

2.Hisa za halmashauri ya jiji ziliuzwa bila kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma ,ambapo simon Group waliuziwa kinyume na sheria inavyotaka,
hawakutangangaza wazi ili pawe na ushindani bali alialikwa binafsi tuh na wakamalizana naye bila ushindanishaji wa wanunuzi kama wenye nia wengine walihitaji.badala yake atunui alipataje taarifa kama Hisa za UDA zinauzwa.sababu hakuna tangazo lilotolewa rasmi.kama sheria inavyotaka

3.Hapakufanyika uthamini wa mali za UDA kujua kabla ya kuuza Hisa za UDA viwanja kama mbagala,gerezani kariakoo,kurasini,,majengo yote ya ofisi za UDA,mitambo ya UDA,na magari ya UDA,Brand ya neno"UDA",kafakana zote za kutenezea UDA,Kujua yalikuwa na thamani gani?

4.Mauzo ya hisa za halmashauri ya jiji hayakupata ridhaa ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa "TAMISEMI" kama sheria inavyotaka,kuwa kwanza ni lazima waziri husika alipaswa kuridhia.

5.kampuni ya UDA ilikuwa chini ya PSRC kama "specified companies" hivyo kabla ya uuzaji wa UDA palipaswa kufanywa mawasiliano na CHC (CONSOLIDATED HOLDING COOPERATION) hawa ndiyo wasimamizi wa mashirika ya UMMA kujua kama nao walikuwa na ripoti kuwa UDA ni hasara au la,badala yake wakarukwa na mauziano yakafanyika bila masiliano nao.

HIVYO MAAMUZI YA BARAZA YAKAWA KAMA IFUATAVYO

1.MAAMUZI YALIYOFANYWA NA BARAZA LILILOPITA KUHUSIANA NA UUZAJI WA HISA ZA JIJI JUU YA KAMPUNI YA UDA YAMETENGULIWA

2.FEZA ZILIZOINGIZWA KWENYE AKAUNTI YA HALAMASHAURI YA JIJI DSM KEA AJILI YA BIASHARA YA MAUZIANO YA HISA ZIRUDISHWE

3.KAMA SERIKALI KUU WATAHITAJI FEDHA HIZO KUZICHUKUA NA KUZITUMIA WACHUKUE TUH NI MAAMUZI YAO LAKINI BARAZA LA SASA LISITUMIE KABISA PESA HIZO KAMA KUHALALISHA BIASHARA HARAMU YA MALI ZA UMMA

MENGINEYO
1.Hii yumeisaida serikali inayopingana UFISADI lwamba hakuna ufisadi mzuri na mbaya wote ni UFISADI Kuwamakini na waandamizi au washauri wa Rais kwa maana wengine wanamslahi tofauti na UMMA

2.Kuweka KUMBUKUMBU sahihi kwa heshima waliyotupa wananchi kwa kuwa moja ya sababu ya watu wa Dar es salaam kuchagua UKAWA ilikuwa ni kukasirishwa kuuzwa kwa shirika lao la miaka MINGI kwa hila na UFISADI.

3.Ni heri kama serikali kuu watazitumia hizo fedha basi dhambi ya UDA haitokuwa juu yetu na vizazi vyetu

4.Sikweli kama fedha hizi zingejenga kituo cha mabasi mbezi,kwa kuwa kituo cha mabasi mbezi ilikikamilike kinahitaji billioni zisizopungua 31 wakati Fedha haramu za UDA ni kiasi cha billioni 5.8 ,hivyo kuzikataa fedha hizi hakuhusiki na ujenzi wa stendi ya mabasi,isipokuwa halmashauri ya jiji inakopa kiasi kikubwa cha fedha na kushirikiana na LAPF

5.Sikweli kwamba palikuwa na mpango wa kila halmashauri ipate mgao wa fedha za UDA ,hiyo haiwezi ikawa ni msimamo wa Baraza kwakuwa jambo hilo lilikuwa nimaoni binafsi ya mjimbe mmoja naye ni MEYA WA CCM, kama njia ya kuzima hoja kwa kutumia fedha,wala si kauli ya baraza zima la madiwani

6.Hivyo maamuzi ya jana yalikuwa ya baraza na kwa pamoja UKAWA tukapiga kura dhidi ya CCM waliokuwa wanataka kufunika kombe,dhidi ya UDA Zikawa kura 7 dhidi ya 6.mambo ya ukawa kuvutana ni media spinning tuh kwakuwa kikao cha ndani ya chama hakuna mtu asiye mjumbe wala waandishi walioingia.

"KAZI MLIYOTUTUMA TUNAENDELEA KUIFANYA"

Na
Senior Councilor Ubungo
BONIFACE JACOB
MJUMBE WA DSM CITY COUNCIL
Senior councillor vibaro vikishajaza akili
 
Back
Top Bottom