Serikali: Magari ya Jeshi la Polisi yaliyoingizwa kutoka India kuchunguzwa baada ya kugundulika kuwa na dosari

mtu watu

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,123
1,616
Dar es salaam : Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni ameagizwa kuundwa kwa kamati ya wataalamu kukagua kwa kina magari ya Jeshi la Polisi yaliyoingizwa nchini kutoka India baada ya kugundulika kuwa na dosari.

Naibu Waziri Masauni ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam baada ya kufanya ukaguzi wa awali wa magari hayo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli.

Magari hayo 173 ambayo ni mapya ya Jeshi la Polisi, yalibainika kuwa magari matano kati yake ni mabovu, na mengine yameshatembea zaidi ya kilimota elfu moja.
 
Naibu waziri Masauni amesema kamati hiyo aliyoiunda itachunguza utaratibu uliotumika kuingiza magari hayo pamoja na kupitia mkataba mzima kwani kumeonekana utata mwingi. Pia magari 5 kati ya 53 ambayo ni sawa na 10% yameingizwa yakiwa ni mabovu. Source ITV habari!
 
Kwahiyo sisi tufanyaje?
 
Back
Top Bottom