Serikali kuzalisha zaidi ya ng’ombe 300,000 kwa njia ya uhawilishaji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Serikali imepanga kuzalisha zaidi ya ng’ombe 300,000 kwa njia ya uhawilishaji ili kuongeza ubora wa mifugo na tija kwenye uzalishaji pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameyasema hayo jijini Mbeya alipokuwa anapokea dume la kisasa ambalo serikali imepewa na Kampuni ya Mbogo Ranches ya wilayani Mbarali katika Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu.

Amesema ng’ombe watakaozalishwa kwa njia hiyo wana uwezo wa kutoa maziwa mengi kuliko wale wa kienyeji na hivyo akasisitiza wafugaji kuchangamkia aian hiyo ya ng’ombe na kuachana na wale wa kienyeji.

Amesema Serikali inalenga kupunguza mifugo kuchungwa na kuhamasisha wafugaji kufuga mifugo ya ndani ili kupunguza migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

“Sisi kama Serikali tunaliona tatizo mbele ambalo linaweza kutukabili la upungufu wa maeneo kwa ajili ya kuchungia, kwahiyo tunawashukuru wenzetu wa Mbogo kwa kutupatia hili dume ambalo tunaamini litatusaidia,” amesema Waziri Ndaki.

Amewataka wadau wengine wa ufugaji kushirikiana na Serikali kupata mbegu bora za mifugo ili kuboresha hali ya ufugaji nchini na kuifanya sekta hiyo kuwa miongoni mwa sekta zinazoliingiza taifa fedha nyingi bila kuzaa migogoro.

Akikabidhi dume hilo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbogo Ranches, Pirmohamed Mulla amesema waliamua kutoa dume hilo kwa lengo la kuisaidia Serikali kupata mbegu bora za mifugo.

Amesema dume walilolitoa lina uwezo wa kuzalisha mbegu 30,000 kwa mwaka endapo litaishi kwa miaka sita huku akieleza kuwa katika shamba lao dume hilo lingekuwa na uwezo wa kuzalisha mbegu zisizozidi 150 katika kipindi cha uhai wake.

Ameongeza kuwa katika shamba lao uzalishaji wa mbegu wa dume hilo ni mdogo kutokana na kulitumia kwa njia ya asili ya kupanda lakini Serikalini litatumika kwa njia ya kisasa ya uhawilishaji ambayo alisema ina tija Zaidi.

Amesema dume hilo limekaguliwa na wataalamu na limeonekana kuwa na ubora wa hali ya juu na hivyo akaihakikishia Serikali kwamba kama litatumika vizuri kuna uwezekano wa kuzalisha mbegu nyingi Zaidi.

“Hili dume lina umri wa miaka mitatu na ndio umri sahihi wa kuanza kuzalisha, serikali ina wataalamu ambao watakaokamua mbegu za hili dume na kuzalishia mifugo mingine ambayo tuna uhakika wafugaji wakiitumia watafaidika Zaidi,” amesema Mulla.

Amewataka wafugaji ambao wanahitaji mbegu za ng’ombe hao wanaweza kuzipata kwenye ranchi mbalimbali zilizopo nchini na kwamba hata serikalini zinapatikana.
 
Na waziri mwenyewe anasema Uhawilishaji? Hii ni teknolojia gani? Halafu hiyo teknolojia inapunguzaje migogoro ya ardhi? Ina maana ng'ombe hao hawali? Hovyo kabisa!
 
Uhamilishaji ni njia nzuri sana kwa maana ya kupata mbegu bora na kupunguza magonjwa kwa mifugo
Hii njia sio ngeni mikoa ya kaskazini na huwa wanaitumia hii njia
Mikoa mingine wafugaji wanapambana hasa kupata ng'ombe breed zenye tija ya juu kwa maziwa na nyama kama simmental, fleckvieh, Angus n.k
Ni hatare sana kwakweli ila kama itafanikiwa hii mbinu aiseh itasaidia sana
 
Uhawilishaji ni njia nzuri sana kwa maana ya kupata mbegu bora na kupunguza magonjwa kwa mifugo
Hii njia sio ngeni mkoa ya kaskazini na Bwana wanaitumia hii njia
Mkoa mingine wafugaji wanapambana hasa wa ng'ombe wa maziwa kupata mbegu bora kama simmental, fleckvieh, Angus n.k
Ni hatare sana kwakweli kama itafanikia
Basi siyo uhawilishaji bali ni "Uhamilishaji" au Artificial Insemination.
 
Back
Top Bottom