Serikali kuwatimua wapiga debe Ubungo tutegemee nini?

Serikali kuwatimua wapiga debe Ubungo tutegemee nini?

Kazi nyingine ni laana. Kazi ya upiga debe imelaaniwa! Ni kazi gani hiyo ambayo huyo unayetaka kumuhudumia hakutaki? Tafuteni kazi nyingine I see!
 
Wale jamaa walipelekea abiria kupoteza mizigo yao, ukifika pale watakugombea na mpk vitu vinapotea, walitakiwa kuwaondoa mda mrefu sana!
Wanakera sana wale jamaa, niliona tukio moja kuna mama alikuwa anasafiri bas wale jamaa wakamgombea weeee! Mwisho wa siku yule mama akajikuta yupo kwenye ngorika ya Arusha, mtoto wake kapakiwa kwenye Dar lux ya Mwanza, mzigo umeshafika kwenye Abood ya mbeya, Beki 3 kapakiwa kweny buti la zungu ya Mtwara. mama wa watu akabaki analia tu hajui la kufanya
 
Waende salama acheni kuipa serikali lawama za ajabu koz mpaka mtu unatoka nyumbani kwako na begi lako unafika ubungo huezi kuwa hujui una kwenda wapy. Sasa wale jamaa wanavyo pokea mtu ni kama hujijui kama una safiri wana kushika shika kila mahali kitu ambacho sio sawa.
 
Hao ni wapiga kura, waachwe bila kubughudhiwa.... sijui kwanini natarajia tamko kama hili.[emoji848]
 
yan watu mmekazana wanaleta kero kero.. qan hiyo serikari yenu ina kero ngap kwa sisi wananchi wake na bado hamkomi kuipenda, mwendo kasi kero ukienda hspital kero polis kero na bado mnawsujudu...
mpia debe tu ambaye uawezo wa kumjibu kuwa sisafiri akakuacha uendelee na safar yako ety ndo anakero mpka afukuze...
 
Zoezi Hilo Halijawahi Kufanikiwa, Acha Tuone Wakati Huu
 
Habari,
Ni kawaida kuwakuta wapiga debe ndani ya kituo cha mabasi ya mikoani ubungo,ambao huanzia kituo cha river side mpka ndani ya kituo cha ubungo.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwapeleka abiria kwenye mabasi husika na hata kuwasaidia kubeba mizigo ili kupata riski ya chochote kutoka kwa abiria hao

Lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani uongozi wa kituo pamoja na askari wametumika kuwatimua kutokufanya shughuli hiyo

Je, Serikali imewawekea njia mbadala ya kujiingizia kipato au kipi tukitarajie kutoka kwa hawa watu zaidi ya 800 baada ya kukoseshwa kazi yao ambayo ilikuwa inawasaidia kuingiza chochote kitu?
Hawawezi kuwaondoa hao watu,ni kama biashara ya machangudoa hauwezi kuimaliza,watazuia kwa muda kisha watarudi tena kama WATEULE.
 
Bomu la ukosefu wa ajira linaendelea kusukwa. Muda si muda litaripuka.
 
Habari,
Ni kawaida kuwakuta wapiga debe ndani ya kituo cha mabasi ya mikoani ubungo,ambao huanzia kituo cha river side mpka ndani ya kituo cha ubungo.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwapeleka abiria kwenye mabasi husika na hata kuwasaidia kubeba mizigo ili kupata riski ya chochote kutoka kwa abiria hao

Lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani uongozi wa kituo pamoja na askari wametumika kuwatimua kutokufanya shughuli hiyo

Je, Serikali imewawekea njia mbadala ya kujiingizia kipato au kipi tukitarajie kutoka kwa hawa watu zaidi ya 800 baada ya kukoseshwa kazi yao ambayo ilikuwa inawasaidia kuingiza chochote kitu?
Nadhani ni muda muafaka sasa iwamulike na wale wanaozagaa hovyo mabarabarani kuuza bidhaa, wakiwemo waliogeuza vibanda vya kusubiria wasafiri kuwa maduka yao binafsi. Dar es Salaam ni jiji pekee Afrika Mashariko lisilo na utaratibu. Kampala na Nairobi hakuna upuuzi huu.
 
Waliambiwa wanunue vitambulisho vya wajasiriamali ili wasisumbuliwe na mgambo
 
Kwani hiyo kazi ya kwanza serikali iliwatafutia?
 
Wanakera sana wale jamaa, niliona tukio moja kuna mama alikuwa anasafiri bas wale jamaa wakamgombea weeee! Mwisho wa siku yule mama akajikuta yupo kwenye ngorika ya Arusha, mtoto wake kapakiwa kwenye Dar lux ya Mwanza, mzigo umeshafika kwenye Abood ya mbeya, Beki 3 kapakiwa kweny buti la zungu ya Mtwara. mama wa watu akabaki analia tu hajui la kufanya
Hahahaha. Nini kiliendelea mkuu kama ulishuhudia hadi mwisho?
 
Tena serikali iwatoe wote hata stendi za mikoani yani wana kero sana
 
Hawa waweza outlawed nchi Zima. Hawa ni kero si ubungo tu bali hata huko uswekeni.

Hawa Sukima ndani na wengine wamejibatiza ati ni ma agent. Hamna lolote bila wao hata nauli zitashuka.
 
  • Thanks
Reactions: A3M
Sipingi wasijitafutie rizki Ila wengi wao wana agenda nyingine, uwizi, bangi, ..sasa hao ndio watawakwamisha wenye nia nzuri ya kujitafutia rizki kuweza kusaidia familia zao
 
Back
Top Bottom